SoC01 Mapambano dhidi ya ukosefu wa ajira

SoC01 Mapambano dhidi ya ukosefu wa ajira

Stories of Change - 2021 Competition

blessideal

Member
Joined
Jan 19, 2020
Posts
5
Reaction score
2
UKOSEFU WA AJIRA
Ukosefu wa ajira ni miongoni mwa matatizo ambayo yamekua yakijitokeza miongoni mwa vijana katika jamii ya Tanzania na Afrika.Ukosefu wa ajira umekua ukipelekea Ongezeko la ajira zisizo rasmi mfano Wizi,Kuuza madawa ya kulevya na mengineyo.Zifuatazo ni baadhi ya mbinu ambazo zinaweza kumkwamua kijana kutoka kwenye wimbi la kutokua na ajira rasmi.

1.Kuboresha mifumo ya kiutawala na kuweka usawa kati ya vijana na wazee katika uongozi; Vijana wapate nafasi za uongozi ili waweze kuwa kiungo mhimu kati ya Serikali na vijana hii itasaidia serikali kutambua nini hitaji la vijana katika wakati husika.Hii pia itasaidia vijana kufikisha hoja za msingi kwa serikali kupitia vijana wenzao waliopo kwenye uongozi ijapokua tumeona hili likitokea kwa baadhi ya vijana wa Tanzania kupewa nyadhifa kama Ukuu wa wilaya lakini bado hitaji ni kubwa ukulinganisha na idadi ya wazee walioshika uongozi wa juu.

2.Kuboresha mifumo ya TEHAMA; TEHAMA ni Teknolojia ya habari na mawasiliano, Wakati teknolojia inakua kwa kasi duniani hapa Tanzania hakuna mifumo wezeshi ya kiteknolojia hata kama ipo basi haikidhi mahitaji ya watu wote.Hivi karibuni tumeshuhudia ongezeko kubwa la watumiaji wa mitandao Tanzania hatupo nyuma sana lakini mifumo yetu ya kiteknolojia ni duni sana haimsaidii mtu kupata kipato bali inamkandamiza kwa mfano masuala ya kuanzisha kodi kwenye mitandao ya Youtube,Website,blogs na Tozo za miamala.Wimbi kubwa la vijana walianza kujitokeza kuanzisha blogs,Websites na Youtube channels kwa lengo la kujipatia kipato lakini serikali ikaweka kodi ambayo vijana wengi walishindwa kulipa na kupotelea mitini.Tozo za miamala pia limekuja kua tatizo kwa vijana ambao walijiwekeza kupitia Huduma za kifedha vile vile kwa vijana ambao wanapokea malipo yao kupitia miamala ya simu.
Serikali inapaswa kuondoa kodi na sheria kandamizi kwenye mifumo ya kiteknolojia kwa sababu kwa sasa teknolojia ndio kimbilio la vijana ambao hawana ajira rasmi.

3.Kuboresha miundombinu; Kuboresha miundombinu kama barabara kutachangia ongezeko la vijana ambao wataweza kujiajiri na kuajiriwa mfano Bodaboda,Uber na mengine.Miundombinu imekua ni kikwazo pia ktk kutatua tatizo la ajira vijana wengi wamekua wakikatisha uhai na wengine kupata ulemavu wa kudumu kutokana na changamoto zinazotokana na ubovu wa miundombinu kama barabara.Pia miundo mbinu ya mtandao(Network) kwa hapa Tanzania sio mizuri kwa baadhi ya maeneo mfano mimi naishi mkoa wa Pwani huku mtandao wa simu ni tatizo na ni mjini kabisa.

4.KUTOA MIKOPO KWA RIBA NAFUU ; Nashauri serikali na taasisi mbalimbali za mikopo kuweka masharti nafuu kwa vijana ambao wapo tayari kufanya ujasiriamali na kuwapa elimu juu ya ujasiriamali ili kuwepo matokeo chanya katika mkopo huo.

5.KUBADILI MIFUMO YA ELIMU; Kwa upande wangu ninaona serikali inapaswa kubadili mifumo ya kielimu na kuongeza masomo ya kiubunifu zaidi.Kwa mawazo yangu mimi mwanafunzi anapomaliza kidato cha sita asiwe anapelekwa JKT bali apelekwe VETA kwa muda atakao kaa VETA atapata maarifa makubwa ya kiubunifu ambayo atakwenda kuyatumia hata akifika Chuoni na baada ya kumaliza chuo tofauti na maarifa atakayopata jeshini.Kuongeza masomo ya Stadi za Kazi,biashara na Kilimo kwa shule za sekondari hii itapelekea kuongeza ubunifu kwa kijana hata atakapomaliza elimu yake basi atapata nafasi ya kujiajiri kwani masomo hayo yamekua yakifundishwa lakini hayana mwendelezo.

HITIMISHO
Serikali inapaswa kupata watu wabunifu zaidi kwenye ngazi za juu ili kuleta chachu ya maendeleo kiubunifu na si kuweka sheria kandaminizi.Pia Vijana wanapaswa kuwa wabunifu na si kusubiri tu serikali.

Asante.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom