Mapenzi yetu yana miaka saba sasa............

richard mlwande

New Member
Joined
Jan 10, 2013
Posts
3
Reaction score
0
Jamani mimi nina mchumba wangu mwaka wa 7 sasa,kwetu hajulikani rasmi na nina mpango siku moja nikamtambulishe,lakini inavyoonesha home hawamkubali sana na mimi mwenyewe wazo la kumuoa nahisi linafifia.Kumuacha naogopa coz kuna siku alinambia siku nikimuacha ANAJIUA so sielewi jamani NAOMBENI MAWAZO YENU NIFANYE NINI???
 
Mapenzi hayachagui.
Kama unampenda kweli utamjali.
 
Kwa nini upendo unapungua hadi unafikiria kumuacha?
 
kama unampenda usimuache kwenu hawamkubali wao ndo watakaa nayee wacha uhuni aiseee
 
Una kazi kubwa sana ya kuamua juu ya maisha yako,kumbuka wazazi na ndugu hawana haki ya kukuchagulia mke bali ni wewe mwenyewe hivyo kama hawamkubali unatakiwa utambue kuwa ni wewe ndiye unayetakiwa kuwafanya ndugu zako wamkubali.
Upendo unaopungua kuna sababu zake hivyo ingefaa uziweke sababu za upendo wako kupungua kwake na tunaweza kukushauri cha kufanya.
Usiogope maneno ya kujiua na vitisho vya mapenzi,vilikuwepo,vipo na vitaendelea kuwepo cha msingi simamia unachoamini ila kumbuka kuwa usipende kumfanyia mwenzako baya ambalo wewe hupendi kufanyiwa.
 
Heri nusu shari kuliko shari kamili, heri umuache tu kuliko umuoe ukamtese. Ataumia sanaa mwanzo ila atazoea!
 
Kiasi umchoke na utafutie sababu miaka saba sio kidogo hata angekua mkeo halali basi mngeshaanza kufanana sura,
Umemuahidi ndoa kwani? au hafai kua mke lakini kua hawara alifaa miaka7? kua mungwana kama ushamaliza matumizi
yako kwake basi muache tuu mungu atampa mwenye kheir na yeye...
 

Hujasema umri wenu, inawezekana bado ni watoto.
Mimi wakwangu alikuwa girlfriend tu kwa miaka minne akawakama sehemu ya maisha yangu alikuwa akiishi kwao na mimi kwangu ilikuwa sewezi kulala bila kusikia angalau sauti yake nilikuwa siwezi kula mpaka nijue yeye keshakula, tumeoana sasa nimiaka 12 tuna binti wa 11 yrs maisha raha mustarehe. Mwanzo wazazi wangu hawakumpenda sana sana mama( kabla ya kuoa) lakini sasa wanapendana sana wamekuwa zaidi ya mtu na mkwe wake na kuwa ni mtu na mama yake.
 

Acha kuzunguka mbuyu mkuu.. Wewe miaka yote 7 ulikuwa unasubiri nini? Umeshakidhi haja zako weee sasa kwa kuwa umeona na uzee umeanza kumpata unasingizia eti nyumbani hawamkubali. Kwanza huenda umeshavutiwa na dogodogo sehemu na unatafuta sababu tu ya kumpiga chini. Mi nakuombea tu ukimwacha uangukie mikononi mwa wale wanaoitwa pasua vichwa ili nawewe ujesikia maumivu yake.
 
Miaka 7 hata ndani ya ndoa penzi haliwi kama mwanzo. Oa mke mwingine baada ya miaka 3 penzi litafifia; na kwakuwa ulimuahidi, you will surely know no peace. She will be happily married kungine lkn kwa kuwa wewe ni mkosaji, utapata kichomi na utamkumbuka mpenzi wako maisha.
 
kwa mapenzi ya ndoa 7 yrs tayari mazoea yameshanza kiasi kwamba penzi linakuwa sio kama la kwanza na zisipochukuliwa hatua madhubuti nda huweza kuingiliwa na mgeni akaketi chumban kwa baba na mama.

to me ingawa uko naye but bado akili yako haijakuwa kiasi cha kuwa mtu mzima bado unaakili za kushkiwa and to me kuliko niolewe na mtu wa akili za kushkiwa home ni bora iyo ndoa ikanipitia mbali.
 

Kaka akipita humu akaona jina lako tu, ujue anaenda kubeba kamba!!
 
Mhh miaka saba yote na bado hajulikani kwenu ni kwa nini? ama ulikuwa unawasikilizia hao ndugu zako watasema nini kumhusu? Sasa kwa kipindi chote hicho kama ulijua kwenu hawamkubali na wewe ukakubaliana na wao kutomwoa kwa nini usingemwacha mapema sasa angekuwa ashasahau maumivu na kupata anayempenda kweli? Haya fanya maamuzi hima na kama humtaki mwambie mapema na lakini kumbuka what goes around.....
 

Uko sahihi sana Kaunga! hiyo ni dhambi ya Uzanzibari na Uzanzibara huwa haiishi itaendelea kukutafuna tuu
 
Hell no!! yaani 7 years wala hujamtambulisha?, are you serious?...eish!!
Hivi naye huyo mwanadada miaka yote 7 wala hajatambulishwa bado tu anasubiria dodo chini ya mwarobaini...!!!
Mapenzi ya dotcom bhanaaaa...ptuuuu!!!
 
hata hueleweki, unachosha
 

Kwa nini unataka kumuacha???Tabia mbaya au umemchoka tu
 
mh sijapenda kabisa tabia yako heee baada ya kumtumia miaka 7 yote hiyo leo unataka kumuacha kirahic hivyo? shindwa kabisa!!! kwanza tuambie hapa kwann upendo unafifia acha kufumbafumba ooh home hawampendi kwan ndo watakaa nae wewe hujatulia tu!! na hiyo dhambi lazima itakutafuna!! kumbuka malipo ni hapahapa duniani! ovyoooo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…