Mapendekezo: Serikali irekebishe au itunge sheria mpya kabisa ya ugaidi au Terrorism Act na itoe miongozo kwa raia kuchukua tahadhari

Mapendekezo: Serikali irekebishe au itunge sheria mpya kabisa ya ugaidi au Terrorism Act na itoe miongozo kwa raia kuchukua tahadhari

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Kesi za ugaidi au kumtuhumu mtu kwa kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi ikiwemo kuua viongozi ni jambo kubwa sana.

Hata ile kuwatuhumu watu fulani katika jamii kuwa wanapanga kutekeleza vitendo vya kigaidi na pia kuua raia wengine pia ni jambo kubwa.

Katika matukio makubwa ya kuleta hofu na taharuki, ugaidi waongoza ukifuatiwa na uhaini.

Kesi za uhaini na ugaidi hazitofautiani sana katika kuzishughulikia kwani watuhumiwa hukaa rumande hadi kesi zao zitapotajwa mahakamani.

Kwa wale wenzangu tuliokuwa shule miaka ya themanini tulifuatilia kwa makini kesi ya uhaini ambapo kundi fulani ndani ya jeshi na baadhi ya raia walituhumiwa kutaka kuipindua serikali ya Tanzania na kumuua raisi wa wakti huo hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Ilikuwa ni kesi yenye mvuto kwani mimi kwa upande wangu nilipenda jinsi uendeshaji wa kesi hiyo, majaji, mawakili, mashahidi na timu ya waandishi wa habari walivyokuwa wakijitahidi kutoa taarifa za kesi hiyo kupitia magazetiu maarufu ya Uhuru, Mfanyakazi, Daily News na yale ya Jumapili, Sunday News na Mzalendo.

Sasa tukirudi katika kesi hii ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake kadhaa, nimegundua kuwa kesi hii haipewi umuhimu mkubwa khasa kwa upande wa serikali kwamba ni hatua zipi imechukua ili kuweza kukabiliana na janga la ugaidi endapo lilatokea au lipo katika hatua za kupanga ni mazuio mangapi labda yamefanywa na jeshi la polisi.

Raisi Samia Suluhu Hassan akiomngea na BBC jana amesema kesi ipo mahakamani lakini hatatoa wito wowote kwa watanzania kuchukua hatua za tahadhari endapo kuna kundi jingine ambalo lipo mbioni kupanga matukio ya kigaidi na hatarishi.

Waziri wa mambo ya ndani pia hajatoa tamko lolote la wizara kuwahakikishia wananchi kuwa nchi ipo salama na kwamba labda polisi haiwatafuti watu wengine kuhusiana na matukio zaidi ya ugaidi.

Isitoshe, hata jeshi la polisi nalo lipo kimya kwa upande wa utoaji taarifa kwa vyombo vya habari kwamba kwa sasa haliwatafuti watu wowote wale ambao kwa namna moja au ingine wanahusika na wale watuhumiwa walioko mahabusu.

Je, ni wakati sasa kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na polisi wakawa wazi wa wananchi na kuwa na utaratibu wa kutoa taarifa zozote zile zinazohusiana na vitendo vya kigaidi, uletaji taharuki, vitendo vya ujambazi na uporaji wa kutumia silaha?

Ugaidi unahusiana na masuala mengine kama utakatishaji fedha haramu, ujambazi wa kutumia silaha na uporaji mwingine, utekaji watu kwa ajili ya kuchomoa viungo vya mwili,Utekaji wasichana wadogo kwa ajili ya biashara ya ngono, uuzaji miili kwa wadada poa na biashara ya madawa ya kulevya.

Ili magaidi waweze kutekeleza shughuli zao ni lazima watumie njia hizio hapo juu ili kuweza kupata fedha.

Katika nchi kama Irak, Afghanistan, Syria, Nigeria na Libya magaidi wana vitega uchumi kabisa ambavo wamejiwekea ili kupata fedha za kuendesha shughuli zao.

Nimeangalia aina ya mashtaka yanomkabili Mbowe na wenzie na nimeona imetumika sheria ya mwenendo wa makosa ya Jinai ilorejewa mwaka 2019.

Katika sehemu ya aina ya makosa au "Particulars of Offence" ni yamo masuala kama kosa limetendeka wapi, mali na amani kuwepo matatani na kadhalika.

Naelewa kesi ipo mahakamani na yaendelea lakini pia hata mashirika na nchi rafiki za kigeni kama Marekani wao wanahoji ushahidi juu ya tuhuma za ugaidi zinazomkabili Mbowe.

