Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Mwangaluka! Mwakaata! Mwagona! Mwaghona! Mughonile! Mapembelo! Kamwene! Ukurasa wa 1
MAONO YA KUENDELEZA NA KUPENDEZESHA JIJI LA MBEYA
“When it comes to innovating big ideas and realising them, the sky is the limit” “Suala la kuibua fikra pana na pevu na jinsi ya kuzitekeleza, huwa halina ukomo”
1. Utangulizi
Naamini ni busara zaidi kutangulia kuwapongeza wakazi wa jiji la Mbeya kwa jitihada walizofanya na wanazofanya siku zote kulijenga jiji. Wana Mbeya wengi hujituma sana, si tu katika kilimo, bali pia katika ujenzi wa nyumba bora, huku wake kwa waume wakifanya biashara kwa juhudi kubwa.
Na kwa upekee kabisa, niwe mwingi wa fadhila kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Jiji kwa kusimamia kidete uboreshaji wa barabara za jiji.
Na kwa kuwa mimi pia ni mpenzi wa kandanda, naipongeza Halmashauri ya Jiji kwa kupata timu nyingine itakayocheza Ligi Kuu. Aidha, niseme wazi kuwa kila ninaposafiri kuelekea au kutokea nyumbani Mwakaleli, huwa navutiwa sana kuvinjari na kuangalia mandhari nzuri ya jiji la Mbeya wakati tunapopanda Igawilo au kuteremka Iwalanje kuelekea Uyole.
Jiji la Mbeya ni bonde (trough) lililopo katikati ya miinuko mirefu ya milima mithili ya matuta makubwa yanayoanzia Lwanjilo na Kawetele kuelekea Njelenje kupitia Utengule, kwa upande wa kaskazini; na kuanzia Iwalanje/Uporoto kuelekea Mbozi kupitia Songwe, kwa upande wa kusini.
Miinuko ya milima hii ni mapambo ya ajabu kabisa na vilele vyake ni vivutio tosha kwa ajili ya michezo na utalii wa kupanda na kushuka milimani (mountaineering sports and tourism). Endapo nyumba nyingi, barabara na
bustani za miti zingekuwa na mpangilio mzuri, ni dhahiri kwamba jiji letu lingependeza na kuvutia zaidi. Japo si mkazi wa jiji la Mbeya - na hata sina nyumba au kiwanja, lakini naona fahari na uzalendo kutoa maono yangu
namna ya kuliendeleza na kulipendezesha zaidi jiji letu la Mbeya.
Na Gwandumi Gwappo Atufwene Mwakatobe
(Mshauri Elekezi Huru na wa Kujitolea)
P.O. Box 589, Mwakaleli, Busokelo, Mbeya
baruapepe: gwappomwakatobe@gmail.com
Tafakuri Hii Ilifanyika Nikiwa Juu ya Mwinuko wa Uyole Kuelekea Iwalanje: Februari 2, 2013