Mapambano bado yanaendelea

Mapambano bado yanaendelea

Uhuru24

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2015
Posts
4,112
Reaction score
4,361
BBC News Swahili

menu

Wanamgambo wanne wa Al Shabab wauwawa katika shambulizi la uwanja wa ndege

05 Januari 2020



[https://ichef]

Image captionUwanja wa ndege wa Manda, uliopo Lamu

Kundi la kigaidi la Al Shabaab limefanya shambulio katika uwanja wa ndege wa jeshi unaotumiwa na majeshi ya Marekani na Kenya eneo la Lamu, kusini mashariki mwa Kenya.

Kundi hilo la kigaidi la mtandao wa Al-Qaeda limesema kuwa tukio hilo halina uhusiano wowote na malumbano yanayoendelea kati ya Iran na Marekani.

Jeshi la Kenya limethibitisha kutokea kwa shambulio hilo katika uwanja wa ndege wa Lamu.

Msemaji wa jeshi la Kenya amesema kuwa wameweza kudhibiti shambulio hilo na wamekuta miili minne ya wanamgambo wa Al Shabaab.

[https://ichef]

Image captionMji wa Lamu, kusini mashariki mwa Kenya

Al Shabaab walikuwa wanajaribu kuelekea kambi ya karibu inayotumiwa na Marekani na jeshi la Kenya.

Wakazi wa eneo hilo wameripoti kuwa walikuwa wanasikia milipuko na baadae milio ya risasi.

Moshi mzito ulionekana katika eneo la tukio.

'Tunataka kuonyesha machungu na maumivu tuliyonayo'Watu watatu wauwawa katika shambulio la kigaidi Kenya

Uwanja wa ndege wa Lamu umefungwa kwa muda usiojulikana.

Mashambulizi hayo yamesababisha madhara kiasi gani?

Image copyrightAFP[https://ichef]

Image captionAl Shabab wamefanya mashambulizi kadhaa ya kikatili Afrika Mashariki

Taarifa zinasema kuwa ndege mbili , helkopta mbili na magari kadhaa yaliharibiwa katika shambulio hilo.

Al-Shabab walidai kuwa kuna vifo vingi na majeruhi wa vikosi vya Marekani na wanajeshi wa Kenya hapo.

Jambo ambalo Christopher Karns, msemaji wa Kitengo cha Jeshi la Marekani Afrika amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa huo ni uzushi wa kukuza mambo.

Aidha hakufafanua zaidi taarifa hizo, AP imeripoti.

[https://ichef]

Image captionManda ni sehemu ambayo jeshi la Marekani utumia kutoa mafunzo ya kijeshi na kikosi kinachotoa usaidizi wa kukabiliana na ugaidi Afrika Mashariki

Kambi hiyo ilikuwa na wamarekani wapatao 100.

Ikumbukwe kuwa mwezi Juni 2018, Komando wa Marekani aliuwawa nchini Somalia wakati wa shambulio la al-Shabab.

Marekani ilianza operesheni dhidi ya wanamgambo tangu rais Donald Trump aingie madarakani 2017.

Marekani ilifanya mashambulizi mengi zaidi ya anga nchini Somali mwaka 2019 zaidi ya miaka ya nyuma.

Hali ya kiusalama katika fukwe za Manda ni imara.

[https://ichef]

Siku mbili zilizopita kundi la kigaidi la Al-Shabaab lilihusika na mauaji ya watu watatu katika basi katika eneo la Lamu.

Na wiki iliyopita kundi hilohilo la kigaidi lilihusika na shambulio lililouwa zaidi ya watu 80 huko Mogadishu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Mogadishu: Bomu lililotegwa ndani ya gari lawaua watu76 Somalia

28 Desemba 2019

Copyright [emoji2398] 2020 BBC. BBC Haiwajibiki kwa taarifa kutoka tovuti zisizo zake.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
prince mrisho com,
Marekani ni kikwazo cha usalama wa dunia.
Anatengeneza makundi ya kihafidhina na kuyauzia silaha kisha anaingia vitani kusaidia upande wapili,
 
Back
Top Bottom