Mapinduzi ya Kiuchumi ya England na dhana nzima ya maendeleo ya Zanzibar

Mapinduzi ya Kiuchumi ya England na dhana nzima ya maendeleo ya Zanzibar

Tuagize

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2021
Posts
244
Reaction score
585
Na:Abdull Najad Faiq

Tunapoizungumzia nchi ya England kijografia ni taifa la kisiwa lililozungukwa na bahari pamoja na mito mingi ama sehem kubwa ila mbali na aina hii yake ya geographia haikua kikwazo kwa England bali ilipelekea kuibuka kiuchumi na kuwa nchi ya kwanza duniani kwa maendeleo ya kiviwanda na pia kichocheo cha uchumi wake iliyonao hadi leo hii tunavyo iona.

England ilianza kupata maendeleo ya kiviwanda na kiuchumi kuanzia mwaka 1750s-1880s,zipo sababu zilizopelekea taifa la England kupiga hatua kubwa kiviwanda na kiuchumi ambazo zinafanana na mazingira yaliyopo Zanzibar kama ifuatavyo

1~Jografia ya eneo:England ni kisiwa ambapo imezungukwa na mito mingi pamoja na bahari ikipatiwa usaidizi na bandari zake mbali mbali ikiwemo bandari ya manchester,Irish,Liverpool na nyenginezo hivyo nchi nyingi za ulaya ziliizingatia England kama kitovu cha biashara kwa kutumia bandari zake mbalimbali hii ilirahisisha kupatikana kwa malighafi kutoka sehem mbali mbali za dunia.

Zanzibar nayo ni kisiwa hakina mito ila kimezungukwa na bahari ya hindi sehem mbali mbali zake kikiwa imepakana na nchi ya Tanzania bara,kisiwa cha mombasa kenya,kisiwa cha comoro ambapo meli kutoka sehem mbali mbali za Afrika mashariki na duniani ikiwemo oman na kwengineko zinaweza kuja na kutia nanga katika bandari zake,kuleta malighafi na kufanya biashara na nchi hivyo kuwekeza katika bandari ya kisasa zanzibar kutaziunganisha nchi nyingi tofauti kibiashara kupitia bahari na kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha biashara kama ilivyokuwa kwa England

2~Utulivu wa kisiasa:Kupitia mapinduzi matukufu ya England ya mwaka 1650s ilipelekea kuimarika kwa amani pamoja na usalama wa nchi hali iliyopelekea kuvutia kwa wawekezaji kutoka kila pembe kuwekeza mitaji yao ndani ya England ukilinganisha na nchi nyengine za ulaya kwa wakati huo zilizokua katika matishio na athar za vita.

Kupitia kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa iliyopo zanzibar tumeshuhudia amani na utulivu ukirejea visiwani hivyo hii ni fursa ya kuvutia uwekezaji zaid na hata watalii wanazidi kumiminika kila siku

3~ Uwepo wa makaa ya mawe na chuma ndani ya England:England ilinufaika kwa kuwepo rasilimali za ndani za makaa ya mawe pamoja na chuma ambazo zilitumika kusisimua viwanda vyake ambapo makaa ya mawe yalitumika kama nishati viwandani na chuma kilitumika kutengenezea mashine mbali mbali za viwanda.

Zanzibar nayo ipo na uwezo huo sababu ina rasilimali ya gesi asilia pamoja na mafuta rasilimali ambazo zinahitaji kuibuliwa tu ili ziweze kusisimua na kuinua uchumi wa nchi ambapo zitaweza kutumika sehem tofauti na pia ni zenye uhitajio na soko kubwa duniani

Zanzibar ni nchi ya kisiwa chenye watu wachache wasiozidi milioni 2 inawezekana zanzibar ikawa na rasilimali chache ila uwepo wa eneo kubwa la bahari pamoja na rasilimali za mafuta na gesi ni nyingi kutosheleza kujitajirisha kiuchumi kwa muda usiozidi miaka 10 ikiwa utapatikana mtaji wa kutosha wa kuziibua rasilimali hizo zilizopo, uwepo wa mipango madhubuti na yenye kutekelezeka sambamba na matumizi sahihi, siioni Zanzibar kuwa masikini ikiwa kila mmoja wetu atakua mzalendo na kuwajibika katika dhamana na nafasi yake.
 
Back
Top Bottom