Kabla ya mapendekezo haya sheria ilikuwa inasema atakayekutwa na hatia ya kuomba rushwa ya ngono atakuwa ametenda kosa ambapo adhabu yake ni faini isiyopungua milioni 2 na isiyozidi milioni 10, ama kifungo kisichopungua miaka 5 na kisichozidi miaka 10 au vyote kwa pamajo.
Kwenye mapendekezo serikali imetaka kifungu hicho kibadilike ambapo mtoa rushwa na mpokea rushwa wote watawajibika kwa kosa hilo, lengo likiwa ni kumaliza vitendo hivi vya rushwa ya ngono.
Wanaharakati wa haki za binadamu wamejitokeza kupinga mapendekezo haya na kusema inamnyima haki mhanga kwa kufanya wanyamaze na hivyo vitendo hivyo kuendelea.
Ila tukija upande wa pili, kuna ambao wanakuwa kwenye mipango yao na mambo yakiharibika anaenda kumshtaki kuwa alimlazimisha kutoa rushwa ya ngono la sivyo angemyima stahiki zake. Je, hawa waachwe kutamba na sheria iendelee kuangalia upande mmoja?
Lakini pia kuna ambao wanalazimisha kutoa rushwa, jamaa anaingia kingi baadaye anaenda kuchomwa kuwa alilazimisha kupewa ngono ndio atoe haki, je, sheria kubaki kumuadhibu anayesemekana ameomba rushwa ambaye kwenye kesi hii ni mtu mwenye madaraka/mamlaka itakuwa sawa?
Nadhani haitakua sahihi tukisema sheria iendelee tu kubana upande mmoja. Ki Katiba, hamna mtu anayetakiwa kuwa juu ya sheria, na kila mtu anatakiwa kuchukuliwa sawa na mwingine, yani "everyone is equal before the law" sasa tukianza kutengeneza sheria ambazo zinafavour upande mmoja na kuacha upande mwingine hata kama cases ni chache, tayari tunatengeneza hali ya kuminya au kupendelea upande mmoja.
Kwanza sheria haisemi atakayelazimishwa kutoa rushwa ya ngono, bali atakayetoa au kuahidi kutoa. Hizi cases zipo tu hata vyuoni na makazini, hata kama ni chache. Hao wachache nao lazima sheria iwaguse.
Endapo victim atakua mtoto wa shule ya msingi, hapa hatutaangalia swala la consent, bali sheria ya kufanya ngono na mtoto itafatwa, na mtenda atachukuliwa hatua kama kawaida.
Lakini pia, naona wanaopinga kifungu hicho kipya wamekua wakitetea upande wao wa kuangalia jinsia ya Ke hasa, kwa kuwa imeonekana wahanga wengi ni wanawake. Sheria haitakiwi kuwa hivyo.
Hatujaona wanaharakati kama hawa wakipinga sheria kwa makosa ya Ulawiti pale ambapo anayetenda na mtendwa wamekua wakihukumiwa. Labda kwa sababu ni jinsi nyingine. Sheria imesema wote watakuwa charged, lakini kwenye ushahidi/mahakamani ndio tutapata facts na uamuzi sahihi. Na wala hamna aliyelalamika kwamba sheria hiyo inamfanya aliyelawitiwa asitoe taarifa.
Nadhani, ni sahihi sheria iendelee kuwepo, ili atakayeshitakiwa kwa kosa hilo akajielezee mahakamani, na mahakama itatoa maamuzi.