Mapenzi vyuo vikuu: 90% ya wanachuo wameoana; 80% wajawazito.

Mapenzi vyuo vikuu: 90% ya wanachuo wameoana; 80% wajawazito.

Kimbori

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
6,112
Reaction score
4,540
Kuna Dean wa Faculty ya ICT katia chuo kimoja (sitotaja jina la chuo) alikuwa anasimulia maswaibu anayoyapata katika kazi yake.
Alisema ya kwamba anahudumiua wanachuo 120, takribani 90% ya wanachuo walio chini yake wanachuo, hususani wanachuo wa mwaka wa tatu (walio mwaka wa mwisho wa masomo) hao wameona.

Wanachuo hao wameona au kwa ndoa rasmi au kwa mmoja kuhamia kwa mwingine kwa muda mrefu (wanaishi pamoja) bila hata ya wazazi/walezi wao kujua. Kati ya 'wanandoa' hao, 80% ya wasichana ni wajawazito, wengi wao wakiwa ni wametoka sekondari moja kwa moja.

Kutokana na ndoa na ujauzito wanandoa hao wamekuwa wakipangiana muda au vipindi vya kuhudhuria masoma, kisha hufundishana wao kwa wao. Wasichana waliopata ujauzito kwa mara ya kwanza, kutokana na kashikashi za kulea ujauzito na ugumu wa masomo, wanatamani kuahirisha masoma.

Kibaya zaidi ni kwamba ufaulu umepungua sana (kwa kuwa hawahudhurii masomo ipasavyo) kiasi cha kutishia utendaji kazi wao baadaye.

Je kwa hali kama hii tutarajie wafanyakazi bora?
 
Dah!mkuu hiyo ni fashen siku hizi hapa nilipo karibu kila mwanafunzi wa 2 na 3 year wa kike ana kitumbo.
 
uongoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
ajafanya reseacrh anaongea tu
 
Its true buddy hata uku kwetu saut mambo ni yale yale ila cwez kuwalaumu kwan ni watu wazma na pia umri unarhusu chamsingi wawe tu waaminifu kujiepusha na magonjwa.
 
Its true buddy hata uku kwetu saut mambo ni yale yale ila cwez kuwalaumu kwan ni watu wazma na pia umri unarhusu chamsingi wawe tu waaminifu kujiepusha na magonjwa.

Hivi nini tafsiri ya mtu mzima wandugu?
Kuwa chuo ndo utuuzima?
Je kuwa chuoni ndo fursa ya kungonoka kila uchao, tena bila ya kinga?
Nafikiri kuwa mtu mzima ni pamoja na kuwa na uwezo wa kufanya mambo kwa wakati sahihi.....since vyuoni tunafuata elimu ni vema tukaweka bidii huko ili hatimaye utoke hapo ukiwa umeiva ipasavyo.
Social life inaendelea lakini isiwe kwa kiwango cha kuamua kuwekana kinyumba kabisa na mimba kutiana.
 
Japo wana haki ya kuoa na kuolewa, wasi wasi wangu ni kwamba:

Moja, kutakuwa na taifa la wasomi wasio na ujuzi wa kutiosha kwa kuwa "wanadoa" hao hawana muda wa kutosha kushughulikia elimu.
Pili, watoto watakaozaliwa wapo katika hatari kiafya kwa kuwa kulea ujauzito huku mtu anakula chipsi mayai bila hata matunda.

Tatu, wanandoa hawa hawajaiandaa au kuandaliwa kuyakabili maisha, hususani baada ya kuhitimu, hivyo kuongeza idadi ya ndoa zinalovunjika.

Nne, wengi wao hawajatoa taarifa nyumbani au kwa walezi wao hivyo kutokuwa na baraka za wazazi/walezi.
 
Hili swala lipo kweli vyuo vikuu, binafsi nmemaliza chuo 2012 na nakumbuka katika mwaka wetu ni mabinti weng sna walkuwa wajawazito na weng pia kuishi unyumba huku familia zao zikiwa hazina taarifa, so ni km mtindo mtindo wa maisha ukawa pale chuoni!
 
Nadhani ugumu wa maisha na kukosa maadili ndio kumewafikisha hapo.
 
Hao ndo wale mwisho wa siku wanaishia kupata; Mwanaume-GPA 1.8 na Mwanamke-GPA 1.8, ukijumlisha unapata GPA 3.6.
 
Japo hayo yapo Naona kama umezidisha eti 90%? . Consequencies za hayo yote ni utata katika ndoa baada ya masomo. wasichana wengi wanaomaliza vyuo watakataliwa na wachumba kwa hofu kuwa si waaminifu. Ndoa nyingi zitasambaratika baada ya muda mfupi. Kwa hivi matatizo mengi ya kijamii yatazuka.
Nashauri kuwe na umoja wa wanawake/waschana katika vyuo kujifunza na kujielimisha nafasi yao na umuhimu wa nafasi yao. Wanawake wakigoma kuwa rahisi wanaume watajifunza adabu na jamii itabadilika na heshima kurudi.Wasomi ni lazima waaminike!
 
Mtoa mada jitahidi kutafiti zaidi utagundua kwamba ndoa hizo hazilengi kuishia mbali zaidi ya hapo chuoni, haya ni maisha yenye kukusudiwa kusaidiana chuoni. Hao wanaopeana ujauzito wanatengeneza taifa la mtaani!
 
Sina uhakika sana na hii maada asilimia 80 mkuu ni kubwa sana,maana yake katika kila watu kumi basi nane ni wajawazito,sidhani kama ni kweli mbona,wajawazito wapo lakini asilimia ni kubwa mno
 
Back
Top Bottom