Tupe mifano mitatu waliofanikiwa kwenye mtandao na wanaishi kwa raha mpaka sasa
Poa takitafuta ila nimeona watu kama watano hivi wanaishia kuumia mioyo tu kwa uhusiano wa aina hii ndio maana naona haulipi sana ingawa kuna wengine wamefanikiwa. ni kwa mtazamo wangu tuhapa lazima tujue lengo la umtafutae ni lipi je tamaa ama wataka kweli mwenzi ktk maisha? Kama si kwa tamaa bac mahusiano yanaweza kuanza popote ndio maana nimekushauri utafute hicho kitabu
Unajua kumchunguza mtu kwenye net inakuwa ngumu japo mtakuwa mnaambiana interest zenu na mambo mengine ila mkija kuonana tu mnaweza amua muoane kwa kuoneana huruma au kwa tamaa labda muonekano umekuzingua hapo unafanya chapchap, mikucha inakuja kutokea wakati mnaishi sasa pamojaInawezekana kupata mke kwa njia hii lakini wake/waume inabidi mchunguzane kweli la sivyo mtapoteana
Inawezekana bwana mbona wangu nimempata kupitia mtandaoni tena hapa JF :bange::bange: