Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 79
- 1,444
Kwamba tume ya uchaguzi Tanzania @TumeUchaguziTZ imepoteza sifa za kusimamia uchaguzi huru na haki kutokana na mapungufu ya kikatiba yanayompa mamlaka Rais kuteua viongozi na watendaji wa tume hiyo. Kumbuka kwamba Rais anayeteua viongozi na watendaji wa tume pia ni kiongozi wa chama mojawapo cha siasa kinachoshiriki uchaguzi ambao unasimamiwa na wateule wake.
Changamoto kubwa ni kwamba tangu wakati wa Magufuli na sasa kwa Samia dola ndio inayoongoza nchi na sio siasa tena kuongoza nchi. Siasa haina nguvu tena ya kuamua nani awe diwani, mbunge na Rais isipokuwa dola ndio inayoamua. Kura hazina thamani tena kama zamani. Mapungufu ya kikatiba kwenye eneo la uchaguzi kimekuwa chanzo cha dola kuwa na nguvu kuliko siasa na kuharibu chaguzi.
Kutokana na mkwamo huo nilikuwa na mapendekezo kadhaa ya kufanya REFORM kwenye katiba ibara zinazohusu uchaguzi na marekebisho ya muundo wa tume ya uchaguzi itakayokuwa huru. Binafsi naamini ili tuweze kuwa na uchaguzi huru na wa haki lazima tuwe na muundo wa tume ya uchaguzi kama ifuatavyo;
1. Kwamba wajumbe wa tume huru ya uchaguzi watokane na mapendekezo ya vyama vinavyounda TCD, uwakilishi wa taasisi moja ya kiraia kama vile TLS pamoja na taasisi za kidini kwa usawa kati ya wakristo na waislamu.
Nimeingiza vyama vinavyounda TCD hapo kwa sababu TCD inafanya kazi kuwakilisha vyama vyote nchini lakini pia vyama vinavyounda TCD ndivyo mara nyingi vinashiriki chaguzi kwa kuweka wagombea na kwenda field. Kingine ni kwamba vyama hivi ni wahanga wakubwa wa uchaguzi usiokuwa huru na haki.
2. Kwamba kama wajumbe wanaounda tume ni 10 basi TCD kwa sababu ina vyama vitano kila chama kiteua mjumbe mmoja na wajumbe watano wanaobakia wateuliwa na uwakilishi wa taasisi kama nilivyofafanua hapo juu.
3. Kwamba nafasi ya mwenyekiti wa Tume na makamu kwa Tanzania na Zanzibar pamoja na mkurugenzi wa tume zitangazwe wenye sifa waombe halafu TCD kushirikiana na taasisi nilizozitaja hapo juu zifanye usaili na kuwapitisha wenye sifa.
4. Kwamba mwenyekiti wa tume, makamu na mkurugenzi waapishwe na jaji mkuu badala ya Rais.
5. Kwamba baada ya muundo huo ngazi ya taifa kukamilika basi tume hiyo iwe na mamlaka ya kuteua wasimamizi wa uchaguzi ngazi za majimbo. Nafasi za wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya majimbo zitangazwe ili wenye sifa waombe halafu wajumbe wale 10 waliopatikana wa tume chini ya mwenyekiti wake wawafanyie usaili, kuwapitisha, waapishwe kwa hakimu au jaji kisha wapangiwe vituo vya kazi.
5. Kwamba nafasi za wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ambao ndio wanaosimamia uchaguzi ngazi ya kata, maafisa wa uchaguzi na nafasi zingine zitangazwe waombaji waombe na kufanyiwa usaili kisha kupangiwa vituo vya kazi.
6. Kwamba nafasi za wasimamizi wa vituo vya kupigia kura ziwe ajira za muda mfupi nazo ziombwe vilevile.
7. Kwamba watumishi wa tume iwe mwenyekiti, makamu, Mkurugenzi, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi au maafisa wa uchaguzi hawapaswi kuwa waajiriwa wa serikali ama taasisi zingine na kwamba watakuwa ni waaajiriwa wa tume ya uchaguzi tu. Hii itasaidia kuondoa mgongano wa kimaslahi kama ilivyo tume ya sasa.
8. Kwamba tume hiyo mpya itakayopatikana ndio iwe na mamlaka ya kuandaa miswada ya sheria za uchaguzi na kanuni kwa kushirikiana na wadau wa siasa .
9. Kwamba watumishi wote wa tume wawekewe kinga za kisheria kwa kutoteuliwa nafasi nyingine na Rais wakiwa bado watumishi wa tume. Maana mtu anaweza kuharibu uchaguzi maksudi kwa ahadi ya kuteuliwa ukuu wa wilaya, mkoa au ubalozi.
Kwamba baada ya muundo wa tume hii kukamilika yafuate mabadiliko ya sheria za uchaguzi pamoja kanuni. Zikiwemo sheria za kuwawajibisha watumishi wa tume wanapoenda kinyume au kuharibu uchaguzi.
Haya ni maoni yangu tu na yanaweza kuboreshwa ili tukapata tume huru zaidi.
Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.