mapenzi na ndumba

Mwanamke tu ww mwenyewe ni ndumba tosha kabisa katika mapenzi izo nyingine mbwebwe za dunia! Mtalishwa na visivyolika bure!
 
naskia hayo mambo yapo kweli lakini tatizo ya hizi dawa huisha nguvu baadae
 
Elimu ndogo ndio shida. Hawajiamini , na makundi. Ukisikia wayaongeao salooni utachoka kabisa.
 
Kwa kweli mtu huwa hajiadhali na dudu lisilong'ata bali hujiadhali na dudu ling'atalo.SO yatupasa tutambue kuwa wengi wa wanawake wanaamua kwenda kwa waganga ni kutokana na kutoeleweka kwetu m2 unachelewa kazin mara simu za ajabu haziishi usiku wa manane mara shutuma ya nyumba ndogo n.k hivi vyote vinampelekea mwanamke ambaye bado ana HAJA na wewe kuangaika huku na kule kukufanya wewe utulie na muendelee kujenga familia pamoja.IKUMBUKWE KUWA MWANAMKE HAWEZI KUKUENDEA KWA MGANGA KAMA HANA HAJA NA WEWE.HIVYO INATUPASA TUWAPE SUPORT YA KUACHA TABIA HATARISHI ZA NDOA ZETU ITASAIDIA KUTOKULA HAYO MANYAMA YANAYOTUMBUKIZWA KWENYE NANII zao.angalizo:Chagua mwanamke angalau ana misingi ya kidini itasaidia kupunguza tatizo hili.asanten
 
Mmm! Mungu atustiri na watoto wetu wakiume,mambo kama haya sijui limbwata sijui nini yote yanatokea na yule mwanamke asie jiamini kwa mumewe au mpenzi wake,kama unajituma kisawasawa na mbunifu mzuri wa mambo,kauli nzuri mkarimu kwa umpendae kwengine akafate nini?
Lakini mume akiwa nyumbani unamuliza leo hutoki manake bwana ww kwa mwendo kama tyre gari! au mume yuko nyumbani ww unatoka unakwenda kwa shoga kuongea kuhusu kikao cha harusi,au uko nyumbani ww uko busy na cm sms kwakwenda mbele,mwenzio akimpata anampa Raha ndio unakumbuka shuka kushakucha matokeo yake unaishia kwa babu,babu anakupa dawa anakwambia hii dawa lazima nianze kuiweka hapa kwenye uume wangu niweke huko halafu na wewe ukampe mumeo,yote hayo kwa ujinga wako2.
 
Yupo kibinti kimenipitisha njia moja mara tatu.Kinakwenda Tandika huko na kimepeleka nguo zangu kwa mganga yaani sina hamu.Hivi visister doo mmmmmmmhhhhh hata kuviona sitamani

Ehee ikawaje?
 

tehe tehe umenikuna mbaya.we kiboko aisee
 
Niliwahi kusikia siku za nyuma Clouds FM, njia panda... small house moja alimwekea mume wa mtu nyama ya ng'ombe kunako ikulu (kwenye nyeti) kwa siku 7, Ile nyama akachomewa, akapewa. Baada ya siku kadhaa, yule bwana akahamia kwa small house na hata kazini akawa haendi, na mwisho wake akawa kama zuzu, na kazi akafukuzwa,
 
mtalishwa sana tu mmezidi mno macho yako juu juu kama mkungu wa ndizi, mtaipata.
 

yanayotokea sana haya,kama ni limbwata,shuntama au ujinga wa mtu sijui,lakini yapo sana inaitwa kulowea.
 
Elimu ndogo ndio shida. Hawajiamini , na makundi. Ukisikia wayaongeao salooni utachoka kabisa.

Mfamaji,wanawake wasomi kibao wanakwenda kwa babu aisee.
 
mtalishwa sana tu mmezidi mno macho yako juu juu kama mkungu wa ndizi, mtaipata.

sasa sangoma ndo atatufanya tuache? Lol kama moto bati chini ni bati chini tu.
 

wape vipande vyao Mkuu!
 
kabisa nakubaliana na wewe cantalisia watalishwa mpaka nyama za paka
 
Bishanga haya mambo yapo sana na kwenye jamii zetu hizi kudanganyana kwingi sana na wanaamini sana haya mambo ambayo kwa hakika hayasaidii. Na hao waganga ni wadanganyifu sana hawana lolote na hata madawa wanayotoa mengine ni ya uwongo ni miti na maganba tuu wametoa kwenye mti wanakupa kama dawa
 

ni tatizo la mob mentality,akianza mmoja baadae genge zima linahamia kwa babu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…