Yussufhaji
Member
- Sep 9, 2018
- 35
- 28
Hadithi ya Mwanamke wa Yoruba Ambaye Aliongoza Mapinduzi Mnamo 1844 Ili Kuweka Watumwa huru Cuba.
Miaka ya 1800, Amerika na Ulaya, ni enzi ya shauku na yenye shughuli nyingi, ambayo ilijazwa na upinzani bora na uasi kutoka kwa wanaume na wanawake weusi kote ulimwenguni. Wakati huo katika historia, utumwa ulikuwa umekomeshwa lakini ulikuwa bado unafanywa katika sehemu nyingi za Amerika na Ulaya.
Wanaume na wanawake weusi, kizazi cha Waafrika waliochukuliwa utumwani, na watumwa wapya walikuwa hodari katika hitaji lao la kudai uhuru kutokana na manyanyaso makubwa kwenye mashamba huko Karibiani. Karibiani na Amerika ndio ambapo Waafrika waliteseka sana mikononi mwa mabwana wa watumwa na waangalizi wa mashamba.
Lakini haijalishi jinsi mabwana wa kizungu walivojaribu kuvunja ari ya watu weusi; Ari nyeusi yenye nguvu ikapigania. Na kila wakati kulikuwa na uasi, iliwashtua na kuwakumbusha mabwan'nyenye wa kizungu kwamba "roho ya Waafrika ilikuwa ngumu kama mgongo wa mti wa Iroko wa miaka elfu."
Kadiri miaka ilivyopita, Waafrika zaidi na zaidi walianza kuasi. Ingawa viongozi wao walikamatwa na kuuawa katika visa vingine, kwa ujumla, watumwa wa kiafrika walikuwa wakiamka kwa nguvu. Ilikuwa katika mahitaji hayo yasiyokamilika ya uhuru ambayo hadithi na mafanikio ya Carlota Lucumi alizaliwa.
Mnano 1843 Carlota alikuwa mtumwa na alikuwa akifanya kazi na kutumwa katika shamba la sukari huko Mantazas, Cuba, iitwayo Triunvirato. Wakati huo, cheo chake kiliongezeka kati ya Waafrika waliotumwa, na kwa hivyo alikuwa na ushawishi katika jamii ya watumwa. Kwa hivyo, kwa miezi, yeye na watumwa wengine watano walipanga kuasi dhidi ya mabwana zao.
Wenzake waliitwa Firmina (mwanamke), Filipe Lucumi, Eduardo, Narciso, na Manuel Ganga. Walianzisha uasi tarehe 5 Novemba 1843, ambapo walichoma moto nyumba nyingi na mashamba mengi pamoja na nyumba ambayo ilitumika kuwaadhibu watumwa. Waliwashambulia Meya na Julian Luis Alfonso, ambaye alikuwa mmiliki wa mashamba hayo.
Hadithi ya ushujaa na uasi wa Carlota ulienea kama moto wa porini katika Cuba. Na kusababisha kwa kuenea kwa uasi katika mashamba 5 zaidi, watumwa wao waliamka na kuwauwa ma mwinyi wa Kizungu, Njaa ilio watapakaa na kiu ya uhuru ndio iliwatia nguvu watu weusi.
Carlota alikuwa mkali sana katika vita hiyo ili kusherehekea mafanikio ya mapinduzi yake kwa kumpiga binti wa mwangalizi wa mashamba na machete yake. Binti huyo aliitwa María de Regla.
Mageuzi yalizidi kuendelea, na yeye alitekwa na askari wa kizungu na kuteswa. Wakamfunga mwili wake kwa farasi na wakawalazimisha kumvuta hadi akafa. Wafuasi wake walipopata mwili wake asubuhi ya Novemba 6, 1943, kwenye eneo la mali ya Triunvirato, walikasirika na kupanda hasira, walishambulia mali zaidi na kuwauwa wazungu wengi. Hata hivyo uasi huu ulifikia ukomo kutokana na ubora wa silaha walizokuwa nazo askari wa kizungu.
Uasi huu ulimalizika baada ya kifo cha Carlota, lakini urithi wake uliendelea na ndio sababu kubwa ya mapambano ya uhuru ya Cuba. Uasi wake ulileta mshtuko mkubwa wa mioyo kwa jamii ya wazungu huko Cuba.
Mpaka leo, Carlota ni mtu muhimu katika historia ya Cuba, kwa jukumu lake katika kuongoza moja ya mapinduzi makubwa wakati wa utumwa.
Alitekwa nyara akiwa na miaka 10 kutoka Ufalme wa Benin ambapo alizaliwa na kupelekwa utumwani. Mtu angetegemea kwamba hali kali za utumwa zingekuwa zimevunja Afya ya msichana wa miaka 10, lakini haikufanya hivyo. Kuanzia umri huo mdogo, alitaka uhuru. Na yeye alikua mpiganaji mkali na mkombozi.
Jina lake la mwisho Lucumi limepatikana kutoka kabila lake, watu wa Lucumi, ambao ni Waafrika-Wabrazil waliibuka kutoka Yoruba ya Nigeria ya leo na Jamhuri ya Benin. Kabila lao liliogopwa sana huko Cuba, kama tu Maroons. Walijulikana kwa kusababisha uasi na kuanzisha makazi yao wenyewe.
Makala hii imeandaliwa na Liberty writers Africa kwa lugha ya kiingereza Septemba 4, 2019 na kufasiriwa kwa lugha ya kiswahili na Yussuf Hajj Khatib Tarehe 16, Febuari 2020 kwa lengo la kuamsha hamasa kwa wanawake wa Kiafrika.
Sent using Jamii Forums mobile app