Maonyesho ya Bishara za Wajasilimali mikoa mbalimbali

Mapfa A

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2015
Posts
250
Reaction score
259
Habari wakuu,

Mimi ni mjasiliamali mdogo, ningependa kufahamu jinsi ya kujua mahali na tarehe ambapo hufanyika maonyesho ya kibishara ya mara kwa mara (tofauti na yale maonyesho ya kitaifa kama saba saba, nane nane n.k).

Ningependa kuwa nashiriki na mimi kuonyesha bidhaa zangu ila nakosa namna ya kujua mahali na tarehe husika.

Kwa mfano utakuta maonyesho ya kibishara yanafanyika mkoa fulani, au ndani ya DSM unakuta kuna kumbi wanafanya hayo maonyesho n.k, je, taarifa hizi zinapatikana wapi?

Natanguliza shukurani wakuu.
 
Kuna online platform naikamilisha mtaweza kuonesha ukiwa popote na kupewa oda .

Utapiga 0713 039 875 kuwahi oda
 
Mengi hayatangazwi ipasavyo utashtukia tu yameshaanza. Jichanganye na wajasiriamali wazoefu utapata taarifa
 
Nenda SIDO watakwambia kila kitu
 
Jiunge na vyama mbalimbali vinavyohusiana na shughuli unazozifanya au vyama vya kijinsia hali etc, ukilipa ada wanakuadd kwenye list, vyama hivi hupewa mialiko na organizers na wao hutoa mialiko Kwa wanachama wao pamoja na taratibu za kushiriki.

Kama ni mfanyabiashara Kuna TCCIA.
Kama ni mkulima Kuna TAHA,
Kama unadeal na viungo Kuna TASPA,
Kuna SIDO,
Kama ni mdada kuna women chamber of commerce
TAMWA
Mama Anna Mkapa foundation na mengi mengineyo.
 
October 5 Hadi 10 maonesho makubwa Kibaha maili moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…