Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Kubadilisha Chama au Wanasiasa si tija ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini Tanzania.
Kujipanga upya kupitia Vyama au kutafuta Wanasiasa wapya si njia bora ya kuleta mabadiliko nchini Tanzania.
Kupigia kelele Ufisadi na hata kuiombea CCM ianguke na kumeguka, hakutaleta mabadiliko ya madendeleo Tanzania.
Tunahitaji Mapinduzi 2010!
Tunahitaji mapinduzi ya fikra, utashi, nia na nguvu binafsi ili tulete mabadiliko ya kweli Tanzania.
Tunapaswa kujijenga kama jamii mpya iliyo huru, yenye kujithamini na kujiamini ili kufanikisha mapinduzi haya.
Mapinduzi anayoyatamka Rev. Kishoka, si kukatana mapanga, Jeshi au kikundi kuamua kupindua Serikali! La hasha! Bali ni mapinduzi ndani ya mioyo yetu.
Mapinduzi ya kweli yataanza na Mtanzania kuamua kuachana na Utegemezi na kuanza kujituma, kujiendeleza na Kujitegemea.
Ndiyo, ni kweli tumeimba nyimbo za kujitegemea kwa miaka mingi, lakini hatukufanya busara na kutafuta njia nyepesi na rahisi kufanikisha azma hiyo ya kuwa Taifa linalojitegemea.
Mapinduzi ya kweli ya kuleta maendeleo na kujenga Taifa linalojitegemea yatatokana Watanzania kwa umoja kujenga mfumo bora wa kiuchumi ambao si mgumu kama ule wa Adam Smith au John Keynes, bali ni mfumo ambao utamfundisha Mtanzania kuzalisha si cha kujihimu kwa siku mbili tuu, bali ni kuzalisha kwa wingi, kutumia maarifa bora ya Sayansi, Teknolojia na Biashara ambayo si magumu kama Aljebra bali ni mepesi na rahisi kama hesabu za kutoa, kuongeza, kugawanya na kuzidisha.
Kosa letu Watanzania na hasa sisi Wasomi ni kukimbilia kulijenga Taifa letu kwa mfumo wa Uchumi unaotumia nyenzo za hali ya juu kuliko uwezo wa kawaida wa fikra au utashi kwa Jamii yetu.
Nikiangalia mkulima, ikiwa atapigwa msasa na kuonyeshwa kuwa akilima heka 20 badala ya heka 2 na kuonyeshwa faida za kulima kwake heka hizo 20 ikiwa ni pamoja na kulima kwa ustadi, kutumia mbolea, umwagiliaji na kujijengea maghala imara ili kuhifadhi mazao yake, basi ni wazi mkulima huyu akiona kipato chake na uwezo wake wa kuzalisha mali unaongezeka, hiyo itakuwa ni kichocheo na motisha wa yeye kuongeza nguvu zake na kujiongezea kipato.
Lakini maendeleo haya yatapatikana ikiwa Mkuilma huyu atakuwa na Uhuru wa kuuza mazao yake bila kunyanyaswa na Serikali ya kijiji, mtaa, Ushirika au Chama cha Kisiasa.
Hali kadhalika yule Mangi wa pale Gerezani na Machinga mtaa wa Kongo, akifundishwa mbinu bora za kufanya biashara yake kwa kutumia nyenzo nyepesi na kujiwekea nidhamu ya kazi na hata kufundishwa kujiwekea hifadhi ya mapato yake Benki, basi ni wazi Mangi na Machinga atapiga hatua ya kimaendeleo.
Pamoja na kuwa Dunia ya leo iko kwenye Teknolojia za Nano, GMO, Digital na nyinginezo ambazo zinaongeza uzalishaji marudufu, ukweli ni kuwa mzalishaji wa Tanzania hawezi kingia katika ushindani wa kimataifa huku akiwa hana umeme, maji au mfumo mzuri wa mawasiliano na ushukuzi ambao unaweza kumfanya ajijenge na kujitosheleza.
Mkulima niliyemtolea mfano hapo juu, si lazima asafirishe mazao yake Dar Es Salaam, bali anaweza kuuza jirani kabisa na anapoishi au kuwa ndani ya mfumo bora wa kuuza mazao yake ambapo hatatumia gharama nyingi kujipatia kipato cha kufidia jasho lake.
Kila kitu kinahitaji utashi, nia na nidhamu ya hali ya juu.
Mtanzania atakapo amka na kuyakubali mapinduzi ya fikra ya kuachana na utegemezi, hiyo itakuwa hatua kubwa ya kwanza na muhimu mno kwa Taifa letu katika kuleta mabadiliko ya kweli, iwe ni kisiasa, kiuchumi au jamii.
