Mapishi kwa asiyejua

Mapishi kwa asiyejua

Allah's Slave

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2008
Posts
562
Reaction score
46
Kesho nipo home siku nzima, Nataka nipike Pishi zuuri ili nile na familia yangu. Ni kitu gani kizuri simple naweza kupika? Nataka nimsuprise wife na nimuweke na housegirl pembeni. Kesho nashangaza familia.

Kesho baba anaingia jikoni. Nipike nini na kivipi? Kitamu alafu kisiwe na macomplication kabisaaaaa. Mkinijibu mapema naamkia kununua asubuhi na kuwapikia mchana.

Lazma niwahi ili nikikosea wife arekebishe na iwe mwisho wa suprise.
 
andaa samaki chukuchuku na ndizi za kuchemsha mkuu ngoja nimuite @gfsonwife kutuletea mahitaji..
 
wee huu msosi ukute samaki mwenye asili ya mafuta utajutaa kukutwa na bwana pepsi. huwa ni mtamu sana sana binafsi napenda sana ndizi za samaki na haswa Sato ama jodari
 
Nimeona maandishi ya Pespi nikaingiwa hamu. dah!
 
wee huu msosi ukute samaki mwenye asili ya mafuta utajutaa kukutwa na bwana pepsi. huwa ni mtamu sana sana binafsi napenda sana ndizi za samaki na haswa Sato ama jodari
gfsonwin hivi unavokiandaa si unachemsha ndizi pamoja na samaki kwa pamoja na vitu kama vitunguu vinakatiwa tu juu au?
 
hapana mie huwa nafanyaga hivi.

namchukua samaki na kumuweka viungo vyote kisha namueka pembeni, nachemsha ndizi kama dk 10 hivi halafu namminia samaki akiwa na viugo vyake juu basi samaki atanza kuiva pamoja na ndizi.

ndizi ni ngumu kidogo hivyo kuzichemsha inasaidia kuzifanya ndizi ziive vyema
 
  • Thanks
Reactions: PLL
Hizi surprise nyingine msije mkalaza wenzenu msalani kwa mivurugo ya tumbo......
 
Huna haja ya kuhangaika na misosi ya Ajabu hii hapa menu rahisi!!
Asubuhi ingia jikoni chukua Unga ngano, mayai hata 4 na maji ya uvugu vugu weka unga kwenye chombo kipana Kama bakuli uchanganye pika chapati za maji!! Kama 3 kwa kila mwana family inatosha!! Mchana tengeneza dagaa wa kigoma na mboga za majani safi na ugali wakati unapika weka Maharage jikoni! Ukifika jioni unga Maharage safi na wali nazi hapo kuna kua na fruits kidogo!! Watoto watafurahi na mama atafurahia very simple healthier meal!!
 
hapana mie huwa nafanyaga hivi.

namchukua samaki na kumuweka viungo vyote kisha namueka pembeni, nachemsha ndizi kama dk 10 hivi halafu namminia samaki akiwa na viugo vyake juu basi samaki atanza kuiva pamoja na ndizi.

ndizi ni ngumu kidogo hivyo kuzichemsha inasaidia kuzifanya ndizi ziive vyema

Thank you sister
 
Last wiki sikupata jibu mapema hivyo sikupika, Ntapika this weekend. Tatizo hivyo viungo vya samaki ni vipi? Ila chakula kinaonekana Simple sana hiki nakiweza kuchemsha tu ntashindwaje. Nitajie hivyo viungo vya samaki ulivyosema unaviweka. Ahsante
 
Hizi surprise nyingine msije mkalaza wenzenu msalani kwa mivurugo ya tumbo......

Yaani umenichekesha.................. Ndio maana ya kujaribu ila pia huenda watoto wakanikubali kuliko hata mama yao kwenye mambo ya mapishi.
 
hapana mie huwa nafanyaga hivi.

namchukua samaki na kumuweka viungo vyote kisha namueka pembeni, nachemsha ndizi kama dk 10 hivi halafu namminia samaki akiwa na viugo vyake juu basi samaki atanza kuiva pamoja na ndizi.

ndizi ni ngumu kidogo hivyo kuzichemsha inasaidia kuzifanya ndizi ziive vyema

Viungo gani ivo?!
 
Last wiki sikupata jibu mapema hivyo sikupika, Ntapika this weekend. Tatizo hivyo viungo vya samaki ni vipi? Ila chakula kinaonekana Simple sana hiki nakiweza kuchemsha tu ntashindwaje. Nitajie hivyo viungo vya samaki ulivyosema unaviweka. Ahsante

kama unataka kupika ndizi za samaki basi mahitaji yake ni haya:-

  • samaki mmoja mkubwa abt 1/2kg
  • ndizi 6 mshare kama ni mchaga
  • karoti moja
  • hoho moja
  • kitunguu kimoja
  • tangawizi kiasi, na kitunguu swaumu kidogo,(vilivyopondwa) chumvi na limao

njia

  1. paa samaki wako kisha umuoshe vizuri. kisha mchane mnofu wake ili adondoke maji
  2. paka vitunguu swaumu, tangawizi limao pamoja na chumvi kwenye samaki wako kisha mweke pembeni.
  3. Menya ndizi zako vizuri na uzioshe
  4. katakata kitunguu, karoti na hoho kisha changanya na ndizi na uzitie maji kisha zibandike zichemke jikoni kwa muda wa dk 10.
  5. mchukue samaki uliyekuwa umemuandaa mtie kwenye ndizi bila kukoroga, ongeza maji kiasi cha kufunika samaki wako, ongeza mafuta kidogo. kisha funika ziendelee kuchemka.
  6. zichemsha hadi ndizi zilainike kabisa na hakikisha ziwe na supu ya kutosha.
  7. ipua ndizi zako na andaa kwa ajili ya kula.
 
Ndio maana naipenda JF. Ahsante sana hapa nimesha Print na lunch ya leo naweka kwenye gari kabisaaa tayari kwa kufanya mambo weekend.

Members kama nyinyi mnaotumia muda wenu na resources zenu kutusaidia na kutuelimisha, Allah Awabariki Sana na Mpate zaidi na zaidi maana kupata kwenu ni manufaa yetu sote. Ntakuja na feedback after this weekend
 
Back
Top Bottom