Uchaguzi 2020 Mapingamizi ya wagombea Urais yatamfanya mwamuzi awe kama Pontio Pilato

Uchaguzi 2020 Mapingamizi ya wagombea Urais yatamfanya mwamuzi awe kama Pontio Pilato

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Najaribu kuifuatilia safari ya njia ya msalaba kupitia Biblia Takatifu, kiukweli kuna baadhi ya maamuzi ni vigumu kuyafanya ukiwa vuguvugu ni ama uwe na Roho Mtakatifu au uwe na Roho wa Shetani.

Naamini Mungu atamuongoza vema Jaji Kaijage endapo kuna mapingamizi yoyote yatatokea.

Pontio Pilato mwisho alisema " Niliyoandika Nimeyaandika"

Nawatakia wednesday yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nawashauri wasiwekeane mapingamizi. Kwa kuwa washateuliwa basi waturuhusu raia ndio tuamue.

Kila mmoja ana mapungufu.
 
Kama Jiwe akiagiza aenguliwe,nani atapinga?
Ataenguliwa yeye!!! Mwaka huu lolote laweza tokea. Sidhani kama watu wenye akili kwenye vyombo vya dola wataruhusu nchi iingie kwenye machafuko au kuwekewa vikwazo kimataifa kwa matakwa ya mtu mmoja tu. Hapana!!!
 
Kama maamuzi ya Tume hayawezi kupingwa popote hata mahakamani,basi sheria hii ni ya hovyo mno.

Hii ni moja ya sababu kubwa kwa mimi kutokupiga kura ndani ya nchi yangu. Hakuna mtu mwenye akili timamu kuendelea kushiriki katika uchaguzi wa viongozi baada ya kuelewa jambo hili.
 
Kwanini mapingamizi wao waje uwanjani watapata mapingamizi huku kwa wananchi.
 
...Yesu akainama chini akaandika aloandika, kisha akainua macho kutizama, ...wanaume wote walishatimua mbio akabaki yeye na mwanamke aliyesingiziwa.... akamwambia enenda zakoo sikuhukumu ukatende memaaa.... 😂 😂

Maneno yaliyomo kwa Bible/Quran huwa yanatuliwaza sanaaa na kutufikirishaaa 🍷
 
Back
Top Bottom