Kinachotushinda kuleta mabadiliko Tanzania si rasilimali, Vyama vya siasa, Katiba, Sheria, Sera, Ilani au Wanasiasa.
Ni mizizi iliyokomaa ya kutegemea misaada!
Ndiyo, ni tabia chafu ya kuwa ombaomba, kutegemea kubebwa, kusaidiwa, kupewa, kuhongwa, takrima, baksishi, kidogodogo hata ruzuku.
Nimetoa mfano hapo juu wa Mkulima, Mchaga na Machinga, na kutamka wazi kuwa inabidi tawe nyenzo nyepesi na kuwafundisha ustadi na umakini katika uzalishaji mali wao na hata kuwafundisha kuwa na mipango bora.
Hilo ni muhimu ili Mkulima, Mchaga na Machinga wawe huru na kuachana na kutegemea au kuishi kwa kutegemea ndani ya mfumo wa kutegemea.
Waswahili husema "mtegemea cha ndugu, hufa masikini", sisi kama Tabaka la Wasomi, Wanasiasa na tulioona mengi na kujua mengi, tumeshindwa kumkomboa Mtanzania mwenzetu kwa kumfanya yeye ni mjima, mjinga na kusimika mizizi ya unyonge kwake, hivyo kumfanya yeye "mtegemea cha ndugu" tukimburuza kila kona na kila mtaa na kumtaka afanye tunachotaka na tunachomuamuru.
Hapa ndipo tulipopotea na tutaendelea kujidanganya kama tutadai kuwa eti tubadilishe kwanza chama, katiba au kuwa na hata wagombea huru.
Tunachohitaji ni kubadilisha fikra zetu, kama wasomi. Tutumie ujuzi wetu na upeo wetu kurahisisha uzalishaji mali na kuimarisha safari ya Taifa letu na watu wake kwenda katika mfumo wa kujitegemea.
Ikiwa kama tunashindwa kuishi kama mfano kwa Mtanzania mwenzetu aweze kutuiga kwa yale yaliyo chanya, ni vipi tutegemee yeye ataamka na kuwa na maendeleo?
Ikiwa Bwana Shamba, Mifugo, Hakimu, Polisi, Muuguzi na wengine, hawaishi maisha na kufanya mambo yanayoendana na elimu zao, tutategemeaje kumfundisha Mzaramo kuwa akikata nyasi na kuondoa uchafu kando ya nyumba atapunguza kwa kiwango kikubwa nafasi ya yeye kupata malaria, huku sisi nyumba zetu zimejaa vichaka na madimbwi ya maji machafu?
Kule kijijini ikiwa Bwana Shamba ni mhubiri bila vitendo na matunda ya kazi yake kwa manufaa yake yakaonekana kwa Wanakijiji wenzake, tutawezaje basi kudai kuwa Wanakijiji hawaambiliki?
Hivyo basi ni wajibu wetu kubadilisha fikra zetu, za majirani zetu na familia zetu ziwe ni fikra endelevu kama tunataka mapinduzi ya kweli.
Jukumu hili ni la kila mmoja wetu na si kusubiri kumsikia Kikwete, Slaa, Maalim Sefu, Bakwata, TEC, Mwanakijiji au Mchungaji waendelee kuyasema haya!
Ndio kila mtu atakuwa na mvuto wake, na njia yake kuifundisha jamii. Lakini hakutakuwa na mwamko au usahihi kama elimu ya kuleta mapinduzi ya fikra na mwamko mpya wa maendeleo ili kujenga Taifa linalojitegemea kutakuja na masharti ya kijinga, kama kujiunga na chama, kubadili dini, kuletewa huduma kwa utiifu wa Chama, Mtu, Dini au lolote lile!
Tunapojianda kwa mwaka 2010, basi tujiandae kuleta mapinduzi ya kweli na si kudanganyana! Nasema mwaka 2010 kwa kuwa kila mmoja wetu keshaamua kuwa kazi ya kuleta mabadiliko ni 2010, hivyo nikisema tuanze sasa, sidhani kama utanisikia au kunielewa.
Wakati ukitafakari mgombea, sera na chama, ambacho unadhani kitaleta mabadiliko na kuimarisha vita dhidi ya Unyonge, Umasikini, Maradhi na Dhuluma, usimsahau Mtanzania mwenzako ambaye kura yake unaitumia kwa manufaa yako binafsi huku yeye akiambulia ahadi nyingi, fulana na ubwabwa na shukrani za kinafiki!
Mwaka 2010 uwe ni mwaka wa Mapinduzi ya kweli kutuletea maendeleo na kutukomboa katika unyonge na utegemezi.
Chaguo ni lako, tumia Uhuru na akili zako kwa umakini!