Mapendekezo kwa Tume ya Haki Jinai

Mapendekezo kwa Tume ya Haki Jinai

Ramark

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2015
Posts
1,989
Reaction score
1,447
Habari wakuu,

Naomba tutumie Uzi huu kuleta hoja zetu za kuboresha mfumo wa haki jinai ili kwayo tuzichambue na kila mmoja kwa nafasi yake akipenda kuwasilisha wazo lako lilipendekezwa humu au kuboreshwa kwa njia ambazo zimetolewa na Tume.

Kwa sasa wanaenda Mikoani ambako watakuwa na mikutano ambayo itakuwa kama Uzi huu pia kwa manufaa nao wanaweza shiriki na kuchota mawazo yetu au mwisho tukawaomba Uongozi wa JF kuwakilisha mapendekezo yetu.

Naamini kwa vyovyote vile mawazo yanayotolewa kule na mtu si Siri lakini hatujapa fursa ya kufahamu kutoka kwa wenzetu walioshiriki Tayari kwa namna tulivyofanya kwenye Tume ya Katiba ya mzee Warioba.

Karibuni
 
Maoni yangu ni kuwa zitungwe Sheria za kurahisisha kumshitaki askari polisi anayemuonea raia,au anayeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa kupofushwa na rushwa.Sheria hiyo pia irahisishe kulishitaki jeshi iwapo mtuhumiwa atafia mikononi mwao maana baadhi Yao vitendo vyao visivyozingatia haki za watuhumiwa vinasababisha watuhumiwa kufia vituo vya polisi.
 
#2 hapo juu, kiini cha yote haya ni kuwa na Katiba mpya, tukipata hii katiba itatupa vyombo vingi ambavyo vitakua huru na vinajitegemea means havitafanya majukumu yake kwa miongozo ya politicians, mfano judiciary huru, na ulichokiongelea hapo juu ni chombo kinachoitwa IPID, hawa ni kama MPs ndani ya majeshi, ukiona umeonewa na polisi unakwenda kwenye desk lao na kufungua docket (kila police station itakuwa na desk ya IPID)hawa kisheria watakuwa na uwezo wa to investigate, arrest and kumpeleka mahakamani police mtuhumiwa, pia tunahitaji kuwa na PP ili kuhakikisha kila mmoja wetu yupo chini ya sheria(elewa PP,atakuwa na uwezo wa kama judge, uamuzi wake ni binding kisheria)
 
Napendekeza kufutwa kwa sheria inayounda TAKUKURU

Maana naona hawana kazi wala shughuli waliyofanikiwa Tangu ianzishwe

Napendekeza sheria inayounda DPP iboreshwe kwa kuunda ofisi ya waendesha mashtaka
Tusiwe na ofisi inayotambulika kwa cheo na pia ianzishe ofisi za waendesha mashtaka wa wilaya
Pia waendesha mashtaka wapewe majukumu ya Direct or indirect investigation ya matukio yote ambapo kwa namna yoyote wanaweza kufungua shauri kwa ushahidi walionao.
 
Pia kwenye sheria ya waendesha mashtaka tuwe special- appointed organization of prosecutors ambao wamethibitishwa na bunge ambao watashughulika na masuala yote uhujumu uchumi, rushwa kubwa, matumizi mabaya ya ofisi, utakatishaji fedha, scandal chafu za viongozi wa serikali

Suala LA Rushwa ni jukumu LA Prosecutors wote kuanzia ngazi ya wilaya kwa Direct or indirect investigation power vested on them by law

Wakishachunguza suala lolote wanapeleka mahakamani direct bila ksubiri ruhusa na DPP Bali Mkuu Mahalia

Kwa nini waendesha mashtaka

Police wanaofanya uchunguzi hawajasoma hata degree ya sheria Bali basics na experience za mafunzo hivyo weledi unakosa pia wao wataendelea kuchunguza na kisha kupeleka kwa prosecutor wa wilaya ambaye ndiye afisa wa mahakama na hivyo tufute judicial police or Police prosecutor

Pia prosecutors wapewe madaraka ya kukamata kwa msaada wa police isiwe kama Takukuru na wawe na right of detention of a criminal.
 
Maoni yangu ni kuwa zitungwe Sheria za kurahisisha kumshitaki askari polisi anayemuonea raia,au anayeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa kupofushwa na rushwa.Sheria hiyo pia irahisishe kulishitaki jeshi iwapo mtuhumiwa atafia mikononi mwao maana baadhi Yao vitendo vyao visivyozingatia haki za watuhumiwa vinasababisha watuhumiwa kufia vituo vya polisi.

Dawa ni katiba mpya, hatuwezi kujenga Ghorofa kwenye tope
 
Back
Top Bottom