Mapishi ya mchicha wa nazi

Mapishi ya mchicha wa nazi

Nanaa

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
5,893
Reaction score
3,709
Mahitaji:

1,Mchicha (Kiasi kinachokutosha).

2.Kitunguu maji.

3.Nazi ( tui zito/ ya pakiti).

4.Curry powder.

5.Pilipili (ukipenda).

6.Mafuta ya kupikia kiasi.

chumvi

Jinsi ya kuandaa:

1.Chambua mchicha wako, uoshe vizuri weka pembeni uchuje maji ( unaweza kuukata kata ukipenda).

2.Weka sufuria jikoni, tia mafuta kiasi, yakipata moto tia vitunguu maji.

3.Kaanga vitunguu, vikiaribia kuwa rangi ya kahawia, weka pilipili nzima, kaanga pamoja na vitunguu.

4.Kisha weka curry powder pamoja na mchicha.

5.Mchicha ukianza kulainika weka tui la Nazi. .changanya vizuri tui na mchicha.

6.Tia chumvi, acha mpaka tui likaukie na uepue mchicha wako tayari kwa kuliwa.

NB; Usifunike sufuria katika hatua zote hizo ( kufunika mboga ya majani kunaifanya itoe maji mengi)
Mboga hii inaweza kuliwa kwa ugali au wali.

CC: farkhina (mwali kakuaa), Dinazarde Mrs Kharusy Angel Nylon Honey Faith mshana junior geniveros na wadau wote.
 
safi sana best mi mchicha unanishinda naupika ila huwi km nnavyotaka mie ntajaribu kwa kweli
 
Bora hiii naunga vizurii sasa yale mambo yetu ya kukanda kanda kitu kiwe lainii ni tafuraniii
 
Hii kitu umeshaivisha Kim nana? Hebu nihabarishe bibie maana nishaanza kujongea pande hizo
 
Last edited by a moderator:
hii safi sana. nkipata ugali na samaki wa kukaanga pembeni, bila kusahau pilipili. shukran
 
Umesahau ndimu

Utalamba hadi vidole

Sema ndio nutrients zinakuwa zimepotea
 
Yani mumie ukiwa unapika mbogamboga ndio unaniita lakini mapishi mengine hauniiti😎
 
Back
Top Bottom