Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,175
- 2,294
Ujasiri wa Maalim Seif wa kwenda hadharani na kuwapa taarifa nzito wanachama na wapenzi wa CUF, juu ya kumtambua Rais Karume ilibidi upongezwe na Taasisi zote kuu na watanzania wote kwa jumla. Katika mazingira yeyote yaliyopo, bila ya kujua hatima ya safari hiyo ndefu, lakini hiyo ilikuwa ni hatua moja kuelekea katika kupunguza mvutano wa kisiasa kati ya CUF na CCM Zanzibar.
Kwa mshangao mkubwa ni zaidi ya mwezi sasa hivi toka tukio hilo litokee, lakini si Pengo, Kilaini, Askofu Shayo au viongozi wa KKKT waliodiriki kutoa pongezi zao kwa tukio hilo. Baraka za viongozi hawa ni muhimu sana, hasa ukizingatia kuwa huko nyuma katika matukio tofauti walijitokeza ni kutoa maoni yao. Kwa mfano wakati wa machafuko ya Mwembechai, Pengo alisikika katika Radio Tumaini akiipongeza Serikali kwa hatua iliyochukua katika kudumisha amani. Nilitarajia katika tukio hili kubwa la kihistoria la kumtambua Rais Karume vile vile kuwa Pengo angetoa pongezi.
Lakini hasa nini maana ya ukimya huo? Hili ni swali ambalo nafikiri kila mtanzania anajiuliza. Sihitaji kuja na mawazo yangu kwa hili, lakini ingekuwa vyema kama viongozi hawa wenyewe wangetjitokeza hadharani na kueleza sababu za ukimya wao. Aidha ningewaomba wanJF wenye upeo mkubwa wakuwaelewa viongozi hawa pamoja na wale waliobahatika kujiwa na Roho Mtakatifu watueleze sababu ya ukimya wao.
Amani ya Zanzibar ni Amani ya Tanzania nzima, hivyo si siri kuwa mapatano ya CUF na CCM Zanzibar ni ushindi kwa watanzania wote. Na hatua iliyochukuliwa na Rais Karume na Maalim Seif ni kwa faida na maslahi ya Tanzania nzima. Tuwaombee waendelee vizuri.