Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Mapigano makali yaliyodumu kwa muda wa masaa 48 huko kaskazini Magharibi mwa Syria yamewaua watu 96, kulingana na shirika linalofuatilia haki za binadamu la nchini humo.
Shirika hilo limesema vikosi vya serikali vikishirikiana na ndege za kivita za Urusi, vilikabiliana vikali na makundi ya waasi kusini mashariki mwa mji wa Idlib mwishoni mwa juma. Shirika hilo lenye makao yake makuu Uingereza limeongeza kwamba hayo yalikuwa mauaji makubwa tangu makubaliano ya usitishaji mapigano yaliyoandaliwa na Urusi, yalipoanza kutumika mwishoni mwa mwezi Agosti.
Makabaliano hayo na mashambulizi ya kutokea angani yamechochea wimbi jipya la watu kukosa makaazi katika eneo la Idlib kuelekea ulipo mpaka wa Syria na Uturuki. Idlib ni jimbo linalodhibitiwa kiasi kikubwa na upinzani karibu na mpaka na Uturuki.