Mh. Rais Samia Suluhu ni kama Rais wa Serikali ya Awamu ya 6. Huyu mama hakuwepo kabisa awamu ya 5. Ni Rais mpya ambaye hakuwahi kuwepo katika Serikali iliyopita.
Kama alikuwepo haya anayoyashangaa leo na kuyakosoa akinanga Serikali ile yalifanyika yeye akiwa kwenye Coma? Hakujua kabisa.
Ningeweza anza msifia kwa haya lakini nashindwa sababu nami ntakuwa mnafiki. CCM mnataka sema Serikali yote na nchi nzima ilikuwa inaongozwa na Marehemu Dr. Magufuli peke yake? Kama ni hivyo hapa nitamsifu sana. Aliweza ongoza zaidi ya watu Mil 50 na ninyi mkiwa pembeni yake akiwa peke yake. Hapo tumsifu.
Yanayofanyika leo na hawa watendaji wa sasa ni kama hawakuwahi kuwepo kabisa kwenye uongozi uliopita. Je nani aliona si sawa akapinga au akajiuzulu?
Watanzania sisi tuna PHDs za Unafiki, sisi ni wachawi.leo hii tunaomsifia huyu mama asipokuja kutubariki kimaslahi tutabadilika tena.
Wakati Magufuli anaingia Madarakani na Bungeni CDM wanatoka Zitto alifanyaje?ni mpaka naye alipokuja guswa maslahi yake akabadili gear.
Huyu mama alipoona maovu yanafanyika aliwahi sema nini?aliwahi fanya nini? Je tunawezaje sema hakushiriki?si alisema watu wapige kura wasipige CCM itashinda?
Mimi sikatai anaweza kuwa na mawazo mema. Lakini napata wasiwasi huu wema wa sasa ni upi? Nitawaamini wale waliopinga uovu toka mwanzo kuliko walioshiriki kula nyama za binadamu halafu baadaye wakaja sema hata hivyo si tamu sana,turudi kula za wanyama.
Wapinzani wa Magufuli imekuwa rahisi kuanza kucheza ngoma hii kwa midundo yake wakiruka huku na kule. Lakini wanasahau CCM ni ile ile na asilimia 80 ya Mawaziri waliokuwepo na Viongozi ni wale wale.
Kanzu mpya lakini sheikh ni yule yule wa zamani. Tuweni makini sana na kujiongopea kwetu.
Mwisho namtakia Kheri Rais Samia. Mimi nasubiri sana kuja kusema neno. Nasubiri sababu subra hufunua Nuru.