MBITIYAZA
JF-Expert Member
- Jan 22, 2017
- 14,947
- 26,074
Nipende kuwatakieni heri ya Christmas na mwaka mpya wanajf wote!
Imezoeleka kupika vyakula vile vile kwenye sikukuu kubwa kubwa !
Leo tugeukie upande wa pili wa nyama !
Firigisi ni nyama tamu sana; hebu leo tengeneza firigisi za foil kwa familia yako
Maandalizi:
Andaa firigisi zako, zioshe vizuri
Weka viungo uvipendavyo (swaumu, tangawizi, pilipili manga, karoti, hoho, vitunguu vingi(hivi viweke kwa uwingi kuliko kiungo chochote yaani kata hata vitunguu vitatu in cubes))
Changanya hivyo viungo na hizo firigisi zako kisha ziache kwa muda kiasi kwenye friji ziingie viungo
Weka katika foil na ufunge vizuri
Weka kwenye oven(hata mkaa inawezekana) ila hakikisha unaweka kwenye moto mdogo ili ziive vizuri
Muhimu: Weka hata saa moja hivi kama watumia mkaa na uwe unageuza lile foil ili kupata moto kote!
Hakikisha kuna kasupu kamebakia huwa kana ladha mujarabu
Angalia kama zimeiva fresh
Chakula hiki waweza kula na ugali au pilau au wali pemben na juice baridii!
[HASHTAG]#mbiti[/HASHTAG]