Kwa mtu kama mimi ambae nimepata kuishi katika nchi za magharibi, wao wanazo sheria za ugaidi Terrorim Act ambazo zinawaongoza vyombo ya usalama na polisi na mahakama katika kuwabaini na kuwakama watuhumiwa wa ugaidi.

Kwa mfano vyombo vya kijasusi vikibaini (baada ya taarifa za kijasusi au intelligencen tips) kuwa kuna kundi fulani linajiandaa kupanga kufanya vitendo vya kigaidi, basi hufanya operesheni maalum na kuhakikisha wahusika wote wanakamatwa na huwa hawakosei.

Hivyo watuhumiwa hukamatwa kwa mahojiano au "questioning" na mahakama huwa standby kutoa muda endepo polisi watahitaji muda zaidi.

Polisi wataendelea kumuhoji/kuwahoji watuhumiwa na ikizidi masaa kumi na mbili basi hutakiwa kuomba kibali mahakamni ili kuendelea kuhoji.

Mara nyingi wakifanya hivi huku pia wanakuwa wanamalizia upande wa upelelezi kwamba ushahidi wote wakusanywa na kupelekwa kwa ofisi ya mwendesha mashtaka ambae akirishia basi mahojiano hukamilishwa kwa polisi kuamua kumfikisha mahakamni mtumhumiwa na kusomewa mashtaka ya ugaidi.

Lakini pia sheria hiyohiyo ya ugaidi huwapa polisi na vyombo vya usalama uwezo wa kumshikilia mtumhumiwa wa ugaidi kwa muda usojulikana ingawa watuhumiwa huwekwa mahabusu kwa muda huo hadi uchunguzi utakapokamilika.

Wengi tumesikia mara nyingi kambi ya "Guantanamo Bay" ambayo imehifadhi watuhumiwa kadhaa wa ugaidi kwa muda mrefu hadi miaka 10 na zaidi!

Hivyo, sheria ya ugaidi terrorism Act ni lazima kwa nchi kama Tanzania kuwa nayo na ndyo inakuwa msingi wa kesi nyingi za ugaidi na haifungamani kwa vyovyote na sheria za utakatishaji fedha wala uhujumu uchumi.

Sheria ya Ugaidi Terrorism Act itaambatana na miongozo ya namna ipi nchi ichukue tahadhari au ni nyakati zipi tahadhari zinatolewa endapo kunakuwa na matishio ya ugaidi au uletaji taharuki.

Hizi huitwa "Threat levels" au viwango vya matishio na vyombo vya usalama huweza kupanga viwango kuanzia 1-5, Kiwango 1 kikiwa ni hali iliyo hatarishi zaidi na tukio laweza kutokea wakati wowote na kiwango cha 5 kikiwa ni hali hatarishi lakini uwezekano wa kutokea tukio ukiwa ni mdogo sana.

Kwa mfano, kitendo cha kukamatwa bwana Mbowe na wenzake kadhaa, kungeambata na moja ya viwango vya matishio au "Threat levels" kwa kuzingatia moja ya tuhuma za ugaidi wanazokabiliwa Mbowe na wenzie ni la kuua vingozi wa kitaifa.

Lakini nchi ikindeleea na maisha yake na polisi na vyombo vya ulinzi na usalama wakiendelea na shughuli zao kimyakimya bado kwa watu wengine wanaopenda kuona kuna kuwajibika fulani kwamba sheria ya ugaidi ipo na nchi yetu imepiga hatua katika utekelezaji wa shughuli zake za kiusalama.

Katika kuendelea huko na maisha Soko Kuu La Kariakoo liliungua mwezi ulopita na baadae kukawepo kwa tukio la kuungua kwa kituo cha kupoozea Umeme cha Soga, na kisha kupasuka kwa bomba kubwa la maji karibu na Msamvu.

Hii ni miundombinu ambayo inakuwa chini ya vyombo vya ulinzi na usalama, na inahitaji kulindwa kwa gharama yoyote ile.

Jeshi letu wa wananchi au polisi wanaweza kujengewa vituo maalum vya ulinzi katika maeneo hayo kuhakikisha vitendo vya hujuma, ugaidi na uharibifu wa makusudi ninakomeswa.

Hivyo napendekeza kuangaliwa upya kwa sheria ya ugaidi na kuboreshwa na pia kuwepo na miongozo ya namna ya kukabiliana na vitendo vya kigaidi.

Sheria hii itakuwa ni mwongozo kwa vyombo vya usalama, polisi na mahakama ambavyo kwa pamoja vitafuata na kutumia sheria hii kama biblia au msahafu.

