SoC02 Maono ya Kapanda

SoC02 Maono ya Kapanda

Stories of Change - 2022 Competition

Kapanda9

New Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
1
Reaction score
0
KILIMO
Sekta inayolisha na kuleta neema kwa mabilioni ya watu imeendelea kupata changamoto za kila aina, Mungu si Athumani, bado imeendelea kutulisha na kutupa afya na ustawi wetu wa kila siku, wanadamu na viumbe vinavyotuzunguka.

Kilimo ni ajira kale sana, miongoni mwa ajira za kwanza za binadamu, ukiachilia mbali ile ya ufugaji, sekta hizi zipo sambamba katika jahazi moja na hazijawahi kuleta tija inayostahili.

Miongoni mwetu wengi tumetoka katika familia ambazo kama hazilimi, basi ndugu wa karibu wanashughulika na kilimo, na kwa tuliopata nafasi ya kutembea na kutembelea au kuishi katika miongoni mwa familia zilizofanya kilimo tumepata nafasi adhimu sana kuona Nyanja na purukushani za kila aina zinazojiri katika kilimo, tena kilimo dhalili cha jembe la mkono.

Afrika, kwa jumla, ukigusia nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, najaribu kutafuta ukusini wa nchi ya Ghana kutokea mahali Jangwa la Sahara lilipo, sijauona bado ila ndio hivyo, wanajiografia na wanamajumui kindakindaki wameshatutanabaishia hivyo, nimetania tu, la hasha sina nia ya kupingana nao.

Asilimia 60% ya ardhi ni inakalika, yani ni maeneo ambayo yanaweza kutumika kwa shughuli mbali mbali, kujenga makazi, viwanda au kuanzisha lile shamba kubwa la matunda na kufanya kilimo cha umwagiliaji. Afrika bado ina nafasi kubwa na inafaa kutumia fursa hii kwa ajili ya manufaa ya binadamu wote na dunia kwa jumla.

Tumepata mabadiliko ya tabia nchi, wajibu wa kuendea shughuli hizi tukibeba ajenda pia ya kilimo chenye uhifadhi na kulinda hali ya hewa ili tunachotafuta katika ardhi kisiwe sumu kwa upande wa pili, na kuleta athari na shida bali iwe sababu ya kushiba na kuweka akiba, na kuchochea viwanda na sekta zingine kuingia hapo kuchagiza harakati hizi na kuzalisha bidhaa za muda mrefu pia, ikibidi kwa kupunguza gharama ili basi mfuko wa simenti usiendelee kuwa juu zaid ya mfuko wa kiroba cha sembe hahahaha!

Bara hili, asikwambie mtu, na unayesoma andiko hili, zingatia hili, ndilo bara lenye vijana wengi kwa asimilia walau 70% ya vijana wote duniani, naam, hujakosea kusoma, kifupi ni kwamba vijana wengi duniani wenye umri wa angalau 19 hadi 35 wapo katika ardhi hii takatifu, Afrika. Lahaulaaa, ni mtaji mkubwa sana huu.

Lakini swali la msingi limebaki kua, je ni kwa faida gani basi vijana hawa watafaa jamii ya waafrika na dunia kwa jumla. Vijana wengi hawaoni fursa katika hili, au la, wamekua wakifanya kwa mzaha, lakini pengine ni sera na muundo wa tasisi na seriakli zao wanamoishi zinashindwa kuratibu kilimo chenye tija ili kuwaonesha na kuwaongoza kufanya sekta hii ikawa rasmi yenye faida endelevu kwa ustawi wa ardhi, chakula na sekta zingine za kibiashara!

Nitawapa habari ya kijana mmoja, Anaitwa Kapanda na maono yake juu ya kilimo, inawezekana ukapata jambo moja au mawili lakini naamini utachukua na kufanyia kazi katika eneo lako, iwe shambani au katika korido za wizara ya kilimo pale makao makuu ya nchi ukaweka mikakati na sera za muda mrefu kunusuru na kuchagiza sekta hii.

