Mapendekezo ya Wadau kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yaliyowasilishwa Bungeni chini ya Kamati ya Miundombinu

Mapendekezo ya Wadau kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yaliyowasilishwa Bungeni chini ya Kamati ya Miundombinu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Maoni haya yanawasilishwa kwa pamoja na taasisi zifuatazo;
1. Jamii Forums (JF)
2. Tanganyika Law Society (TLS)
3. Legal and Human Rights Centre (LHRC)
4. Tanzania Mobile Network Operators Association (TAMNOA)
5. Tanzania Bankers Association (TBA)
6. Twaweza
7. Tanzania Human Rights Defenders (THRDC)
8. Multichoice Tanzania

Maendekezo kwa Ujumla
  1. Bodi iondolewe. Tunapendekeza bodi iondolewe ili kupunguza Gharama za uendeshaji wa Tume inayoundwa chini ya Sheria hii. Badala yake tunapendekeza kwamba Tume isimamie shughuli zote za ulinzi wa taarifa binafsi na faragha bila kuingiliwa na mamlaka yoyote.
  2. Tunapendekeza pia kwamba Mkurugenzi akishateuliwa na kuidhinishwa na Bunge basi awajibike kwa Bunge. Hii itasaidia Tume kuwa huru na kupimwa uwajibikaji wake na Bunge.
  3. Mpangilio wa sura. Tunapendekeza kwamba Sura ya 8 iwe Sura ya 3 ili kuweka mtiririko mzuri na wenye kuleta maana.
  4. Tunapendekeza iwepo sehemu inayoweka utaratibu wa kufanya tathmini ya athari za kutoa taarifa (Data Protection Impact Assessment) na isomeke kama mfano uliombatanishwa hapo chini (mwishoni)
  5. Tunapendekeza kwamba ridhaa ya Maandishi isiishie kwenye taarifa nyeti tu; badala yake itumike kwa taarifa zote binafsi.
  6. Haki ya Mhusika wa Taarifa binafsi kupata nakala ya taarifa zinazokusanywa au zilizochakatwa haijaainishwa katika Muswada
  7. Muswada haujaweka haki ya kuomba idhini ya haki ya taarifa binafsi kuhamishwa kwenda kwa msimamizi wa mirathi au mwakilishi wa kisheria (Right of Transmission)
  8. Tunapendekeza kuwepo katika Sheria hii kifungu kinachosema wazi kwamba kama kuna mgongano wowote kati ya sheria nyingine na sheria hii, basi sheria hii itatamalaki kwa masuala yote ya taarifa binafsi na faragha.
  9. Tunapendekeza kuwepo na Masharti ya Mpito ili kuwapa wadau muda wa kujipanga kutekeleza matakwa ya sheria hii.
  10. Tunapendekeza maneno ‘Maslahi ya Umma’ yapewe tafsiri maalum kwa sababu yametumika mara tatu ndani ya muswada
  11. Tunapendekeza maneno ‘Usalama wa Taifa’ yapewe tafsiri maalum kwa sababu yametumika mara mbili ndani ya muswada
  12. ‘Ridhaa ya mhusika wa taarifa’ (consent) ipewe tafsiri kuepusha mkanganyiko wakati wa utekelezaji wa sheria
  13. Uficho/faragha/kutokujulikana kwa mhusika wa taarifa (anonymization) wakati wa matumizi ya taarifa binafsi kibiashara haujapewa kipaumbele katika Muswada. Tumeambatanisha mfano wa kifungu pendekezwa hapo chini.
  14. Mdhibiti wa taarifa binafsi hajatajwa kokote kwenye muswada (Data Controller). Tunapendekeza aongezwe kwenye vifungu husika kama tulivyopendekeza kwenye bango-kitita. Aidha, tafsiri iwekwe kwenye kifungu cha tafsiri ya maneno.
  15. Kifungu cha 5 kinachozungumzia Misingi ya Ulinzi wa Taarifa hakijajumuisha Msingi wa Uwajibikaji. Tunapendekeza msingi huu uongezwe na isomeke “Mdhibiti wa Taarifa Binafsi atawajibika moja kwa moja kwa uchakataji wa taarifa binafsi ikijumuisha wachakati na wawakilishi wake wakati wa uchakataji wa taarifa binafsi chini ya maelekezo yake”
  16. Tunapendekeza kiongezwe kifungu kipya baada ya kifungu cha 39 kitakachotoa nafasi ya wahusika katika malalamiko kumaliza mgogoro wao nje ya utaratibu wa Tume na Mahakama ili kupunguza mrundikano wa mashauri kwa Tume. Tunapendekeza kifungu hicho kisomeke kama mfano ulioambatanishwa hapo chini.
  17. Tunapendekeza kifungu cha 65 kibadilishwe badala ya kuweka ulazima kwa kila mkusanyaji, mchakataji na mdhibiti wa taarifa binafsi kuwa na sera ya kukusanya, kuchakata, kudhibiti na kulinda taarifa binafsi; kazi hiyo ifanywe na Tume kwa kuweka sera ya mfano (standard) ambayo itafuatwa na watajwa wote hapo juu.

Unaweza kusoma Muswada uliopendekezwa na serikali pamoja na maoni ya wadau kwa kina kwenye viambatanisho (attachments) hivi:
 

Attachments

Back
Top Bottom