Mapendekezo ! vyama vya siasa vifutwe, vinaliangamiza Taifa

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,063
Reaction score
12,866
Wanabodi,
Katika nchi yetu tumekuwa na mfumo wa kupata viongozi vya kisiasa kupitia mfumo wa vyama vya siasa na katiba yetu hairuhusu wala kutambua mgombea asiye na chama cha siasa.

Nimekuja hapa nikiwa na mawazo tofauti ambapo nimeweka katika mizania faida na hasara ya uwepo wa vyama vya siasa nimegundua hasara ni nyingi zaidi kuliko faida.

Tumekuwa tukipata viongozi wetu kutoka ndani ya vyama vya siasa hali hii imetuletea matabaka katika vyombo vya maamuzi kuanzia serikali za mitaa mpaka bungeni. Viongozi wanaotokea chama fulani wamekuwa na maelewano na kushirikiana na viongozi wenzao kutoka chama kimoja jambo ambalo si afya kwa maendeleo ya taifa.

Kumekuwa na tabia ya hawa viongozi tunaowapata kutoka vyama vya siasa kutanguliza maslahi ya vyama vyao kuliko maslahi ya taifa. Aghalabu tumeshuhudia wabunge wa CCM wakiitetea serikali katika mambo ambayo yanastahili kukemewa hii ni kwa vile tu serikali ni ya chama chao. Hii ni hasara kubwa kwa taifa na inapunguza uwajibikaji wa serikali.

Vyama vya siasa havina msaada katika kukemea mwenendo mbaya na maadil ya kiutumishi wa makada wao ambao ni viongozi wa umma. Wabunge na hata madiwani wengi utendaji wao wa kazi umekuwa wa kusikitisha na mara nyingine wanatelekeza majimbo yao na kuonekana kwa nadra hadi uchaguzi ukikaribia lakini vyama vya siasa hivi vimekuwa hutaona chama kikimuonya au kumuwajibisha mwanachama wao ambaye ni kiongozi kwa kutotimiza wajibu wake kwa wananchi. Unaweza kusema kazi ya kuwawajibisha wawakilishi wa wananchi ni ya wananchi wenyewe kupitia sanduku la kura lakini je vyama vya siasa vina kaz gani baada ya uchaguzi? Mbona vinaendelea kupokea ruzuku?

Uwepo wa vyama vya siasa unavuruga umoja na mshikamano wa wananchi. Wananchi wanagawanyika kutokana na itikadi hizi za uCCM na UCDM hali hii hailisaidii taifa bali inaliangamiza. Tumesikia mara nyingi watu wakiumizana hadi kuuwana kwa sababu itikadi za kisiasa.

JE VYAMA VYA KISIASA VIKIFUTWA TUTAPATAJE VIONGOZI?

Napendekeza mfumo wa kura za maoni utumike kupata wagombea binafsi katika chaguzi katika ngazi zote.

Mathalani katika ngazi ya mtaa wananchi watapendekeza majina ya watu wanaoona wanafaa kugombea uenyekiti wa kijiji. Baada ya kupatikana majina kadhaa basi waliopendekezwa watapewa muda wa kuchukua na kurejesha fomu za kugombea. Wao wenyewe watatafuta wadhamini . Lakini kwa mtu ambaye ana nia ya kugombea uchaguzi na jina lake halijatwa na wananchi atakuwa na haki ya kugombea lakini itabidi awe na wadhamini mathalani kwa mwenyekiti wa kijiji wadhamini 10. Wagombea waliopendekezwa na wanachi watachukua fom za kugombea bure lakini wagombea ambao hawakupendekezwa watachukua fom kwa malipo.

Ngazi ya Udiwani uwe huo huo wa wananchi kupendekeza majina ya watu wanaoona wanafaa kugombea na mtu mwenye nia ya kugombea na hajapendekezwa achukue fom kwa malipo.

Ngazi ya ubunge wanyeviti wa vitongoj ndio watapendekeza majina ya wanaoona wanafaa kugombea. Watapendekea mtu yeyote yule mwenye sifa zinazotajwa na katiba isipokuwa sifa ya kuwa mwanachama wa chama cha siasa itaondolewa. Mtu binafsi ataruhusiwa kugombea kwa utaratibu uliotajwa juu.

Ngazi ya Urais. Wabunge watapendekeza majina na mtu mwenye nia ya kugombea na hajapendekezwa (mgombea binafsi) utaratibu utakuwa huo huo uliotajwa juu.

Kwa namna hii tutapata viongozi bora zaidi , tutaondokana na mipasho bungeni, mambo ya uchama hayatakuwepo bungeni na masuala ya ruzuku kwa vyama vya siasa yataondoka na vile vile tume ya uchaguzi na polisi wataondolewa majaribuni.

NAWASILISHA.
 
Hakika Kuwe tu na Chama kimoja.
Chama cha Mapinduzi.
Tutaokoa pesa nyingi za Maendeleo.
Wakulima wa Korosho bado wanadai Pesa zao za kuvuja jasho la jembe la mkono.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja kwa asimilia 💯
 
Mfumo unaotufaa ni kama wa urusi,au China,lakini huu wa demokrasia ya magharibi,ni mfumo ghari sana,
Hebu fikiria tuna wabunge 300+,wote wanalipwa na kodi zetu,uchumi wetu hauna uwezo wa kugharamia mifumo kama hii,
Tunachotakiwa kufanya ni kupunguza idadi ya wilaya,mikoa,vyeo kama wakurugenzi,makatibu tawala,idadi ya wizara,
Mfano pesa itakayotumika kuendeaha uchaguzi ujao 2020,kama ingetumika kutoa mikopo kwa vijana wa vyuoni,au tujenge miradi yenye tija kwa wananchi,maji,hospitari nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…