Mapenzi ya kweli!

Kaunga

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2010
Posts
12,529
Reaction score
13,494
Wana MMU huenda tukajifunza kitu hata katika kipindi hiki cha mapenzi ya vitu au convinience!

Kuna couple moja ilikuwa haina uwezo wa kifedha iliyoishi huko Brazil. Kipindi cha Noel ambapo wenzetu wanatabia ya kupeana zawadi kilipofika, kila mtu aliumiza kichwa ampe mwenzake zawadi gani.

Mke ambaye alikuwa na nywele nzuri na ndefu (ingawa hazikutunzwa vizuri) aliamua kwenda kuziuza (ili kina King'asti wanunue) na kumnunulia mumewe mkanda wa saa yake ambao ulikuwa umekatika.

Huku nyuma mume naye aliamua kwenda kuuza ile saa isiyo na mkanda na kumnunulia mkewe brush ya nywele na mafuta ili nywele za mkewe zizidi kupendeza.

Walivyofika nyumbani Mke kafunga lemba kichwani na mume kaficha zawadi yake. Siku ya kufungua zawadi ilivyofika mama anaona brush na mafuta ya nywele ambazo hana, na mume anapata mkanda wa saa ambayo hana.

Mtaconclude wenyewe!
Robo weekend njema!
 
mmmh, haya mapenzi yamekuwa adimu sana, sasa hivi ni 1+1=11.

Sijui ni lini yatarudi
 
ndiyo maisha ya ma-surprise hayo... huwa siyapendi sana, though, huwa naona yako artificial mno
 
Khaa!Aliyeuza cheni kapewa hela bandia,aliyetoa hela kapewa cheni fake!. . Ngoma droo,mbwa kala mbwa!
 
mmmh, haya mapenzi yamekuwa adimu sana, sasa hivi ni 1+1=11.

Sijui ni lini yatarudi

I know, ila hiyo ni true story!
JF ni mimi na Eiyer tu ndio twaweza hata kuuza jicho ili kumsitiri mwingine!
 
ndiyo maisha ya ma-surprise hayo... huwa siyapendi sana, though, huwa naona yako artificial mno

Lakini zaidi ya suprise, huoni mdada kuuza nywele zake kwa ajili ya mumewe ni gesture iliyo juu sana?
 
Safi sana. Mapenzi ya kweli hutoka moyoni na kukufanya umjali mwenzako bila kuangalia shida zako!

Nywele zitatunzwa na kuota halafu zitauzwa tena na saa mpya ya baba itanunuliwa! Na maisha yataendelea
 
Khaa!Aliyeuza cheni kapewa hela bandia,aliyetoa hela kapewa cheni fake!. . Ngoma droo,mbwa kala mbwa!

Hny, mwisho wa siku zawadi ambayo kila mtu kapata ni true n unselfish love; which is zawadi kubwa kuliko kitu chochote duniani!
 
Safi sana. Mapenzi ya kweli hutoka moyoni na kukufanya umjali mwenzako bila kuangalia shida zako!

Nywele zitatunzwa na kuota halafu zitauzwa tena na saa mpya ya baba itanunuliwa! Na maisha yataendelea

Nakubaliana nawe mazima; upendo adimu sana huo, hasa siku hizi mmoja anapojitoa kabisa na mwingine anategeshea tu au anapass time! Nayatamani sana haya mapenzi, l wish nitapata wa kushare naye!
 
Nakubaliana nawe mazima; upendo adimu sana huo, hasa siku hizi mmoja anapojitoa kabisa na mwingine anategeshea tu au anapass time! Nayatamani sana haya mapenzi, l wish nitapata wa kushare naye!

Kila mmoja anatamani mapenzi ya kweli shida ni jinsi ya kuyapata hasa katika kizazi hiki cha doti com. Mungu akusaidie upate mpenzi wa kweli sawa sawa na mahitaji ya moyo wako.
 
sasa mie nisemeje?

Mie niko tayari kata mkono na yeye yuko tayari kata mguu.

I know, ila hiyo ni true story!
JF ni mimi na Eiyer tu ndio twaweza hata kuuza jicho ili kumsitiri mwingine!
 
sasa mie nisemeje?

Mie niko tayari kata mkono na yeye yuko tayari kata mguu.

Mguu upi wa kati? Hawezi hata kama anakuona unakata roho aise! LOL
 
Katika zama hizi za demokrasia ya mapenzi, Japo kila mmoja alikuwa na lengo zuri ila baada ya kufungua zawadi lazima lawama zingekuwepo, kwa nini umeuza ile saa bila kunishirikisha, kwanini umekata nywele bila kunishirikisha, mwisho kununiana na cku kuharibika.
 
Ni kweli aisee, ila hopefully mwishoni watapata meseji iliyondani zaidi ya saa na nywele. Ila story hii ilinitouch sana!
 
hakuna kitu inaitwa mapeni ya kweli, usijidanganye zama hizi ni wizi mtupu.

Jitunze ili ujifurahishe mwenyewe sio mpenzio... copy that.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…