Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,012
- 5,571
Napenda sana biskuti, especially nikila na Icecream (nachovya kama ugali na mboga).
Recipe hii nilipewa na Mama Zurie nami nashare nanyi ndugu zangu.
MAHITAJI:
Unga wa Ngano Kikombe kimoja na Nusu.
Butter (Unsalted) vijiko vinne vya chakula.
Sukari(Napendelea iliyosagwa) vijiko sita vya chakula.
Yai Moja.
Vanilla Extract au Flavour yoyote uipendayo.
JINSI YA KUKANDA UNGA:
Weka Siagi kwenye bakuli lako la kukandia.
Weka sukari na uanze kuchanganya kwa kijiko/mwiko hadi vichanganyike kabisa mchanganyiko usiwe na texture ya sukari.
Pasulia yai humo na uchanganye hadi mixture iwe laini itoe kama povu fulani hivi.
Ongeza Unga na uchanganye hadi vichanganyike kabisa.
Weka flavour yako kama Vanilla au yoyote ile(kijiko cha chai kimoja kinatosha).
Ukishachanganya kila kitu weka kwenye friji kwa muda wa dakika 30.
KUOKA:
Washa Oven kwenye 150 Degrees Celcius.
Toa Unga kutoka frijini.
Changanya Unga wako kwa mkono kisha usukume kwenye kibao au sehemu flat na ukate shape mbalimbali.
Panga shape zako ulizokata kwenye baking Sheet.
Weka Baking Sheet yako kwa Oven na Uset muda wa dakika 15-20.
Toa Cookies zako, ziache zipoe na kisha serve kwenye kisahani kizuuriiii tayari kwa kula.