Tatizo kubwa la wanawake huwa mnakabidhi mioyo yenu pasipo kusoma mchezo
Mi naona bora afe tu
Hahaha...nataka nianze kukusanya rambirambi!!hahahaha Lizzy huishi vituko wewe....hahahah, kufa hafi cha moto atakiona.
Mmmh!!Wakati uswazi kwenu kila mtu ni Kanumba Kanumba ...Hiyo fani ya maigizo mimi imenipitia kushoto kabisa
Hahaha...nataka nianze kukusanya rambirambi!!
Roho mbaya gani?!Lizzy.......hiyo roho mbaya umeipata wapi???
Ndugu zangu,naombeni ushauri,kweli nakiri nimekosea. Suala langu lipo hivi,mimi nilizaa na mwanamke mmoja japo sikumpenda kwani nilijipa moyo nampenda kumbe ilikuwa si kweli kwani nilikutana naye nikiwa na wawazo mengi kutokana na kuachana na mpenzi wangu wa kabla yake,niliyezaa naye huyu tuna uhusiano wa mwaka na zaidi hivi,akiwa mjamzito nikapata mwanamke niliyempenda kwa dhati,kutokana na ujana nikamvisha pete ya uchumba, naye nipo naye kwenye uhusiano yapata miezi tisa sasa,wote wanajuana na hakuna anayekubali kuachana nami,mwenye mtoto hakubali na mwenye pete anasema hawezi kubaki na pete,ndugu zake na jamaa washajua namuoa. Wote wanataka kutumia nguvu hadi za jadi nisimwache hata mmoja na najua ipo siku mambo yatakuwa makubwa sana na wote wanipenda kwa dhati japo mimi toka moyoni nampenda niliyemvisha pete ila mara zote namfikiria mwanangu ataishije bila baba? naombeni ushauri,mimi ni mkristo siwezi kuoa wake wawili,nipo tayari kurudi kwa mwenye mtoto ili niilee familia yangu ila mwenye pete naye hakubali,nifanyeje ndugu zangu?
Hakuna mtu mwenye uwezo wa kukulazimisha kukaa nae....nipo tayari kurudi kwa mwenye mtoto ili niilee familia yangu ila mwenye pete naye hakubali,nifanyeje ndugu zangu?
Dah! Una wakati mgumu kweli aisee, washirikishe ndugu zako unaowaamini uweze kutatua kesi hiyo.....nashukuru Shantel,sasa kwenye nguvu za jadi ndio sijui itakuwaaje. Mimi siamini mambo hayo ila wao wanaamini na wanataka wadhuriane wao kwa wao,nimejaribu kuwasihi wasifanye hivyo ila kila mmoja anaapa kumwendea mwenzie kwa waganga kama nikionesha upendeleo kwa yoyote. Kati yetu watatu kila mtu anaishi kwake ila kila mmoja kati yao wawili kaweka wapambe wa kutoa taarifa kama nimekwenda nyumbani kwa mmojawapo na tifu linafumuka hapo.
Siku zote naamini ndoa itadumu tu kama chanzo chake kilikuwa ni upendo na si huruma. Ila hao wanawake wote wawili ni characters. Yani wanakugombea. Eti wanasema watarogana. aaah. Ungekuwa na moyo wa chuma ningekushauri uwapige chini wote wawili utaoaje wanga bwana! Utalishwa mauchafu wewe mpaka uwe taahira! Yeyote utaye muoa lazima akupe limbwata utulie maana kama washahapa kurogana unadhani watarogana wao tu wewe wakuache?
Tafuta wife material bwana hachana na hao wadada hawakufai.
Jamaa ndio ameishakiri kua kakosea, anachoomba mumsaidie afanye nini?? Au amuone Pinda akapate ushauri wa maamuzi Magumu???unajua bro ,mm sijapenda ulivyo fanya sio. kama nitakukera samahani, na madhali umeweka bayana kutaka ushauri subir nikueleze kweli, ,, why? ulimpa mimba uyo dada na hukua ukimpenda? nini malengo yako kwake? umesha haribu maisha yake ,, na hukua na love juu yake hata kidogo,unajua man hapa ndipo munapo kosea.. hiyo ni parnishment na ni saiz yko munatakiwa mujifunze na makosa,, dada wa watu alikusabilia bcz alikua amini na alikupenda,kumbe ww unampenda mwengine,, ata kua mm siwez kukusamehe daima,, samahani wanajamii lakin nahis kama ,, niliofanyiwa mm hivi ,, au mtu afikirie awe mwanamke kama mm afanyiwe hivyo nn ata hisi???
In maana bado unawakula wote?nashukuru Shantel,sasa kwenye nguvu za jadi ndio sijui itakuwaaje. Mimi siamini mambo hayo ila wao wanaamini na wanataka wadhuriane wao kwa wao,nimejaribu kuwasihi wasifanye hivyo ila kila mmoja anaapa kumwendea mwenzie kwa waganga kama nikionesha upendeleo kwa yoyote. Kati yetu watatu kila mtu anaishi kwake ila kila mmoja kati yao wawili kaweka wapambe wa kutoa taarifa kama nimekwenda nyumbani kwa mmojawapo na tifu linafumuka hapo.