Maono yangu na kesi ya JKT na Uzalendo

Maono yangu na kesi ya JKT na Uzalendo

hahaha always done

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
1,126
Reaction score
1,973
kwanza nina imani ndogo na uzalendo unaoenda kujengwa kwa vijana huko jkt,,kipindi cha ujamaa walifanikiwa kwa sababu babu aliwabana kwenye kumiliki mali,,wote tukawa sawa, hata ukiiba huwezi kununua chochote na hata ukinunua labda uchimbie chini kama watu flani walivyofukia matrekta huko moshi,kwa hiyo watu wakawa waaminifu ili kuepuka hadha hizo,na wakaitwa wazalendo,,,,vyuo vikuu walikuwa wachache tena wenye maisha yanayofanana(umaskini),,,utagoma vipiii,,,urudi maskani eti umefukuzwa chuo kwa kugoma wazazi wenyewe wana imani kubwa na chama cha babu ko uzalendo ukaendelea kuwepo,,,,alafu hata viongozi walikuwa hawana mambo mengi,,watoto wao tulisoma nao kwenye shule za kijiji,,leo hii mtoto wa flani anasoma nje kuanzia la kwanza hadi phd akija anapewa wizara afu mnasema jkt itawajenga kiuzalendo,,,

Kweli niwe mzalendo ktk mazingira magumu kama haya, na kwata juu afu mwananchi mwenzangu kala bata mwanzo mwisho huko kwa obama na bado nikigoma mnasema sina uzalendo niende jkt,,,ninachoona mimi,, siku vijana wakifuzu jkt wakaingia chuo,,ukatokea mgomo ,,,itabidi waje makomando kutuliza huo mgomo,,mana hayo mabomu vijana watakuwa wameyajua,hizo risas vijana watakuwa wamezizoea,,

Alafu neno uzalendo linaweza likawepo kwa staili ya ubabe mana wote ni askari,,na nina imani migomo katika nchi ya kibepali isiyotenda haki ni kawaida,,wakitaka uzalendo mafisadi,,kutokuwepo kwa usawa katika maisha ,dharau vikomeshwe na si huko jkt walikojidanganya,zaid vyuoni kutakuwa uwanja wa vita mabomu ya machozi yatakuwa outdated,,

Itabidi waje na vifaru tena, na kwa taarifa hata waloenda jkt enzi hizo wote ndo wenye kashifa za ufisadi siku hizi,,,lbda waseme tunawafunza ukakamavu na wasiende ndani sana mana haitafaa hata kwa ukakamavu
 
Back
Top Bottom