Mapinduzi ya Zanzibar yako hatarini.. Wazanzibari wamelala...


Unazungumza kama una uhakika sana wa unachozungumza... wanaonisoma vizuri wanaelewa ninasema nini. Kama hujanipata naweza kukusaidia kuelewa kile ambacho ninakisema.
 
Mwanakijiji, acha kuwatisha wa zanzibar. Madai yako kuwa JWTZ inalinda mapinduzi ya zanzibar, unapaswa kuelewa kuwa hakuna Tanzania bila ya Zanzibar. Unataka kuaminisha umma kuwa wabara tuna uchungu na Zanzibar kuwashinda wazanzibar wenyewe ambao ndg zao kibao walipoteza maisha ktk kuudai uhuru? Zanzibar italindwa na wa zanzibar wenyewe.
 
As it reads in my signature; "I support Let Zanzibar go Movement" waondoke hata leo. enough is enough
 

Wazenj nendeni zenu hati sisi tumewachoka....hamna kazi hamna elimu, ni malalamiko na kupiga domo tu.
 
Kha! asilimia kubwa ya wa zanzibar wamezaliwa baada ya mapinduzi kwa hiyo hawana sababu yoyote ya kuendeleza upumbavu huo, na tayari wameshajuwa huo ni ujanja wa Yanganyika tu ili waendelee kuitawala nchi yao.kwa hiyo tafuta cd nyengine hiyo naona hawataoskiliza tena.
 
Off-topic kidogo......hivi jina chama cha "mapinduzi" lina uhusiano wowote na "mapinduzi" ya Zanzibar? Najaribu kufikiria sababu ya wazanzibari sasa kuanza kuona uwepo wa neno "mapinduzi" katika jina la serikali yao ni kero kwao!
 

Mbona ninyi "counter-revolutionists" mnapinga bila hoja kama ambavyo "revolutionists" wanajibu kwa hoja? Nobody has given us a reason why Zanzibar will be better-off outside the Union. Au mnataka tuanze kuwachambua kuwa sura na rangi zenu zinawasuta? Sijaona mzanzibari mweusi (mwenye zanzibar) akipiga domo kudai muungano uvunjike. Wote ninyi TV na video zinawaumbua kuwa mna asili ya waarabu.

Mtauvunja Muungano lakini mapinduzi yatalindwa kwa damu ya wabara. Harudi tena Muarabu katika pwani ya Afrika Mashariki!
 

Unajuwa siku zote adui yako muombee njaa. Lakin vile vile dua la kuku haliwezi kumpata mwewe.

Mimi nimeishi sana Tanganyika na kubahatika kusomea huko kuanzia skuli darasa la sita Mchikichini, Tambaza Boys sec, Ilboru boys Sec na UDSM na nikapita JKT ruvu na kumalizia Mgulani. Hivyo nimeona mngi sana ya kasumba kwutoka kwa wabara dhidi ya waZnz.

Nakumbuka hata darasani walikuwa na dharau sana lakin kichwani wengi walikuwa hamna kitu. Wao na kwa jinsi ya mafunzo walopewa huko sunday school ni kuona kila Mznz ni goi goi na hawezi kuwa na akili darasani na hawezi uongozi. Kitu hicho kwa watu wa Bara ni chuki walizopandikiziwa na makovu ya UKOLONI wa mwingireza mbao ulitukuza sana dini yao na kujenga skuli nyingi za madh'hebu yao ukilinganisha na zile za waislam. sasa wamezoea kuona wao ni wasomi na wana uwezo wa kila kitu kuliko wengine.

Kumbuka kwa hilo ndilo liliweza kupelekea hata muasisi wa Chadema na waziri wa fedha mstahafu Mzee Mtei kuona kwanini kuna waislam wengi katika Tume ya kukusanya maoni ya kuundwa kwa katiba mpya. Kwani wanaamini waZnz hawawezi chochote.

Sasa ndio jua linawachwe na kuleta ghilba na fitna kama hizo.

Kwa mwenye akili timamu nafikiri atajiulize.
1. Iweje jiichi lenye watu zaidi ya milioni 12 lilazimishe kuungana na nchi yenye watu chini ya laki moja na nusu. tena kwa uwiano ulio sawa kwa kila kura?
2. Tena baya zaidi jiinchi hilo likubwa likubali kupoteza utaifa wake na jina lake na kukumbatia jina la muungano.
3. Cha aibu zaidi jiichi hilo kukubali lisiwe na serikali yake na kukumbatia ile ya muungano wakti kiichi kidogo kinakuwa na Serikali yake.

Kwa mwenye akili atagundua kuna jambo hapo limefichwa ambalo mpaka leo wenzenu wa upande wa pili hawalioni wala kuligundua si kwa sababu JKN ni saint bali ni uzuzu wa mawazo na kutegemea kutafuniwa kila kitu.

Kwani mtu mzima unaweza kumtishia nyau?

 
Barubaru,
Shukuru ulikuja mapema Tanzania bara. Ndio maana ukaweza hata kusoma. Ungekuwa kule sasa hivi zingebaki stori tu trust me!!! Halafu jua kinawachwea kina nani, Zenj au huku bara?
 

Tutajie japo mkristo mmoja anaeng'ang'ania muungano! Si Pinda alishawaambia - tena ndani ya bunge- kuwa mkitaka jitoeni? Mnasubiri nini?
 

