Allah's Slave
JF-Expert Member
- Mar 14, 2008
- 562
- 46
andaa samaki chukuchuku na ndizi za kuchemsha mkuu ngoja nimuite @gfsonwife kutuletea mahitaji..
wee huu msosi ukute samaki mwenye asili ya mafuta utajutaa kukutwa na bwana pepsi. huwa ni mtamu sana sana binafsi napenda sana ndizi za samaki na haswa Sato ama jodari
gfsonwin hivi unavokiandaa si unachemsha ndizi pamoja na samaki kwa pamoja na vitu kama vitunguu vinakatiwa tu juu au?wee huu msosi ukute samaki mwenye asili ya mafuta utajutaa kukutwa na bwana pepsi. huwa ni mtamu sana sana binafsi napenda sana ndizi za samaki na haswa Sato ama jodari
gfsonwin hivi unavokiandaa si unachemsha ndizi pamoja na samaki kwa pamoja na vitu kama vitunguu vinakatiwa tu juu au?
hapana mie huwa nafanyaga hivi.
namchukua samaki na kumuweka viungo vyote kisha namueka pembeni, nachemsha ndizi kama dk 10 hivi halafu namminia samaki akiwa na viugo vyake juu basi samaki atanza kuiva pamoja na ndizi.
ndizi ni ngumu kidogo hivyo kuzichemsha inasaidia kuzifanya ndizi ziive vyema

Hizi surprise nyingine msije mkalaza wenzenu msalani kwa mivurugo ya tumbo......
hapana mie huwa nafanyaga hivi.
namchukua samaki na kumuweka viungo vyote kisha namueka pembeni, nachemsha ndizi kama dk 10 hivi halafu namminia samaki akiwa na viugo vyake juu basi samaki atanza kuiva pamoja na ndizi.
ndizi ni ngumu kidogo hivyo kuzichemsha inasaidia kuzifanya ndizi ziive vyema
Last wiki sikupata jibu mapema hivyo sikupika, Ntapika this weekend. Tatizo hivyo viungo vya samaki ni vipi? Ila chakula kinaonekana Simple sana hiki nakiweza kuchemsha tu ntashindwaje. Nitajie hivyo viungo vya samaki ulivyosema unaviweka. Ahsante
kama unataka kupika ndizi za samaki basi mahitaji yake ni haya:-
- samaki mmoja mkubwa abt 1/2kg
- ndizi 6 mshare kama ni mchaga
- karoti moja
- hoho moja
- kitunguu kimoja
- tangawizi kiasi, na kitunguu swaumu kidogo,(vilivyopondwa) chumvi na limao
njia
- paa samaki wako kisha umuoshe vizuri. kisha mchane mnofu wake ili adondoke maji
- paka vitunguu swaumu, tangawizi limao pamoja na chumvi kwenye samaki wako kisha mweke pembeni.
- Menya ndizi zako vizuri na uzioshe
- katakata kitunguu, karoti na hoho kisha changanya na ndizi na uzitie maji kisha zibandike zichemke jikoni kwa muda wa dk 10.
- mchukue samaki uliyekuwa umemuandaa mtie kwenye ndizi bila kukoroga, ongeza maji kiasi cha kufunika samaki wako, ongeza mafuta kidogo. kisha funika ziendelee kuchemka.
- zichemsha hadi ndizi zilainike kabisa na hakikisha ziwe na supu ya kutosha.
- ipua ndizi zako na andaa kwa ajili ya kula.