Mapendekezo ya mishahara kwa Watumishi Tanzania

Mapendekezo ya mishahara kwa Watumishi Tanzania

Davan

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2020
Posts
1,125
Reaction score
1,413
Yafuatayo ni mapendekezo yangu kwa serikali kuhusu viwango vya mishahara vya watumishi wa umma.

1. Watumishi wenye stashahada/diploma basic salary iwe 1,200,000/=
2. Watumishi wote wenye shahada ya kwanza\degree basic iwe 1,700,000/=
3. Masters na PH D, hizi ziachwe tu kwenye vyuo vikuu na upande wa afya.

Walau viwango hivyo vinaweza kumfanya mtumishi aishi bila stress tofauti na sasa. Pia hivyo viwango vitumike kwa wizara na taasisi zote za umma tofauti na sasa hivi ambapo kila taasisi ina mishahara yake mambo yamekuwa vurugu tu. Degree hiyo hiyo taasisi Y inalipwa laki 7 wakati taasisi Z inalipwa 1.5 mill.
 
Ninavyofahamu Mimi kwa uzoefu wa kuwafanyia '"intelijensia" ya muda mrefu , Mwalimu ni yule wa "astashàhada" hao wengine ni mbwembwe tu !
Napendekeza waanze na "take-home" ya Milioni 1.5 !
 
Sawa.
Ila ikumbukwe kuwa mtumishi yeyote anayekaa kusubiria nyongeza ya mshahara ndani ya hii miaka 10 ya Mheshimiwa basi huyo mtumishi hana akili timamu.
Namfananisha na msafiri anayekwenda Arusha kutokea Dar lakini asubuhi anaacha kwenda Ubungo anakwenda Kigamboni
Wajumbe wa bodi ya mishahara wapo humu wataona. Naamini hili linawezekana maana muda sio mrefu tutaanza kuuza umeme nje ya nchi kutoka STIGLER
 
Ninavyofahamu Mimi kwa uzoefu wa kuwafanyia '"intelijensia" ya muda mrefu , Mwalimu ni yule wa "astashàhada" hao wengine ni mbwembwe tu !
Napendekeza waanze na "take-home" ya Milioni 1.5 !
Hiyo take home yako ni sawa na take home ya mtumishi anaekaribia kistaafu kwa sasa
 
Mshahara hujawahi kumfanya mtu aishi vizuri, ukilipwa hata laki lakini una kipato kingine unaishi vizuri sana.
 
Kizazi Cha watanzania kijacho labda....lkn kwa hiki Cha uncle Maaagu....aaaahh thubutu
 
Mshahara hujawahi kumfanya mtu aishi vizuri, ukilipwa hata laki lakini una kipato kingine unaishi vizuri sana.
Hiko kipato inabidi kiwe kikubwa kuliko mshahara..... Otherwise kuna watu unawatosha fresh tu....
 
Muwe wazalendo na mpunguze tamaa ya pesa, mkijengewa flover, SGR na vituo vya afya hiyo ni zaidi ya nyongeza ya mshahara.

Hata Rais aliwahi kusema mshahara wake haumtoshi.
 
Kwan sasa hv mishahara ikoje kwenye hizo viwango vya elimu kwa yule anayepokea mshahara wa chini na yule anayepokea mshahara wa juu.?
 
Sawa... But kuna watu wanadhani walimu wa astashahada hawana uwezo wa kufundisha watoto wao,ngoja niwaeleze kitu hakuna walimu bora kama hawa wa cheti walimu wengi wenye digree wanajiona kuwa wao ni kila kitu ko hawastahili kuwafundisha watoto wetu but angalia maprofesa wengi wamefundishwa na walimu wa cheti na wale wa upe coz hawa ni walimu wanaotambua thamani ya ufundishaji na kile wanachowafundisha watoto wetu.
Mimi naongea hili nikiwa na ushahidi kuna mwl alikuwa anafundisha drs la 1&2 baadae akastaafu ikabidi tumpe mwl wa digree aliyetoma sec kuja msingi ajabu tulipata watoto wengi sana wasiojua kusoma tofauti na alivyokuwepo mwl wa UPE..
 
Kwan sasa hv mishahara ikoje kwenye hizo viwango vya elimu kwa yule anayepokea mshahara wa chini na yule anayepokea mshahara wa juu.?
Viwango vya sasa hivi kwa level ya degree
1. Wizarani na halmashauri laki 7.
2. Taasisi/mashirika/wakala/mifuko ya hifadhi huku kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake kuanzia 1.2 - 1.8 mill
 
Muwe wazalendo na mpunguze tamaa ya pesa, mkijengewa flover, SGR na vituo vya afya hiyo ni zaidi ya nyongeza ya mshahara.

Hata Rais aliwahi kusema mshahara wake haumtoshi.
Hakuna mwenye tamaa ila sio sawa malipo yatofautiane sana
 
Back
Top Bottom