Mapendekezo ya muundo wa baraza la mawaziri - 2010-2015

Kwa muda mrefu tumeweka Madini na Nishati mahali pamoja kiasi kwamba ni vigumu kuzionea zikitenganishwa. Binafsi ninaamini Madini ni sekta kubwa mno kwa nchi yetu kiasi kwamba kuiweka na wizara nyingine hatuitendei haki. Nishati ni sekta kubwa na yenye kugusa watu na taasisi mbali mbali (zote) nahivyo kuiweka na sekta nyingine kubwa ni kutoitendea haki. Matatizo ya nishati na madini ambayo tumeyapata miaka hii naamini kiasi kikubwa ni kutokana na kuunganishwa kwa sekta hizi mbili na hivyo kuzifanya zikose mkazo unaostahili. Wakati umefika tuzitenganishe kama tunataka kuzisimamia vizuri.
 

It make sense.............

revised list is as follows.....
1. Ministry of Finance, Economic Planning and Public Service
2. Ministry of Foreign Affairs (includes EA portfolio)
3. Ministry of Education, Science and Technology
4. Ministry of Health
5. Ministry of Legal Affairs
6. Ministry of Housing, Lands and Surveys
7. Ministry of Agriculture, Livestock and Marine Resources
8. Ministry of Labour and Social Development
9. Ministry of National Security (Polisi, TAKUKURU, UwT, Magereza na Uhamiaji)
10. Ministry of Public Works, Aviation, Telecommunication and Transport
11. Ministry of the Environment, Energy (Gas, Oil, Coal? au?) and Water Resources
12. Ministry of Tourism
13. Ministry of Information,Youths, Sports and Culture
14. Ministry of Trade and Industry
15. Ministry of Local Governments
16. Ministry of Defense & National Service
17. Ministry of Minerals/Mining

Bado utaona Wizara 20 ni maximum..........na si lazima Wizara zote ziwe na manaibu.............

Pendekezo:
Manaibu Waziri wawe pia wanaingia ktk Cabinet............it does not make sense kama hawaingii............
 
Ingependeza zaidi akatuwekea japo mawaziri amabao tumewaona serikali iliyopita na kuujua utendaji wao. Hawa wapy wawezaacha blank!
 
nadhani ni mchanganuo mzuri. I strongly second your view and opinion!
 


Mwanakijiji:

  1. Usalama wa taifa inakuwa chini ya rais. Hivyo hakuna haja ya kuwa na wizara yake.
  2. Sheria na mambo ya ndani ni walewale
  3. Kwa sababu sasa hivi serikali ni regulator na sio mzalishaji basi hizi ziungane
    • Wizara ya Nishati na Raslimali za Mafuta - Ministry of Energy and Oil Resources
    • Wizara ya Madini - Ministry of Mining
  4. Hizi zifuatazo ni zilezile
    • Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi - Ministry of Agriculture, Livestock and Fisheries
    • Wizara ya Maji na Usalama wa Chakula - Ministry of Water Resources and Food Security
  5. Hizi nazo zinafanana
    • Wizara ya Afya - Ministry of Health
    • Wizara ya Maendeleo ya Jamii - Ministry of Community Development
  6. Kutokana na kuwa siku hizi serikali haifanyi umachinga hizi pia ziwe pamoja
    • Wizara ya Fedha na Uchumi - Ministry of Finance and Economic Affairs
    • Wizara ya Biashara, Viwanda, Masoko, na Uwekezaji - Ministry of Trade, Industry and Investments
 
Zakumi nimekupata.. lakini nikiangalia naona kuna kubananisha sana; labda tuwe na baadhi ya wizara na nyingine ziwe taasisi huru kabisa.
 

Imekaa vizuri ila mambo ya usalama wa Taifa haya yanatakiwa yawe chini ya raisi moja kwa moja, hivyo wizara ya usalama wa Taifa iwe chini ya ofisi ya raisi
 
Mawazo yako ni mazuri sana,ingawa naamini serikali ya CCM si serikali sikivu na haiwezi kamwe kukubaliana na mawazo kama haya.Mimi naona katika pendekezo lako la kuwa na wizara 23 ni zuri.Lakini,tungeweza kupunguza zaidi na kubaki na wizara 22 kwa kuunganisha wizara za "Wizara ya Nishati na Raslimali za Mafuta,na Wizara ya Madini"na kuwa "wizara ya nishati na madini" kama ilivyo hivi sasa.Sehemu nyingine ambayo hukuigusia ni suala la manaibu waziri,mimi nafikiri hakuna haja ya kuwa na manaibu waziri zaidi ya mmoja katika wizara moja,kwani kufanya hivyo ni kuongeza garama za uendeshaji wa serikali zisiokuwa na tija yoyote.
 
