Saint Leo
Member
- Nov 9, 2018
- 46
- 57
UTANGULIZI:
Kulingana na takwimu za hivi karibuni(Sekta ya Mifugo)Idadi ya mifugo hapa nchini imeongezeka ambapo idadi ya ng’ombe imeongezeka kutoka milioni 33.9 hadi milioni 35.3; mbuzi kutoka milioni 24.5 hadi milioni 25.6; kondoo kutoka milioni 8.5 hadi milioni 8.8. Kuku wameongezeka kutoka milioni 87.7 hadi milioni 92.8 ambapo kuku wa asili wameongezeka kutoka milioni 40.4 hadi milioni 42.7 na kuku wa kisasa wameongezeka kutoka milioni 47.3 hadi milioni 50.1; nguruwe kutoka milioni 3.2 hadi milioni 3.4;
Sekta ya Mifugo katika mwaka 2021 ilikua kwa kiwango cha asilimia 5.0 sawa na mwaka 2020 na mchango wake katika Pato la Taifa ulikuwa asilimia 7.0 sawa na mwaka 2020;
Katika Makala hii ningependa kujikita zaidi kwenye aina tatu za wanyama ambao ni Ng'ombe,mbuzi na kondoo,hii ni kwasababu kwa wanyama hawa inaonekana CHANJO imesahaulika kitu kinachofanya mifugo mingi kupotea kila mwaka na gharama za utunzaji kwa wakulima kuongezeka.
CHANJO
Chanjo ni dawa ya kibaiolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani. Jinsi chanjo zilivyomuhimu kwa kukinga magonjwa mbalimbali kwa binadamu,ndo hivyo hivyo kwa wanyama wengine!
HALI YA CHANJO KWA WANYAMA NCHINI.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa zaidi ya Ng'ombe,mbuzi na kondoo barani Africa,lakini mifugo hii imekuwa ikishambuliwa na magonjwa mengi ilihali mengine yanaweza kuzuiwa kwa njia ya chanjo.Takwimu zinaonesha ni aslimia 10 pekee kati ya hiyo mifugo ndo huwa inapatiwa chanjo.
UMUHIMU WA CHANJO KWA WANYAMA NA WAFUGAJI.
1. Kulinda afya ya wanyama na kupunguza gharama za matibabu. CHANJO ni mojawapo ya njia rahisi zaidi ya kuzuia ugonjwa,siku zote watu wanasema Kinga ni bora kuliko tiba. Wafugaji nchini wamekuwa wagumu kuelewa haya maneno na kuyatumia kwa mifugo yao. Mfano,kumtibia ng'ombe aliyeugua homa ya mapafu maarufu kama (CBPP) inaweza ikagharimu zaidi ya Tsh50,000 mpaka anapona au asiweze kupona kabisa.,Ng'ombe huyo unaweza kumchanja kwa gharama ndogo zaidi(chini ya Tsh600) na ukawa na uhakika wa afya yake! Hapa elimu zaidi inahitajika kwa wafugaji.
2. Chanjo inapunguza vifo. Kuna magonjwa ya mlipuko mengi hata kwa wanyama kama ilivyo kwa binadamu,magonjwa haya yanaweza kuzuiwa kwa chanjo. Chukulia mfano Corona ilivyotokea kwa upande ya afya ya binadamu,jinsi chanjo ilivyosaidia kupunguza vifo ndo hivyo hivyo inaweza kupunguza vifo hata kwa mifugo yetu. Ni lazima hili suala tulitilie maanani zaidi.
3.Chanjo inasaidia mazao ya Mifugo yanakuwa bora zaidi. Hii ina maana kubwa sana kwa wafugaji. Tukiwa na takwimu nzuri ya chanjo za magonjwa,itasaidia sana mazao ya mifugo kama nyama,maziwa nakadharika kuuzwa nje. Inakuwa na faida kubwa zaidi kwa wafugaji na taifa kwa kuongeza kipato. Biashara za kuuza nje ya nchi zitaongezeka mara dufu.
-faida za chanjo kwa mifugo ni nyingi sana nimegusia tu hizo chache,
NINI KIFANYIKE KUONGEZA IDADI YA MIFUGO KUPATA CHANJO.
1. Elimu kwa wafugaji. Jinsi ya kufikisha elimu kwa wafugaji ndo ilipochangamoto. Kuna watu wengi ikiwemo vijana wamekuwa na elimu ya ufugaji kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini. Serikali inaweza watumia hawa vijana kutoa elimu kwa wafugaji kupitia njia mbalimbali kama semina kwenye maeneo husika. Serikali ipo siku zote,imefikia wapi? Hapa ndiyo utaona mwanya wa taasisi binafisi kuingia kwenye suala la chanjo kwa wanyama nchini.
USHIRIKI WA TAASISI AU MTU BINAFSI
Mtu au taasisi inaweza chukua vijana wenye nguvu na uelewa wakaweza shiriki katika utoaji wa elimu kuhusu chanjo na watu wakaweza kuchanja! Hii itakuwa na maslahi kwa taasisi,vijana kama ajira na wakulima wenyewe. Suala likiwa endelevu miaka kadhaa tunaweza fanya mapinduzi makubwa sana ya hii sekta yetu ya mifugo ikiwemo kuondoa kabisa baadhi ya magonjwa ya mifugo kama SOTOKA YA MBUZI NA KONDOO(PPR) kama ilivyo kwenye kampenzi ya kutokomeza ugonjwa huu Africa.
Thamani ya wanyama nchini itaongezeka mara dufu endapo watakubalika kuuzwa nje ya nchi kwenye soko la dunia.
CHANZO CHA CHANJO ZA UHAKIKA
Kwa bahati nzuri Tanzania kumekuwa na makampuni bora sana na uhakika ambayo yamethibitishwa na serikali kwa uzalishaji wa chanjo za wanyama chini. Hii itasaidia kuhakikisha chanjo zinazohitajika zinapatikana kwa urahisi na usalama zaidi pia kwa gharama nafuu nchini. Kampuni mojawapo ni HESTER BIOSCIENCE AFRICA LIMITED iliyopo KIBAHA nchini.
Hii makala imelenga zaidi kutoa hamasa kwenye suala la chanjo kwa wanyama wakubwa kama N'gombe,kondoo na mbuzi kama watu wanavyozingatia kwa wanyama wadogo kama kuku na mbwa. Kwa pamoja tunaweza na Mungu awabariki.

Upvote
2