Mapenzi yameisha au nimekosea nini?

Mapenzi yameisha au nimekosea nini?

Pedrz

Member
Joined
Apr 2, 2021
Posts
89
Reaction score
116
Wana ndugu Habari za muda huu, naombeni ushauri wenu wakati kama huu naona mtanisaidia kwa mawazo pia

Na Mpenzi wangu tulipendana sana na penzi letu sasa hivi lina kama miaka 4 Na kama hakuna shida yeyote iliyotupata tukashindwa kuitatua na mapenzi kuendelea lakini hii ya sahv naona imekuwa serious sasa

Mwenzangu kwao ni lastborn na mm ni firstborn kwahyo matatizo kidogo tu yakitokea kwenye mahusiano yetu anayapeleka home nimeshamkanya lakin hataki kunielewa na ameahidi kubadilika lakini sioni hayo mabadiliko.

Nakumbuka tukiwa mwaka wa 2 wa mahusiano yetu aliwahi kuniaga anaenda kwa dada ake lakini alivyorudi home alikua kabadilika wakunijibu short mpaka nilipogundua alikua akichart na mwanaume mwingine, kiukweli niliumia sana na nilitaka tuachane ila nilimsamehe na kuahidi kubadilika na kweli niliona juhudi zake za kubadilika na penzi likazidi

Mwaka wa tatu sasa wa mahusiano yetu kwao wananijua na mimi kwetu anafahamika, tulibahatika kuwa na duka lakini halikukizi mahitaji yetu ndipo nilipomwambia mpenzi maisha sahv ni magum acha nitafute kazi na kweli Mungu alinisaidia na kupata kazi mkoani na ndipo niliamua kufunga lile duka na kukaa nae mkoani

Ila hapa ndipo alipokuja na wazo na kuniambia mpenzi sasa nataka kubeba mimba basi tulipima vipimo vya awali na kujua hana ujauzito wowote na nilimpatia ujauzito na safari ya ujauzito ikaanza rasmi

Hapa ndipo shida ilipoanzia nikichelewa kufika home basi itakua ni ugomvi siku nzima na kununa, tuligombana sana kiasi akaomba aende home akapunzike kidogo nilimpa ruhusa akaenda home

Alivyorudi maisha yakaendelea ila shida zikarudi tena kila binti wa kazini niliyeongea nae kwake ilikua tatizo nilimwelezea lakini hakutaka kunielewa alikesha kushinda na simu yangu na kufuta namba za wafanyakazi wenzangu wote wa kike nilimvumilia nikajua nimabadiliko ya ujauzito

Kuna siku alinikwaza alivyomtafuta mfanyakazi mwenzangu akijua labda ni mpenzi wangu na kumwambia maneno mabaya niliumia nakuona aibu gani hii nilimgombeza alikasirika na kuria sana nilimwomba msamaha akuelewa alimwambia dada ake na dada ake alivyonitafuta hakutaka story na mimi zaidi ya kunigombeza na maneno yasiyo na stara hata kidogo niliumia nikamfata mpenzi wangu nikamwelezea situation yote na jinsi dada ake akuniheshimu aliniomba msamaha na mimi nilimsamehe maisha yakaendelea ila alichoniambia anataka kuondoka home na anahisi simpendi tena na yeye anaona hanipendi nilimwambia ni hali ya ujauzito tu utakuwa sawa akaelewa na maisha yakaendelea

Shida kubwa inakuja hapa nilipata mwaliko kazini wa mama mtu mzima tu kwake na alitualika watatu nikamshilikisha mpenzi wangu ila alikataa nikamwambia haina shida

Sasa jambo hili halikufanikiwa maana mama alijipanga kwake na kuomba ruhusa hata kazini ili tufike kwake kumsalimia niliona sio vibaya na ntaonekana mtu wa ajabu nikaongozana na wenzangu tukaenda ila sikumwambia mpenzi wangu muda natoka sikutaka kumficha maana kama angejua badae angeumia zaidi nilimwambia nilienda kwenye ule ugeni

Alikasirika sana sikutegemea kama angebadilika hvyo alinitukana maneno mabaya ambayo ajawahi kuniambia na akakusanya vitu vyake na anataka kuondoka kwenda kwa dada ake na hataki kujuana na mimi tena wala nisimtafute yeye na mtoto tena, nashindwa kuelewa kama hili kosa ndo limepelekea haya yote na akiwa amebakiza mwezi kujifungua anataka kuniacha nashindwa kuelewa shida ni nini naombeni mawazo yenu.
 
