Maonyesh ya sababa 2008 na kasheshe zake

Mhache

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2008
Posts
345
Reaction score
25
Maonyesho ya sabasaba ya mwaka huu yalionyesha ubora zaidi ya yaliyotangulia. Tatizo ni jinsi ya watu kuingia uwanjani hapo ili kujionea biashara zilizoletwa kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na nje ya Tanzania. Lengo la makampuni mbalimbali na mashirika kuleta bidhaa ni ili kujitangaza.

Mimi binafisi ni mdau wa biashara ila nilishindwa kuingia uwanjani siku yenyewe ambayo ni tarehe saba kwani watu walikuwa wengi mlangoni wakigombea kuingia uwanjani. Ninashauri pawepo na utaratibu wa watu kukata tiketi sehemu nyingine na si lazima iwe siku hiyo ya maonyeho ili kupunguza msongamano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…