Mapenzi ya kweli yapo

mshamba_hachekwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2023
Posts
20,704
Reaction score
66,337
Leo wakati napitapita mtandaoni nimekutana na hiki kisa nimeona nikilete humu MMU;

Kisa hiki ni hadithi ya ukweli ya mapenzi kati ya bibiye Kate na mumewe Godfrey, ambaye anasemekana kuwa ndo mwanaume mwenye sura mbaya kuliko wote duniani.


Kate alipokwenda kumtambulisha Godfrey nyumbani kwao, ndugu zake walimkataa wakidai kwamba ana sura mbaya sana, Pia marafiki zake walimsema sana kwamba alikosea kuchagua mume.
Lakini Kate aliamua kuishi nae bila kupata baraka kutoka kwa wazazi, na walifunga ndoa.


Wameishi kwenye ndoa zaidi ya miaka 25 sasa na wamebarikiwa watoto 4.

Alipohojiwa, Kate alisema haya kuhusu wakati mahusiano yao yalipokua yakipitia misukosuko;

"Watu wanasema sisi sio watu wa kutoshana lakini nilikuwa nampenda. Nilijua hana uwezo hivyo niliangalia zaidi ya sura yake. Tulipoanza kuchumbiana, mawasiliano yetu yalikuwa sawa na niliona uaminifu kwake, na hadi leo, haijawahi kubadilika."

Mwaka 2002 Godfrey aligombea kwenye mashindano ya sura mbaya, na akaibuka mshindi wa kwanza. Kate anasema alifurahishwa sana na usHindi huo.


 NB: Godfrey alipata wake wengine, jumla ya watoto wao na wa Kate ni 8.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…