Simplelady
Member
- Oct 26, 2009
- 44
- 22
Jamani naomba mwenye kujua namna ya kupika mbege anielekeze tafadhari
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
inbox me kama bado hujapata msaada kwani mimi si mwenyeji sana jukwaa hili
inbox me kama bado hujapata msaada kwani mimi si mwenyeji sana jukwaa hili
pm za nini tena..
Jamani naomba mwenye kujua namna ya kupika mbege anielekeze tafadhari
jinsi ya kutengeneza mbege .
ndizi mbivu aina ya mbembo au ndizi bukoba au mix za ndizi,unazichemsha baada ya kutoa maganda hadi zibadili rangi na kuwa kama kahawia,unaziepua na unaziifadhi kwa muda kwa hali ya hewa ya moshi zinakaa siku saba hadi juu zinaota kama ukijani kwa juu.
unachukua ulezi unauosha na kuchuja mchanga na unatafuta majini ya mgomba unatandika kwa sakafu then unaweka ule ulezi juu yake ukiwa na majimaji kwa kuutandaza mithila ya mtu anayetadanza kifusi,unauacha kwa muda hadi uwe kama unaota then unaubandua na kuuchambua chambua.ukimaliza unauanika juani hadi ukauke (ukitafuna huu ulezi wakati umekauka ni mtamu balaa) then unapeleka mashineni kusaga uwe unga halafu unapika uji wa huo ulezi,hatua ifutayo ni kuchanganya zile ndizi na maji kiasi kama unatengeneza juisi unachuja na kunachanganya na ule uji unakoroga pamoja then unaacha itulie ili yale machicha ya ulezi yachuke chini.baada ya hapo unaweza ukanywa siku hiyo hiyo au ukalaza hadi kesho yake ili ichachuke kuwa pombe.
kama kuna maswali ruksa,ninaandika kwa kutumia simu ndio maana nimeandika kwa kifupi.