Tukifanya hivyo nchi yetu itakuwa imepiga hatua mbele na kuondoa masuali meengi ambayo huulizwa mara pale wale wanaharakati na wanasiasa wanapokumbwa na dhoruba za tuhuma za ugaidi lakini ikawa taabu kutafsiri ugaidi na namna ya kupinga kasi hiyo.
 
Kipaumbele ni KATIBA MPYA bila ya katiba mpya huu udhalimu na dhuluma za maccm waakishirikiana na polisiccm utaendelea milele. Ikishapatikana Katiba mengine haya mengine yatakuja tu ili kulinda HAKI na USAWA wa Watanzania wote ili kuachana na huu uhuni uliokithiri nchini wa kubambikia kesi FEKI kwa Watanzania na Viongozi na wanachama wa vyama vya siasa na hasa Chadema kwa zaidi ya 95%.
 
Magaidi gani walioko Tanzania? kama ni wale wa Kibiti tulishaambiwa na Sirro walikimbilia Msumbiji, kwanini asingetuambia wapo waliobaki wako Dsm au kwingineko?

Hii issue ya ugaidi polisi waliileta wakati ule wa uchaguzi ili kuisaidia CCM kusginda uchaguzi, sioni maana ya kumtuhumu mtu gaidi halafu mkawa mnapiga nae story muda wote wakati toka mwaka jana Mambosasa alishasema wana ushahidi dhidi yake.

Mnasubiri mpaka Katiba Mpya ianze kudaiwa ndio mnaleta story za ugaidi ili mcheze na akili za wasiojielewa wawaogope wapinzani wakidhani ni watu wa vurugu, huu mchezo CCM na polisi wameuanza zamani sana enzi ya CUF ya Maalim na Lipumba.
 
Ugaidi ni nini?

Kuna aina ngapi za ugaidi?

Ni viashiria vipi vinaonyesha chembe chembe za ugaidi au mtu kuanza kuhesabiwa kama gaidi?

Hukumu dhidi ya ikoje au inatolewaje?

Tuanzie hapo.
 
Magaidi gani walioko Tanzania? kama ni wale wa Kibiti tulishaambiwa na Sirro walikimbilia Msumbiji, kwanini asingetuambia wapo waliobaki wako Dsm au kwingineko?

Hii issue ya ugaidi polisi waliileta wakati ule wa uchaguzi ili kuisaidia CCM kusginda uchaguzi, sioni maana ya kumtuhumu mtu gaidi halafu mkawa mnapiga nae story muda wote wakati toka mwaka jana Mambosasa alishasema wana ushahidi dhidi yake.

Mnasubiri mpaka Katiba Mpya ianze kudaiwa ndio mnaleta story za ugaidi ili mcheze na akili za wasiojielewa wawaogope wapinzani wakidhani ni watu wa vurugu, huu mchezo CCM na polisi wameuanza zamani sana enzi ya CUF ya Maalim na Lipumba.
Ugaidi upo ila umejificha.

Kijana Hamza anatupa angalizo kuwa ugaidi waweza kutokea Tanzania na watu wenye silaha wapo.
 
Ugaidi ni nini?

Kuna aina ngapi za ugaidi?

Ni viashiria vipi vinaonyesha chembe chembe za ugaidi au mtu kuanza kuhesabiwa kama gaidi?

Hukumu dhidi ya ikoje au inatolewaje?

Tuanzie hapo.
Ugaidi ni kitendo cha kutumia nguvu na silaha kutisha watu kwa malengo fulani ya kisiasa.

Pili, hakuna aina za ugaidi bali yapo malengo ya aina tofauti ya ugaidi yanayotokana na maoni tofauti, misimamo mikali na makusudio maalum.

Tatu, hakuna anaeweza kuona viashiria vya ugaidi isipokuwa polisi maalum wa kupambana na ugaidi.

Nchi nyingi hukumu ya ugaidi kutofautiana zingine huwa kuanzia miaka 5 kwenda juu hadi maisha.

Hukumu hiyo huzingatia mambo kama mhusika mkuu, wahusika wasaidizi, matayarisho, na utekelezaji wa kitendo cha ugaidi.

Hivyo mtu alietumiwa kufanya kitendo cha kigaidi hukumu yake ni tofauti na yule alieandaa shughuli nzima ya ugaidi.
 
Katiba mpya ndio SULUHU.. viraka vimetosha
Sidhani kama ugaidi unahusika na katiba mpya.

Ugaidi upo na waweza kutokea wakati wowote.

Ni kazi ya vyombo vya usalama kuchunguza na kubaini dalili za ugaidi.
 
Back
Top Bottom