Siku zote inaaminika kuwa mteja ni mfalme. Je ni kweli? Wakati mwingine mteja anaamua kwenda kutafuta huduma sehemu nyingine. Yote ni kwasababu amekutana na maswaibu mengi pindi alipohitaji kupata huduma. Baadhi ya watoa huduma hawana lugha nzuri kwa wateja.
Siku moja nilimshuhudia mama mmoja ambaye alijifungua sehemu ya mapokezi katika hospitali fulani. Yote ilisababishwa na mtoa huduma kushindwa kumhudumia mama huyo kwa haraka. Mbaya zaidi mtoa huduma alitoa maneno machafu kutokana na mama huyo kujifungua mahali pa mapokezi kiasi kwamba majengo ya hospital kujawa na hasira. Kama majengo yangekuwa yanapumzi basi mtoa huduma huyo angepata kipondo ambacho kingemfunza. Masikini! Mama huyo alifariki papohapo kwani hakupata huduma stahiki.
Wafanyakazi wengi hawatambui wajibu wao. Upande mwingine wanaweza wakawa wanajua wajibu wao lakini hawafanyi Kama kazi inavyowataka wafanye. Inakera Sana! Kwenda mahali kupata huduma lakini usipatiwe ama upatiwe huduma isiyo Bora.
Si ofisi za serikali wala ofisi binafsi, kasumba ya kushindwa kutoa huduma nzuri kwa wateja bado ipo na inaendelea kutafuna watu wengi. Pia wafanyabiashara na wajasiriamali, bidhaa Ni zao lakini wanashindwa kuwa wakarimu kwa wateja. Kuna siku nilishuhudua muuza nyanya alivyomjibu mteja,"ukitaka nyanya chukua, hutaki tambaa!". Hakika mabadiliko chanya yanahitajika kwa watoa huduma.
Zipo faida nyingi za kutoa huduma kwa wateja,Kama vile; kumfanya mteja kurudi tena kupata huduma yako,kuongezeka kwa uzalishaji,kukua kwa taasisi ,kuimarisha ustawi na maendeleo ya taasisi nk.
Iwapo mtoa huduma atashindwa kutoa huduma nzuri kwa wateja, atasababisha kushuka kwa uchumi katika taasisi kwasababu wateja watashindwa kurudi tena na kupata huduma. Taasisi au Biashara haiwezi kuwa na mafanikio kama hakuna wateja. Siku zote mteja Ni mfalme. Japo kuwa kuna wateja ambao huanza kuchochea ugomvi, lakini mtoa huduma anatakiwa kuwa mpole, kujishusha na kumhudumia mteja kwa upendo pasipo kuweka hasira dhidi ya mteja.
Sifa za mtoa huduma ni pamoja na;kutumia lugha nzuri na yenye busara kwa wateja,kuwa na tabasamu kwa wateja,kumkaribisha na kumsikiliza mteja kwa upendo na na hatimaye kumpatia huduma inayotakiwa kwa ubora.
Katika jamii zetu, watoa huduma iliyo Bora wanaweza kuwa ni wawili kati ya elfu moja. Wengi wao husababisha kilio kwa wateja. Ipo kasumba moja mitaani… utasikia mwanamke anasema "sisi wanawake hatupendani, nilivyoenda kupata huduma nimekikuta hicho kidada kinajishaua,kimenijibu vibaya wala Sina hamu! Yaani bora ningemkuta mwanaume angenihudumia vizuri." Kasumba hii imeendelea kutafuna watu wengi. Kuna mtu mwingine, Kama Ni mwanamke anapoenda kupata huduma sehemu,halafu akamkuta mwanamke mwenzake huwa anahairisha na kuamua kurudi nyumbani au kutafuta mahali pengine ambapo yupo mtoa huduma mwanaume.
Mpaka lini hali hii itaendelea? Wateja watalia mpaka lini? Ipo tija ya kuleta mabadiliko katika sehemu za kutolea huduma. Mtoa huduma na mteja ni Kama viungo vya mwili. Kama Macho hayajatazama,mkono hauwezi kuchukua kitu.