Haya ni mawazo mazuri mzee, big up
 
kwa nini umetanganisha usalama wa chakula na kilimo?

Kwa nini usalama na uokoaji vinakuwa wizara tofauti?

kwa nini kila siku tunatenganisha utawala na sheria?
 
ngoja tusubirie tuone itakavyokua ahsante mwana kijiji mzee wetu kwa mchango wako

Mzee Gomezi
 
kwa nini umetanganisha usalama wa chakula na kilimo?

Kwa nini usalama na uokoaji vinakuwa wizara tofauti?

kwa nini kila siku tunatenganisha utawala na sheria?

Companero.. wewe ungependa ziwe vipi? ndio maana ya kugonganisha vichwa.
 
Wewe si miongoni mwa wale wasiomtambua Rais?! Sidhani kama atautambua ushauri wako, kwa sababu huonyeshi kuwa na nia nzuri na Rais wetu.

"..... akamjibu, Kama nimesema vibaya, ushuhudie ule ubaya; bali kama nimesema vema, wanipigia nini?" Yoh.18:22-23. Aaahh, Kumbe yalishaandikwa miaka mingi tu huko nyuma!!!!
 

MMJ,
Asante kwa pendekezo zuri na lenye tija kwa Taifa. Lakini nimepata infos za uhakika kwamba mkulu anakuja na baraza la mawaziri 33.
 
Ulaji usiwe ndio kigezo cha kuundwa wizara. Tanzania inataka kuona zaidi ya watu wachache kujinufaisha
 
Mapendekezo haya yanapunguza ulaji kwa karibu watu 30 kutoka ilivyo sasa. Hatari moja ambayo tusije kuiingia vibaya ni kusema kuwa tupunguze tu idadi ya wizara tukiamini itaennda na effiency wakati sehemu nyingine za mfumo wetu zimebakia vile zilivyo. Kwa mfano, kuna taasisi au vyombo ambavyo vimeundwa ambavyo kisheria vinatakiwa viwe chini ya waziri hivyo Rais yeyote anapokuja anajikuta anaviweka chini ya wizara fulani kwa mfano "Habari". Binafsi Habari isingekuwa na waziri yeyote na kuachwa iwe taasisi huru na isisimiwe na waziri yeyote. Lakini sheria yetu ya Magazeti n.k zinadokeza wazikuwa yupo Waziri anayeshughulikia masuala ya habari!

Lakini vile vile katika kutaka udogo tusije tukawa na baraza dogo mno katika namba lakini watu wake wamerundikiwa mengi mno kiasi cha kuwa inefficient. Ndio maana nimeweka hapo juu kabisa misingi ya kwanini mapendekezo haya yako jinsi yalivyo. Udogo to for the sake of udogo au kupunguza gharama za kuendesha hakuhakikishi kuwa baraza litakuwa more effective.
 
Mzee, mchango huu ni mbegu bora kwa ajili ya ustawi wa taifa letu. Twendeni kwa mtindo huu, Tanzania yenye neema inawezekana. Thank u.
 
Wizara nyingi ni majina tu hurudia shughuli zile zile tu na hivyo kuleta migongano ya kiutekelezaji.............mapendekezo ya Wizara ziwe 15 tu nazo ni;-

1) Utawala bora

2) Ulinzi na usalama

3) Mambo ya Nje

4)Miundo Mbinu

5) Mambo ya Ndani

6) Elimu

7) Rasilimali za asili na utalii

8) Kilimo

9) Fedha na Mipango

10) Afya

11) Utamaduni na Michezo

12) Maji na Mifugo

13) Nishati

14) Ardhi na Makaazi

15) Madini
 
Ni maoni yangu lakini naomba mchango wa wanaJF. Kuna ulazima gani ya Rais kuchagua mawaziri from wabunge. Tumeona mara nyingi mawaziri wanaochaguliwa sio wale wenye uelewa wa mambo yanayofanyika kwenye wizara zao. Inabidi atumie hata mwaka ili aelewe kinachoendelea wizarani. Then after 1 year Rais akiamua tuu anaweza kumuhamishia wizara nyingine, then semina elekezi inaanza tena.
Maoni yangu; kwa nini wasichaguliwe watu kutoka kwenye jamii ambao wanaweza kufanya kazi hii na wah. wabunge wabaki nkuwa wabwakaji wa kuinyoshea kidole serikali katika utendaji wake? Hii inaweza kutuondelea watu wanaogombea ubunge kwa ajili ya kuja kuwa mawaziri tuu instead kuwatumikia wananchi!
Nawakilisha!!
 
Katiba yetu mbovu ndo inaelekeza hivyo.La kwanza liwe ni kubadilisha katiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…