Mapenzi Yamzingua Bibi wa Miaka 92

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
Bibi mwenye umri wa miaka 92 wa nchini Marekani ametiwa mbaroni kwa kumpiga risasi mwanaume jirani yake ambaye alikataa kumpa 'denda' bibi huyo ambaye alizidiwa na penzi kwa jirani yake ambaye siku zote alikuwa akimtolea nje bibi huyo.
Bibi Helen Staudinger mjane mwenye umri wa miaka 92 mkazi wa Florida nchini Marekani ametiwa mbaroni kwa kuishambulia kwa risasi nyumba ya jirani yake ambaye alikataa kumpa busu.

Helen aliwaambia polisi kuwa alienda kwa jirani yake mwenye umri wa miaka 53, Dwight Bettner, na kumuomba ampe angalau busu ili autulize moyo wake uliojaa cheche za mapenzi kwa jirani huyo.

Baada ya Dwight kukataa kumbusu Helen, Helen alisema kuwa hataondoka mlangoni kwake hadi pale Dwight atakapokubali kumbusu.

Helen aliwaambia polisi kuwa mzozo mkubwa ulizuka kati yake na Dwight na kupelekea bibi huyo arudi nyumbani kwake kuchukua bunduki na kuanza kuishambulia kwa risasi nyumba ya Dwight.

Mojawapo ya risasi ilipenya kwenye dirisha la chumba cha Dwight na kusababisha Dwight kujeruhiwa na vioo va dirisha hilo. Risasi zingine tatu zilipigwa kwenye kuta za nyumba ya Dwight.

Dwight aliliambia gazeti la Star-Banner kuwa kwa miezi sita tangu alipohamia nyumba ya jirani na bibi Helen, amekuwa akisumbuliwa na bibi huyo anayemtaka kimapenzi.

"Nilimwambia kuwa nina uhusiano na mwanamke mwingine lakini alikuwa akisisitiza lazima niwe mpenzi wake", alisema Dwight.

Dwight aliongeza kuwa bibi Helen aliwahi kumshambulia mwanamke mmoja ambaye alifikiria alikuwa ndiye mpenzi wa Dwight.

Bibi Helen amefunguliwa mashtaka ya kufanya shambulizi la silaha kwenye makazi ya watu.
 
Kha, kibibi kinalazimisha penzi!

Kaaaz kwelikweli.
 
Kweli mapenzi ni upofu! Kibibi hadi kimekamata bunduki...kha!
 
Hii sasa ni kali kwa mfano huyo jamaa angemkubalia huyo bibi cha kujiuliza ni je mchakamchaka wa huyo kijana angeuweza ?
 
mbona huyo bibi bado nazi kabisa!! mpeni huyo bibi namba zangu antafute 0713 800800.
 
Hii sasa ni kali kwa mfano huyo jamaa angemkubalia huyo bibi cha kujiuliza ni je mchakamchaka wa huyo kijana angeuweza ?

Hapa ni kinyume chake, mchakamchaka wa Bi Helen angeuweza huyu kijana?
 
Huyu ajuza ana pepo la ngono au akili zake zimepunguka..kumpeleka mahakamani ni kupoteza hela ya walipa kodi.
 
Mi naona angekubali tu, ila kwa conditions. Ki muandikie urithi wa mali zake zote kisheria halafu afanye hicho anacholazimishwa na bibi huyo kufanya.
 
Dah!!ya wezekana bibi ana mfadhaiko na mahitaji yake ya kimwili bado yapo juu so kama familia ingeangalia namna ya kutatua tatizolake hata kwa kumkodia mtu ili awe anampelekea faru au niaje wakuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…