Tumbo haliwezi kupokea chakula Kama mdomo haujafanya kazi ya kupokea na kuruhusu meno yatafune. Hivyo basi, Mtoa huduma bila mteja hakuna huduma. Na mteja bila mtoa huduma hapati mahitaji yake. Wote wanategemeana.
Nazishauri taasisi za serikali na binafsi kuhakikisha sheria na taratibu zinafuatwa kikamilifu na wafanyakazi au watoa huduma,kufanya tathmini dhidi ya utendaji kazi kwa watoa huduma na pia kuweka kifaa cha kiteknolojia kama vile CCTV camera ambacho kitasaidia kuonyesha uendeshaji wa huduma zote. Na endapo itagundulika wapo watoa huduma ambao hawawajibiki, wachukuliwe hatua.
Kuna ofisi zingine ukienda, unawakuta watoa huduma wamekaa kikundi wanapiga stori zao huku mteja akisubiri kupata huduma. Mwisho wa siku mteja haudumiwi anaambiwa arudi siku ya pili kupata huduma. Na hiyo siku akienda, Mambo ni yaleyale.
(Chanzo Cha picha;hapa kwetu.blogsports.com)
Pia, wakati mwingine mtu hapati huduma kwa wakati kwasababu ya mlolongo mrefu. Mfano, mteja anahitaji kupata huduma yake ndani ya siku moja, ila kwakuwa mlolongo wa kuipata hiyo huduma umekuwa mrefu, inapelekea kutopata huduma kwa wakati.
Huduma Bora hupatikana iwapo kuna uongozi na usimamizi Bora,sera na miongozo ya kazi,uwajibikaji na kuajiri walio na sifa zinazohitajika.
Mabadiliko chanya yafanyike katika taasisi za serikali na taasisi binafsi na ofisi ndogondogo za kutolea huduma. Kila mtoa huduma atambue nafasi yake na awajibike vyema. Ile nidhamu na unyenyekevu aliokuwa nao wakati anatafuta kazi.. vyote viendelezwe hata anapopata kazi.
Mteja akifurahi ni mafanikio ya taasisi au Biashara. Ukigombana na mteja,utapoteza mengi. Vaa vazi la uwajibikaji katika nafasi yoyote uliyonayo.uwe mwalimu,uwe daktari,katibu muhtasi, mfanyabiashara na kadhalika, unalo jukumu la kumjali na kumuhudumia vizuri mteja.
Mteja pia anapaswa kuzingatia taratibu zilizowekwa sehemu ya kutolea huduma. Wapo baadhi ya wateja ambao ni wasumbufu na hupendelea kuvunja sheria na taratibu. Mfano;maeneo tofauti tofauti ya kutolea huduma, mteja anawakuta wateja wengine wapo kwenye foleni lakini kwasababu ana urafiki na mtoa huduma,anaamua kupitiliza katika chumba Cha kutolea huduma pasipo kujali kundi alilolikuta.
Mteja unayo sababu ya kuheshimu taratibu za kazi ili kumuwezesha mtoa huduma kutoa huduma iliyo Bora. Pia, Kama ambavyo mtoa huduma anatakiwa kusimama katika nafasi yake ya utoaji huduma ndivyo mteja unatakiwa kufuata sheria na taratibu za haki ulizozikuta.Mfano, umewakuta wengine kwenye foleni ya kupata huduma, unatakiwa nawe upange foleni hiyo bila kumuumiza aliyewahi.
Mtoa huduma usiweke upendeleo kwasababu una uhusuano na mteja ambaye amechelewa, ukamuhudumua yeye ukaacha kuwahudumia waliowahi.
Mwisho,Kila mmoja anatakiwa kuwajibika katika nafasi yake. Ikiwa Ni kiongozi,unatakiwa kuwajibika katika uongozi wako, ikiwa Ni mwajiriwa au mtoa huduma simama katika nafasi yako. Mteja heshimu taratibu za kazi. Kila mtu akiwajibika ipasavyo itakuwa na manufaa katika nyanja zote za maisha, hususani katika maendeleo.

Upvote
0