Maono ya Kapanda:
Kapanda alikua ni kijana mpole na mwenye kuchunguza, utotoni alipata mafunzo ya awali ya kusoma tarakimu na silabu akiwa nyumbani, basi akiwa na miaka 5, aliweza kuunganisha herufi na kusoma gazeti. Aliwashangaza familia yake, ni kijana yatima aliyekua analelewa na baba yake mdogo kipenzi. Walipoona majabu haya, moja kwa moja akapelekwa Shule, akaanza darasa la kwanza. Kwa utajiri wa maeneo waliyoishi, shule yake ilikua pembezoni mwa bahari, fukwe la pwani ya Bagamoyo.

Kapanda alipenda kuona rangi za buluu za maji ya bahari, mawimbi na harufu ya pwani ilimfanya apende sana kwenda maeneo yale kila atokapo shule kabla ya kurudi nyumbani, ikawa ndio tabia yake. Ikafika wakati ikawa anatoroka shule anakwenda baharini kushinda huko.

Baba yake mdogo akaona kuna haja ya kufanya mageuzi, Alisafirishwa kwenda mkoani Morogoro kwa baba yake mdogo mwengine, wakasema saaafi, tumepatia hapa kijana atasoma, atakaa mji kasoro bahari, na kweli ikawa hivyo.

Katika makuzi yake, akiwa darasa la tatu, shule waliyokua wakisoma na ndugu zake ilikua na shamba la mahindi, yani uji wa shule ulitoka shambani, utakulaje ambacho hujazalisha, ndio maana halisi na kivitendo ilitekelezeka pale.

Pamoja na shamba la shule, ilikua ni ratiba kila ifikapo siku za wikiendi au wakati mwingine siku za jioni, family yote kwa pamoja ilikwenda shambani katika mashamba ya familia. Walijishughulisha na kilimo cha Nyanya, Mpunga, Mahindi, Maharagwe na wakati mwingine wakalima miwa.

Sehemu kubwa ya walicholima kilikua kwa matumizi ya nyumbani, na walilima mbogamboga pia. Walikula, waligawa pia kwa ndugu waliopita kusalimia na walipokuwa wakiondoka, ilikua ni neema kwao kubeba magunia walau matano ya mpunga na madebe ya mahindi. Ilikua ni jambo la kawaida sana kupelekeana vyakula na ilikua ni sehemu ya utamaduni kwa miaka hiyo.

Kilichomshangaza Kijana Kapanda, kadri anavyokua ni kuona kilimo kile hakina tija kwao, uzalishaji ulikua mwingi lakini sehemu kubwa ya mazao ni kula, kugawa na mengine hasa kipindi cha msimu wa nyanya, ni kusaza na nyanya kuharibika. Ilikua ule kachumbari hadi utoke minyoo au ziozee shambani na kutupwa.

Kilimo ambacho kimekua kiini chamabadiliko ya sekta kadhaa, kimeachwa nyuma, kilimo kimekua cha kwenye nadharia na mikakati isiyokua na viunganishi kuunganisha sekta zingine kwa asilimia 100%.

Kilimo kisipokua na sera endelevu, jembe la mkulima litaendelea kila siku kuleta chakula, lakini wakati mwingine kutokana na mambo na changamoto kadhaa za hali ya hewa, huyu anayetumia jembe la mkono kuna siku atashindwa kuinua jembe ili achimbe muhogo akachemshe.

Ni lazima kwa sisi vijana, kwa wanataaluma ya kilimo na serikali, kutatua changamoto hizi, kilimo ni ajira kale, ni ajira ya kimungu pale alipomwambia Baba yetu wa Imani Adamu akajitafutie, kilimo ndio ilikua ajira yake na msingi wa utafutaji wa mwanadamu. Ni haki yetu ya kuzaliwa tuliyopewa na Mungu, ni dhulma kwa jamii yetu na kwa vizazi na dunia kama hatutumii nafasi hii adhimu.

Kuzalisha ajira chakula, akiba ma kuhakikisha hakuna binadamu atalala na njaa kwa siku moja, ndio, inawezekana. Ni wajibu wetu kuleta mabadiliko katika kilimo, wajibu wa kukuza na kulima kwa ustawi wa watu wetu, viwanda vyetu na dunia na ardhi yetu tukufu.

Ahsanteni, tufanye Tafakuru Pamoja!
 
Upvote 0
Back
Top Bottom