Mkuu, watachonga kwa saana!
Ndoa hii hana talaka! Labda wakazoe ule udongo wa Tg na Z'bar uliokorogwa kwenye kibuyu na Nyerere wakishirikiana na Karume kuumwaga bahari ya Hindi, wauchambue huu ndio wa kwetu na huu ndio wa kwenu! Tulieni mzae tu! Nilikuwa siupendi muungano huu saana lakini hapa tulipofikikia ninadiriki kusema toka rohoni kwamba;
"MAPINDUZI DAIMA! MAPINDUZI DAIMA! MAPINDUZI YADUMU!"
 

Mhh...Nafikiri kuna mtu kaaiiba Password ya Barubaru, Moderator hebu check kama aliyeandika kweli ndiye Barubaru?
 
Barubaru,
Shukuru ulikuja mapema Tanzania bara. Ndio maana ukaweza hata kusoma. Ungekuwa kule sasa hivi zingebaki stori tu trust me!!! Halafu jua kinawachwea kina nani, Zenj au huku bara?

Ndahani,

Kumbuka dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana hususan ubaguzi wa kidini ambao Tanganyika imerithi kutoka kwa wakoloni wa Kizungu wa kujiona iimani moja no bora zaidi kuliko nyengine. Imani hiyo ndio inayostahili kila kitu kuliko ingine na kujiona wao first citizen ship na wengine kuona ni second citizenship.

labda nikuulize.
Je unajuwa kwanini waTanganyika walidai uhuru wao toka kwa wazungu?
Hilo ndilo sasa litatokea kwa watu wa imani inayodhulumiwa haki zao na stahiki zao huko Tanganyika kama mtakuwa nje a muungano.

Kumbuka kuwa hakuna marafu ...

 

Kisheria serikali ya mapinduzi haipaswi kuwepo. Kwa nini? Kwa sababu tulipokaribisha vyama vingi 1992 umaana wa mapinduzi haukuwepo pia kwa kuwa mapinduzi yale yaliiondoa serikali iliyopatikana kupitia vyama vingi. Sasa unakuwaje na serikali ya mapinduzi huku kuna chaguzi zimefanyika?
 

Wewe ni mwandishi wa magazeti?

Well serikali iliyokuwepo before 1964 was just an arab puppet (according to you) serikali ilokuwepo after 1964 was also a puppet of a black colony Tanganyika (FACTS) and the government of the black colony before 1961 was a puppet of germany and the government of black colony after 1961 was a puppet of USA, and the government of two puppeted nations is also a puppet! Therefore zanzibaris are simply tryng to overthrow the puppet government and to get their own controlled government while the otherside(unknown as tanganyika) are tryng to be loyal to their masters (USA) and willing to do anything for them!

Who asked the JMT to protect SMZ if JMT couldnot even protect their regions? If its not for the intrest of Tanganyika! Arent you ashamed that your country is not even known as a semi nation state??

History repeat itself, if SMZ were here by revolution they will be out by revolution! There is proof! 🙂 have a nice day reporter!
 
Hili naamini ni kweli ndio maana tunataka tuwasaidia Wazanzibar watoke walinde mapinduzi yao wenyewe au wawaombe radhi wale waliopinduliwa kwa mapinduzi yaliyopangwa na Tanganyika!!

Hivi hufahamu kweli? Wazanzibari wooooote ama labda niseme 95% hawapo tayari kulinda mapinduzi ya dhulma na ya uongo! Sasa wewe unataka kuwasaidia nini? Wasaidie wapindue saivi basi,sijui utawapa msaada gani, maana ushaambiwa yule shahidi aliyeshuhudia kutia saini ya muungano basi na yeye anasapoti jamhuri ya watu wa zanzibar, hao watoto wa ASP wenyewe nao wanataka jamhuri yao sasa wewe na hao watoto wa ASP sijui nani wa kumsapoti, na nani aombwe radhi? Wazanzibari wawaombe radhi waarabu kwa lipi? Mapinduzi yamefanywa na kina john okello kisha waombe radhi wazanzibari?? Mbona unataka kufanya watu wacheke tena mwanakijiji?

Ukweli unajulikana, wengine tunao mababu wa tangu enzi hizo za mapinduzi, kwaiyo tunajua nani walipanga mapinduzi. We unafikiri Nyerere atatunga kitabu ambacho kitamfanya aonekane mbaya? Ushawahi kusoma history ukaona kama serikali ya tanganyika imekubali kufanya uchafu?
 

Hiyo mipovu inavyokutoka mpaka unapoteza mwelekeo,kunywa maji,tulia halafu rudia tena kutoa hoja tuelewe ujumbe unaotaka kuwasilisha.Ni ushauri tu.
 
Hiyo mipovu inavyokutoka mpaka unapoteza mwelekeo,kunywa maji,tulia halafu rudia tena kutoa hoja tuelewe ujumbe unaotaka kuwasilisha.Ni ushauri tu.


Mamy punguza jazba japo inauma lakin ukweli ni ukweli japo umekujeruhi.

Umsome kwa utulivu sana na kwa uzuri sana between lines kwa NIA ya kuelewa na insh'Allah utaelewa na kama kutakuwa na mush'kira au pahala hapakukujilia vizuri basi mlango upo wazi kuuliza.

Pole sana mamy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…