dinoza
Member
- Jun 22, 2024
- 8
- 5
Kwa miaka mingi kupita kwa hivi leo tunaita ni stori, kumbuka na rejea mwaka 1924 kulikuwa na watanzania nao waliishi kama wewe uishivyo hivi sasa mwaka 2024. Ni miaka 100 imepita tangu 1924, ni kizazi na vizazi vimepita na miaka hairudi nyuma inasonga mbele, kufikia mwaka 3024 basi fahamu kwamba kutakuwa na watu wanaishi kama unavyoishi hivi sasa, napo itakuwa imepita miaka 100 ambayo ni kizazi na vizazi.
Kinachofanya tutofautiane kizazi na vizazi ni mtindo wa maisha(life style), miaka ya 1924 mtu kumiliki baisikeli ilikuwa ni mjadala mkubwa na lazima uhojiwe kisawasawa, lakini hivi leo tulipo kumiliki baisikeli ni suala lisilo na maana yoyote ni kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha, sasa hivi tulipo hapa kumiliki ndege(private jet) ni suala ambalo litaleta mjadala lakini acha nikwambie miaka ya 3024 kumiliki ndege litakuwa ni suala la kawaida mno kutokana na life style ya miaka hiyo.
Naomba tulejee elimu ya Tanzania toka mwaka 1924 ilikuwa ni elimu ya kikoloni,ambayo haitoweza kukusaidia kwa chochote, elimu hiyo imeendelea mpaka miaka ya 2000 ina mana ni vizazi na vizazi vinasoma kitu kilekile toka mwaka 1924 kitu ambacho sio sahihi,kama nilivyotoa utangulizi hapo awali kwamba kila kizazi kina mtindo wake wa maisha kwanini katika suala la elimu miaka hii ya 2024 tunaishi miaka ya 1924 ni mambo ambayo yalishapita muda wake.
Elimu imekuja kushindwa nguvu na kuonekana sio ya maana kwamba tuna wasomi ambao hawawezi kujitegemea kutokana na elimu walizozipata, naomba kueleza kwamba hapa sizungumzii mabadiliko ya shule binafsi kujifunza kingereza, kwenda shule na mabasi, madarasa kuwekewa vioo na marumaru, umeme, kula chakula hukohuko shule, hapa ninamaanisha mfumo mzima wa elimu kwanini haubadiliki.
Mabadilika mitaala na mada lakini sio mifumo(system), vijana wa sasa tunao uwezo wa kubadilisha mfumo wa elimu kwenda katika mfumo wa kisasa ambao ndio utakuwa unaendana na mabadiliko ya sayansi na tekinolojia kama ifuatavyo;
Kuwepo na elimu ya msingi kwa miaka 7, kisha elimu ya sekondari ambayo ndio hasa inahitaji mabadiliko kama ifuatavyo...
Mwanafunzi akishahitimu elimu yake ya msingi atahitajika kuchagua kitu ambacho ana uwezo nacho mfano; mwanafunzi huyu ana uwezo wa kuwa dakitari basi ataanza kusomea udakitari akiwa kidato cha kwanza na achague ubobevu anaouweza kama ni daktari wa macho basi aanze kusomea macho akiwa kidato cha kwanza kwa miaka 4 kisha afanye mtihani moja kwa moja aingie chuo na kujiongezea maarifa zaidi kuhusu macho tu, ili abobee zaidi kiasi kwamba mtu akisumbuliwa na jicho akikutana na daktari huyo anasaidiwa kwa wakati na umakini wa hali ya juu, kadhalika vivo hivyo kwa kada zingine kama urubani, ualimu, uhasibu, ushonaji, udereva, uinjinia, ufundi, kila mwanafunzi aweze kujiendeleza na fani awezayo kama mwanafunzi ana kipaji cha muziki basi aimbe, ana kipaji cha mpira basi na aingie uwanjani yeye na mpira tu.
Suala la kuwalundikia wanafunzi masomo mengi kwangu mimi sioni kama lina tija kwasababu mwanafunzi anakalili na sio kuelewa ndio maana ukiingia mtaani ukimwuliza mtu aliyemaliza kidato cha nne akakaa mtaani miaka kadhaa mwulize what is biology hawezi kuelezea kutokana na kwamba alikalilli darasani kutokana na kuwa na masomo mengi.
Elimu yetu imekuwa ikisaidia wanafunzi darasani kujibu mitihani kwa kukalili na sio elimu ya vitendo kuelewa zaidi.
Mabadiliko ya mfumo huu yataleta maendeleo na kuongeza ufanisi wa elimu na ujuzi kupunguza miaka mingi ukiwa katika elimu,mtu anasoma takribani miaka 25, kupitia jukwaa hili nawomba vijana katika kizazi chetu tuwabadilishie watoto wetu mfumo wa elimu na sio mitaala.
Kwa kufanya hivi tunaweza kuwa na madakitari wabobevu, walimu wabobevu,wachezaji mpira wabobevu, wanamuziki, wafanyabiashara, viongozi, wanasheria wabobevu, kila mtu awe na taaluma yake na hakuna kuchanganyikana.
Tupo katika mfumo ambao mtu kasomea uwalimu na anakuja kupata ajira ya uhasibu ilimradi awe na cheti tu kitu ambacho sio sawa.
Mfano dhahiri tunaona wenzetu wa mataifa endelevu mtoto akigundulika ana kipaji cha kucheza mpira basi maisha yake yote yataelekezwa huko katika akademi za mpira wa miguu, vivyo hivyo kwa madakitari anabobea katika kutibu ugonjwa wa aina fulani.
Dakitari wa tumbo hawezi kumtibu mgonjwa wa meno. Napenda kuiona Tanzania mpya miaka ijayo na hii itatokana na kubadilisha mifumo hii kwa sasa.
Hakuna kinachoshindikana hata treni zamani ziliendeshwa kwa makaa ya mawe lakini kutokana na mabadiliko leo tunazo treni zinazotumia umeme.
Kwanini tushindwe sekta ya elimu.
Naiomba Serikali na wadau wa elimu hasa vijana kutoa maoni juu ya elimu hii bora ambayo itapunguza ukosefu wa ajira kwa asilimia kubwa.

Upvote
5