Unaleta demokrasia kwenye mahusiano? Utakufa vibaya wewe.

Dada mtu shem wako anakugombeza na wewe ulivyo zoba zobinyo unaikubali hiyo hali, sikutukani ila we ni fala sana na hao washajua udhaifu wako watakuendesha mpaka upate presha na kisukari na uachwe hapo.

Be a man mkuu achana na u nice guy utakuua, punguza kumjali na kumshirikisha kila jambo maana inaonekana hata ukitaka kwenda kupupu unamwambia na akikukatalia akanuna unahairisha matokeo yake utajinyea bure.

Unakera sana, badilika wewe kwanza ndio yeye nae atabadilika vinginevyo utagombezwa hadi na vitukuu vya huyo dada yake.
 
Huyo binti ana wivu uliopitiliza na wivu ukizidi sana mara nyingi uleta hasara
la pili huyo binti malezi yake yanatia shaka pengine anadeka sana au anaona hata akikaa kwao bila mme anaridhika

sina ushauri, mapenzi ni ya wawili tu
 
Huyo binti ana wivu uliopitiliza na wivu ukizidi sana mara nyingi uleta hasara
la pili huyo binti malezi yake yanatia shaka pengine anadeka sana au anaona hata akikaa kwao bila mme anaridhika

sina ushauri, mapenzi ni ya wawili tu
Hilo ni kweli ndo walivyomlea hvyo mshua ake anampenda sana na kiukweli wana uwezo
 
Unaleta demokrasia kwenye mahusiano? Utakufa vibaya wewe.

Dada mtu shem wako anakugombeza na wewe ulivyo zoba zobinyo unaikubali hiyo hali, sikutukani ila we ni fala sana na hao washajua udhaifu wako watakuendesha mpaka upate presha na kisukari na uachwe hapo.

Be a man mkuu achana na u nice guy utakuua, punguza kumjali na kumshirikisha kila jambo maana inaonekana hata ukitaka kwenda kupupu unamwambia na akikukatalia akanuna unahairisha matokeo yake utajinyea bure.

Unakera sana, badilika wewe kwanza ndio yeye nae atabadilika vinginevyo utagombezwa hadi na vitukuu vya huyo dada yake.
Nashukuru kiongozi ntalifanyia kazi
 
Mm naona wew ndie MWenye matatizo.
Umekua dhaufu mpka unafokewa na shemeji si ufala huo.
Ukiendelea kua zoba utateseka sana watakuendesha kama gari bovu.
 
Miaka minne 4....mnakaa pamoja...
Hamjaoana....

Nadhani sasa mmechokana pumzishaneni mkimkumbukana mtarudiana
Yaan ushauri wako haujawah kuwa wa watu kupambania penzi lao,wew huwa nikushauri watu waachane tu

Ulishawah kupatwa na nini kwenye mapenz haya
 
Nina mwanamke kama huyo,tuna watoto wawili,ila napanga kuachana nae,nataka nimuachie kila kitu nimkimbie

Yaan simu yang hatak iite,na ikiita na kupokea na nikaongea kwa kifupi ni tatzo

Kuna wakat wananipigia watu wa heshima mfano mama,anaanza kuropoka wewe ni kuongea na malaya zako tu,mbaya zaidi haya masmart mic zake huwa zinanasa zaidi sauti iliyopo mbali

Huu huwa nauita wivu wa kijinga
 
Back
Top Bottom