SoC02 Mapambano ya kutokomeza Malaria

SoC02 Mapambano ya kutokomeza Malaria

Stories of Change - 2022 Competition

Manventure

Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
10
Reaction score
4
MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA.

Malaria ni ugonjwa unaoambukizwa na mbu jike aitwaye anopheles. Mgonjwa anaambukizwa na mbu jike mwenye vimelea vya plasmodium. Mbu huwa na mazalia maeneo yenye majani marefu au mengi, maji yaliyotuama kama madimbwi, visima, na maji ya mvua yaliyotuama.

Takwimu zinaonesha ugonjwa wa malaria umeenea takribani nchi 91 duniani hadi 2016. Kwa mujibu wa WHO, mwaka 2017 kuliripotiwa visa takribani milioni 219 katika nchi 87 za ugonjwa wa malaria. Sehemu kubwa ya maambukizi ya malaria hutokea bara la Afrika hasa kusini mwa jangwa la sahara.

Kama jamii tukichukua hatua fulani kwa sehemu kubwa tutafanikiwa kupunguza visa vya malaria.

Dalili za malaria.

Baada ya kupata vimelea vya ugonjwa dalili huonekana siku kumi (10) hadi wiki nne baada ya kuambukizwa. Mtu anapopata malaria huonesha dalili zifuatazo;
Kutetemeka kwa baridi,
kutoka jasho jingi,
kichwa kuuma,
kichefuchefu,
kutapika au kuhara,
maumivu ya tumbo,
kuharisha, kuwa na damu katika kinyesi, maumivu ya misuli ya mwili.

Kama mtu amepata moja ya dalili hapo juu, japo wengine inaweza kutokea dalili moja au zaidi ya moja anakuwa amepata ugonjwa wa malaria.

ATHARI ZA MALARIA
Malaria ni moja ya miongoni ya magonjwa yenye tishio kubwa sana duniani japo haionekani kwa haraka lakini imesababisha vifo vingi sana, mfano mwaka 2016 pekee vifo zaidi ya laki nne. Pia, watu 435,000 walifariki kutokana na malaria mwaka 2017.

Athari zitokanazo na malaria ni pamoja na;
Kuvimba mishipa ya damu kwenye ubongo ( au malaria ya ubongo),
kujaa maji kwenye mapafu ( au pulmonary edema),
upungufu wa damu ( anemia) kutokana na kuharibika kwa seli za damu, upungufu wa sukari mwilini na hali ikiwa mbaya zaidi hupelekea kifo.

NJIA ZA KUPAMBANA NA KUTOKOMEZA MALARIA
Malaria ni ugonjwa ambao umekuwepo muda mrefu sana. Zipo njia nyingi ambazo miaka ya nyuma wamezitumia, hata sasa tunatumia kukabiliana nayo. Leo tuangazie njia kuu mbili za kupambana na malaria, ambazo ni kutumia chandarua chenye dawa na kuua mazalia ya mbu.

Njia ya kwanza: Kutumia chandarua chenye dawa.

Chandarua husaidia sana kuzuia mbu wasitufikie hasa wakati wa kulala. Elimu ya sasa sehemu kubwa inahimiza kutumia chandarua tena chenye dawa. Naungana na hoja ila matumizi ya chandarua pekee haiwezi kukomesha mbu kuwepo au kuzuia malaria kabisa bali inazuia mbu wasikufikie tu.

Ni sawa na mfano huu. Nyumba yako imevamiwa na maadui, wengine ndani na wengine nje halafu unaangamiza waliopo ndani pekee na kuacha walioko nje. Kuna wakati watarudi na kuingia tena kukushambulia.

Vivyo hivyo, kutumia chandarua pekee haitoshi. Kaya nyingi za sasa hutumia chandarua pekee na kusema wamefanikiwa kupambana na malaria. Njia sahihi ni kusafisha maeneo yanayozunguka makazi kwa ujumla na kuua mazalia ya mbu kabisa.

Ndipo matumizi ya chandarua yawepo ili kujikinga na mbu wataokuwa wamebakia.
Maoni yangu nasema matumizi ya chandarua ni sahihi lakini matumizi ya chandarua bila kutokomeza mazingira ya mbu sio sahihi.

Njia ya pili: Kuua na kutokomeza mazalia ya mbu.

Watu wazima na wazee wengi husema hapo awali walitumia njia ya kutokomeza mazalia ya mbu zaidi. Lakini sasa ipo wapi mbinu hii?

Kwa kuwa malaria haipatikani kutoka mtu mmoja kwenda mwingine, ni vema kutokomeza kabisa mazalia hayo ili kutokomeza malaria kabisa.


Kwa nini mazalia ya mbu na sio chandarua?

Sehemu ambazo mbu hawa huzaliana huwa na mayai ya mbu hasa kwenye maji yalotuama, hivyo kila siku kunakuwa na uwepo wa mbu. Maeneo hayo yakitokomezwa inazuia uzalishaji zaidi wa mbu. Lakini chandarua ni unazuia tu mbu wasikufikie bali wao wanazidi kuzaliana.

Nchi zilizofanikiwa kutokomeza malaria.
Ukitazama nchi zilizofanikiwa kupambana na malaria walijikita katika kuangamiza mazalia ya mbu na sio matumizi ya chandarua. Mfano mzuri ni China ambayo WHO imeitunuku cheti kufanikiwa kutokomeza malaria kabisa.

Sio China pekee ilofanikiwa kupambana vita dhidi ya malaria, nchi nyingine 11 ni pamoja na; United Arab Emirates (UAE), Morocco, Turkmenistan, Armenia, Argentina, Kygyzstan, Paraguay, Sri Lanka, Algeria, and Salvador.

Ni hakika nchi zote hizi ziliweka nguvu katika matumizi ya dawa za kuulia vimelea vya malaria na kuangamiza mazalia ya mbu kabisa.

Kutumia dawa za kupulizia ipo sambamba na kuua mazalia ya mbu.

Dawa hizi maalumu kuangamiza vimelea hivi hupulizwa chini ya uangalizi wa wataalamu na sehemu kama vile kuzunguka nyumba, mabwawa, visima na maeneo mengine.


Dawa za kuulia vimelea zinaweza kupuliziwa kwenye mashamba, maeneo yenye maji yaliyotuama, kwenye mifumo ya maji ili kuua mayai ya wadudu wote ikiwa ni pamoja na vimelea vya plasmodium na mayai ya mbu.

Maboresho gani yafanyike.?

Elimu kuifikia jamii kwa njia mbalimbali na tofauti tofauti kama vipindi vya televisheni, magazeti, redio, mitandao ya kijamii na njia nyingine sahihi ambazo jamii itapata ujumbe sahihi na wakati sahihi.

Pia, kuna msemo usemao “cha kale ni dhahabu”. Hata kama kuna maendeleo ya kijamii, sayansi na teknolojia hatupaswi kusahau au kutotilia maanani njia za kale zilizotumika kupambana dhidi ya ugonjwa wa malaria.

MAREJEO.
Chandarua kipya kinachoimarisha kinga dhidi ya Malaria - BBC News Swahili (picha #1)
RC Mongella azindua zoezi la upuliziaji dawa ya ukoko wilayani Ukerewe (picha #2 na picha #3)

_100817638_77357696-6c9e-48b7-9a24-916f7049c8f2.jpg
3.JPG
MBU.jpg
 
Upvote 0
Hili andiko sikutag @shindanolauandishi.
Sijui watalionaje?
Kwa anaefahamu namna JF @JF wanàweza kuliona msaada please
 
Back
Top Bottom