Nawasalimu wote,
Nianze kwa kumpongeza mheshimiwa Rais SSH kwa hatua anazochukua kuleta maboresho katika mfumo wa "Haki-Jinai", katika hili nimeona ana nia ya dhati kuleta mabadiliko chanya.
Nikiwa mhanga wa mfumo uliopo wa haki jinai nimeshuhudia mabadiliko kadhaa yaliyoanza kufanyika ikiwemo kubadilisha baadhi ya vifungu vya sheria ambapo baadhi ya makosa/tuhuma mtuhumiwa anakamatwa tu pale upelelezi umekamilika ili usikilizaji wa kesi uanze mara moja ili haki itendeke (kwa mujibu wa sheria).
Sanjali hilo kasi ya usikilizaji kesi imeongezeka hivyo kupelekea kupungua mahabusu magerezani ikilinganishwa na enzi za " mwenda zake".
Hivi karibuni amenzindua tume itakayopitia mfumo wa haki-jinai ili kuleta maboresho katika mfumo mzima; hoja ni kwamba nikiwa mhanga wa mfumo wa haki jinai uliopo na ukizingatia tume hiyo imesheheni vigogo wastaafu ambao sidhani kama wanajua madhila ya wahanga wa mfumo wetu wa haki-jinai, ninaomba yeyote kati yetu anajua namna gani ninaweza kupeleka maoni yangu kwenye tume (ikiwezekana ana kwa ana) ninaamini ninazo input ikizingatia nilisweka gerezani (kama mahabusu) kwa miaka mitatu kwa makosa ya "kutengenezwa".
Naomba kuwasilisha.