Mapacha : Mapenzi Na Usaliti.

Darcityconfidential

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2015
Posts
351
Reaction score
367
"Sheila amka, we Sheila". Ni sauti aliyoisikia Anita akiwa anapata fahamu baada ya usingizi Mzito wa saa kadhaa akiwa katika lodge Moja iliyopo maeneo ya Mbagala, Saba saba kwa Mpili. Sheila anaamka akiwa na wenge kichwani kutokana na kunywa pombe kali usiku wa siku iliyopita ghafla anashtuka baada ya kujikuta yuko uchi wa mnyama kitandani na kuonyesha dhahiri kutokujua nini kiliendelea usiku wa jana katika sherehe ya kuzaliwa ya rafiki yake Penina. " Unaonekana bado unausingizi sana, mimi naondoka. nimekuachia pesa hapa juu ya draw utapomaliza kupumzika uende nyumbani kisha utanipigia simu". Ilikua ni sauti ya kijana mtanashati alionekana kuwa na nidhamu ya hali ya juu. "okay sawa". Anita anaitikia kujikaza kutoonyesha haelewi kilichotokea na kujigeuza kisha kuigiza kama amelala. Kijana anatoka na kuondoka akiashiria kuwahi mahala flani muhimu .


Anita anakurupuka kitandani na kutafuta ilipo simu yake ya kigachani na kumuendea Penina hewani, simu inaita mara kadhaa haipokelewi, Anita anajaribu kupiga kwa mara ya sita anapokea Penina, "haloo". Anita anaongea kwa jazba, "uko wapi Penina?, Mi nimefikaje hapa nilipo?, huyu mkaka nilie lala nae ni nani?". "Anita nipigie badae kidogo mi bado nimelala". Anajibu Penina kwa sauti nzito iliyoonyesha bado yuko kwenye wimbi la usingizi mzito. "We penina hivi...". Kabla hajamaliza sentensi Penina anankatisha "Sikia we tangulia nyumbani nikirudi nitakueleza kila kitu sahivi siwezi kuongea anita, badae". Kisha anakata simu. Anita anatafuta nguo zake zilizo kuwa pembezoni mwa kitanda anavaa kisha anachukua pesa taslimu shilingi elfu thelathini zilizowekwa juu ya draw na kijana alietoka hapo ndani kama dakika kumi zilizopita na kuanza safari ya kurudi nyumbani kurasini.


Ni nyakati za alasiri mnamo saa tisa Anita anasikia Penina anamuomba amfungulie mlango, Anita anaamka kwa haraka na kufungua mlango, anaingia Penina akiwa na vifurushi vya mahitaji ya kuandaa chakula vinavyoashiria alipitia sokoni akiwa anarudi nyumbani. "Vipi besti za hapa nyumbani?", Penina anamuuliza Anita,
"salama tu dear, ila nimekusubiri kwa hamu kama hufiki maana sina hata amani". Penina anacheka kisha anamuuliza Anita kwa utani "presha haijashuka kweli?". Wote wanacheka kisha Anita anaonyesha msisitizo kutaka kujua nini hasa kiliendelea jana usiku. Penina anamueleza, "yule mshkaji ni rafiki yangu tulisoma wote wote o-level Mbeya. Jana alipokuona alikupenda nikamwambia aje tu akueleze ila wewe nahisi ulikua umelewa maana niliongea nae leo mchana akaulizia sheila, kumbe wewe jana ulimdanganya jina!". Penina anacheka na Anita nae anacheka lakini kicheko cha Anita ni kumfurahisha tu rafiki yake Penina na wala si amani ya moyo aliyokua akiitegemea. "Sasa ilikuaje nimelala nae ?" Anita anauliza. "Muda wa kusepa ulipofika wewe ulimng'ang'ania sana Fred kwavile namimi nilikuwa na shemehi yako Leonard nikaona nikuache uende nae kwakuwa nayeye Fred alishaniambia amekupenda". Penina anamjibu Anita. Penina akionekana na uso wenye maswali mengi anamtandika tena swali Penina, "Na ni kwanini Ameniachia pesa? ". Penina anacheka sana kisha anamjibu kwa kunuuliza swali, " kwani we ulitaka umpe bure?". " ahh wewe Penina sio hivyo bhana, mi kwanza sijiuzi, Pili hajanifanya chochote". Anita anajibu. "Unanificha Anita, au sio? ". Anita anamweleza Penina kuwa ni kweli Fred hamkumfanya chochote lakini alimpa pesa taslimu tshs 30000 anamuhakikishia kuwa amejikagua na hakufanyiwa chochote. Usiku unaingia baada ya kupika na kupata chakula cha usiku simu ya Penina Inaita kumbe ni Fred alipiga kuuliza kama sheila amerudi salama nyumbani maana alisave namba yake kwenye simu ya Anita lakini Anita hakumtafuta. Penina anacheka kisha anamwambia yupo salama na kumkabidhi Anita simu aongee na Fred. "Haloo sheila Mambo vipi ?", Anita anaitikia kisha anacheka Fred anapomuuliza mbona unacheka Anita anajibu, "Nahisi pombe jana ilizidia, Mimi hata siitwi Sheila, jina langu ni Anita". Fred anasema alihisi tangu jana kuwa alidanganywa jina, wanaongea kwa dakika kadhaa kisha Fred anamueleza kuwa alisave namba yake kwenye simu kwa jina la Fred kwahiyo kesho akipata Muda amjukie hali, Anita anaafiki kuwa atafanya hivyo kisha wanatakiana usiku mwema na kukata simu.



Saa ya muito inapiga kelele saa 12:00 alfajiri siku ya jumapili, Anita anaamka tayari kwaajili ya kujiandaa kuelekea kanisani. Kanisa la katoliki lilipo temeke, Anita anatafuta usafiri na kuelekea ibadani. Anarudi kutoka kanisani mida ya saa tatu asubuhi akimkuta Penina bado amelala. Anaandaa chai na kumuamsha rafiki yake na kumkaribisha chai. Baada ya chai wote wanafanya usafi kwaajili ya kujiandaa na wiki inayo anza kesho. Wakiwa wamepumzika Anita anapata wazo la kumpigia simu Fred na kumjulia hali, Fred anafurahi na kumwambia kuwa jioni atakuwa na muda hivyo kama hatojali awatembelee yeye na Penina wanapoishi, Anita na Penina wanashauriana kwa sekunde kadhaa kisha wanaafikiana kuwa Fred awatembelee jioni ya saa kumi. Anita anapagawa na kuanza kuhaha kwa kutojua ni nguo gani atavaa, Penina anamcheka na kumtania kuwa ameshazama kwa Fred(ameshampenda Fred), Anita anajaribu kukataa lakini Penina kwa uzoefu wake anajua tayari kuwa Anita ameshautayarisha moyo wake kwa Fred.


Itaendelea...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…