MAPAMBANO YA RUSHWA NA TANZANIA TUITAKAYO MIAKA 5 MPAKA 25
Rushwa inaweza kutafsiriwa kuwa ni hali ya kupokea na kuchukua mali au pesa ya serikali au kampuni kwa faida binafsi. Rushwa inaweza kuwa katika namna mbili tofauti; rushwa kubwa na rushwa ndogo. Tanzania inakabiliwa na tatizo la rushwa za aina zote mbili kwa kiwango kikubwa.
Rushwa kubwa iliyozoeleka kwa jina la ufisadi umekuwa kama donda ndugu lisilo na dalili ya kupona likihusisha utoaji na upokeaji wa pesa kutoka na kwenda kwa watu wenye nyadhifa kubwa serikalini, kampuni au taasisi na rushwa ndogo, ambazo zimekuwa zikitolewa na kupokelewa na watu wa hali ya kati na masikini mara nyingi ni katika kuhakikisha matatizo yao yanatatuliwa kwa haraka na wepesi.
Katika kupambana na rushwa za aina zote mbili, serikali ya Tanzania mwaka 1975 ilianzisha Kikosi cha Kuzuia Rushwa kisha ikabadilishwa kuwa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (TAKURU) mwaka 2002.
Katika kuboresha taasisi hiyo mwaka 2007 ikabadilishwa tena na kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Lengo la kubadilisha taasisi hiyo ilikuwa ni kuzuia uwezekano wa rushwa kutokea kama njia ya kumaliza kabisa nchini Tanzania.
Ili kufikia lengo hilo taasisi ilianzisha dawati lenye mkurugenzi wake linalohusu uzuiaji rushwa likiwa na majukumu ya kufanya tafiti, kuchambua mifumo, kufuatilia matumizi ya rasilimali za umma, na kwakutanisha wadau ili kuweza kuzuia rushwa.
Pamoja na juhudi hizi zilizofanywa na TAKUKURU bado Tanzania ni moja kati ya nchi zenye kiwango kikubwa cha utoaji na upokeaji wa rushwa.
Kwa mujibu wa chombo kinachotumika kukadiria kiwango cha rushwa katika sekta ya umma kwa nchi mbalimbali duniani (Corruption Perceptions Index) inaonyesha Tanzania ni nchi ya 87 kati ya nchi 180 duniani. Kwa kiwango hicho, Tanzania inahitajika kufanya jitihada za makusudi ili kuweza kujinasua kutoka kwenye tatizo hili.
Kuna namna mbali mbali zinazoweza kuisaidia kupunguza kiwango cha utoaji na upokeaji wa rushwa nchini Tanzania kama ifuatavyo;
Elimu kuhusu madhara ya utoaji na upokeaji wa rushwa, moja ya sababu za watu kupokea na kutoa rushwa ni ukosefu wa maadili. Maadili hufundishwa kwa watu kupitia shule na hutegemea zaidi umri wa mfundishwaji ili aweze kuyaelewa na kuyaishi. Kwa bahati mbaya nchi yetu haina utaratibu wa kufundisha watoto kuikataa rushwa tangu shule ya msingi, sekondari mpaka vyuo hivyo suala la rushwa halichukuliwi kama ni uhalifu kwa watu wengi katika jamii zetu. Kitendo cha kufundisha kitawezesha wanafunzi kuichukia rushwa tangu mapema hivyo itasaidia matumizi ya nguvu ndogo kuikataa rushwa watakapokuwa watu wazima.
Uwazi katika ofisi za umma kuhusu mambo ya uwekezaji na maendeleo, kumekuwepo siri nyingi kwenye ofisi ya umma kwa vitu vilivyofaa kuwekwa wazi ili wananchi waweze kujua nini kinaendelea. Uwazi huo utasaidia wananchi kufahamu mchakato mzima kuhusu mambo ya uwekezaji na maendeleo. Kwa nchi kumi zilizoelezwa kuweza kupambana na rushwa ambazo ni Denmark, Finland, New Zealand, Norway, Singapore, Sweden, Switzerland, Netherlands, Germany and Luxemburg huweka wazi taarifa zote zinazohusu umma kupitia wanahabari ili kuwaarifu wananchi. Uwepo wa uwazi huo unaonesha ni sababu moja wapo kwa nchi hizo kuweza kuzuia rushwa kwa kiwango kikubwa.
Mfumo huru wa kimahakama, utoaji na upokeaji wa rushwa ukishakuwa kitu sugu basi ni vyema kukawa na mfumo huru utakaowezesha kutiwa hatiani kwa wahusika wa pande mbili. Kumekuwepo tuhuma kadha wa kadha ambazo zinaviashiria kutokuwepo kwa uhuru kama vile baadhi ya ripoti kubakia siri hata baada ya maamuzi ya mahakama kutolewa. Hali hii inamchochea mpokeaji na mtoaji wa rushwa kuendelea na tabia hiyo kwa vile kuna uwezekano wa kupindishwa na kupendelewa akifika mahakamani. Utekelezaji wa kisheria umekuwa na kigugumizi kikubwa sana katika kuchukua hatua kali kwa watoaji na wachukuaji wa rushwa. Kukosekana kwa uhuru katika mahakama kunaweza kupelekea kesi ya rushwa ikafanyiwa maamuzi chanya kwa ya kumpendelea aliyetiwa hatiani kwa kutoa rushwa pia hivyo jambo hili likakosa kupatikana mwisho wake.
Uwepo wa asasi huru za kiraia, asasi za kiraia zimesaidia sana katika uelimishaji kuhusu mambo tofauti. Ni vigumu kwa serikali yenyewe kujichunguza na kujirekebisha kwa vile rushwa ipo katika taasisi za serikali. Hivyo basi kwa kutumia asasi za kiraia zitasaidia kuongezeka kwa uelewa madhara ya rushwa.
Adhabu kali kwa watuhumiwa wa rushwa, wakati mwingine hutokea binadamu kutokuwa wepesi kuelewa, kadri wanavyoeleweshwa ndiyo wanazidi kutokuelewa. Katika mazingira hayo njia pekee inayofaa ni adhabu kali kama vile kifungo cha maisha jela pamoja na kazi ngumu au kunyongwa. Njia hii imezisaidia sana nchi za mashariki ya kati kama vile Irani, Falme za kiarabu na Lebanoni, nchi za mashariki ya mbali kama vile Uchina na Korea ya kusini.
Mambo hayo yaliyopendekezwa hayawezi kutokea ndani ya kipindi kifupi uvumilivu na uthabiti unahitajika kwa kiwango kikubwa.

Upvote
2