Mapishi ya Mchemsho wa ndizi na nyama

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Mahitaji

  • Ndizi mbichi 6
  • Nyama ya ng'ombe (nusu kilo)
  • Viazi mviringo 2
  • Kitunguu swaum tumba tatu
  • Tangawizi 1/2 kijiko cha chai
  • Kitunguu maji kimoja kikubwa
  • Nyanya 1 kubwa
  • Mafuta (vegetable oil) 1/4 kikombe cha chai
  • Chumvi kijiko cha chai
  • Limao moja
  • Pilipili mbili
Matayarisho

Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa


Asprin karibu hubby.
 
Nakuja mama... ngoja nimalizie kurekebisha hiki kitasa...
 
Nyama ikiwa ni ya kitimoto hasahasa Cylinder head, Itapenedeza Zaidi.
 
Kweli babu anafaidi vingi [emoji3]
 
Naomba unitafutie nyuzi zinazohusu mapishi ya tambi. Thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…