Mapishi ya Mlenda wa majani ya maboga

Mapishi ya Mlenda wa majani ya maboga

Fixed Point

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2009
Posts
11,304
Reaction score
12,746
Mapishi ya Mlenda wa majani ya maboga:
Mahitaji:
1. bamia gram 250
2. Majani ya maboga 200
3. Nyanya chungu (kama utapenda) gram 100
4. Magadi 1/4 kijiko cha chai
5. chumvi - to taste
6. nyanya ndogo 1
7. Karanga zilizosagwa gram 100
8. maji - kikombe 1

Matayarisho:
1. Osha na kata bamia na nyanya chungu vipande vidogovidogo
2. Osha na kata majani ya maboga ndogondogo

Jinsi ya kupika
1. Bandika maji mpaka yachemke
2. weka chumvi na magadi
3. Weka majani ya maboga, bamia, na nyanya chungu
4. vikishachemka kwa kama dakika 5, weka nyanya, acha ichemke kidogo.
5. weka unga wa karanga na acha uchemke kwa kama dakika 5 - 7.
Tayari kwa kuliwa.
Mboga hii inapendeza kuliwa na ugali
 
Mi apo kwenye gram umeniacha kabisa Fixed Point.
Maana uku uswahilin kwetu kuna nyanya za mafungu sh 100, 200 500
Sasa gram 200 ni kama nyanya ngapi za sh ngapi??!
Nadhani umenipata...
Mentor umenichekesha sana. haya tufanye majani ya maboga fungu moja la 150 na bamia za 200. hii imekaaje?
 
Last edited by a moderator:
ha ha haaaa!!! Sasa umejulia wapi kupika mlenda vizuri hivyo?
sisi pia tunakula sana mlenda, na kwa kweli napenda sana kupika, especially napika mlenda mzuri sana. kuna mume wa rafiki yangu akitaka kula mlenda tu anani-call aje kula kwangu
 
sisi pia tunakula sana mlenda, na kwa kweli napenda sana kupika, especially napika mlenda mzuri sana. kuna mume wa rafiki yangu akitaka kula mlenda tu anani-call aje kula kwangu

Duh!!! Ila angalia usije ukaishia kuharibu ndoa ya watu.
 
Duh!!! Ila angalia usije ukaishia kuharibu ndoa ya watu.
hilo haliwezekani kabisa, I know what I am doing and I am happy where I am. more over, she is my bff, hakuna kitakachokuja between us, not even husbands.
 
mimi napenda sana mlenda, naweza kula kila siku na nisichoke. nikiwa naumwa au mjamzito ugali mlenda ndo chakula kinachopanda sana

Wewe!i have to see yu!how cumz ukiwa mjamzito unapenda kula chakula ambacho na mi nakipenda nikiwa mjamzito,kuna sehemu kuna watu walifanya kakitu kwenye uzao wetu!i bet!this is more than jus coincidence mlongo wangu!khaA!
 
wewe!i have to see yu!how cumz ukiwa mjamzito unapenda kula chakula ambacho na mi nakipenda nikiwa mjamzito,kuna sehemu kuna watu walifanya kakitu kwenye uzao wetu!i bet!this is more than jus coincidence mlongo wangu!khaA!
ha haaaaaaa, mlongo wangu uyumwiki?
hapo ndo ujue kuwa kuna kitu, au usikute ni mtoto wa uncle zangu, ha haaaaaaaaaaaaa. kwa kweli itabidi tukutane tuhadithiane kwanza
 
tena waambie unaliwa na nyama ya kuku mlongo wangu!watell watell
wewe, kuna siku ilitokea kesi, nilikuwa kwa uncle wangu, jumapili tumeenda kanisani tunarudi tukakuta mke wa mjomba kachinja kuku kapika na wali. mtoto wake akaanza kuhoji leo ni sikukuu gani, na inakuwaje tumeenda church bila nguo mpya na wakati ni sikukuu
 
Mngoni kwa nyama kha!hapo hajaweka likolo la nyungu pembeni a.k.a pitiku!
 
Mngoni kwa nyama kha!hapo hajaweka likolo la nyungu pembeni a.k.a pitiku!
nyumbani kwangu nina bustani, yaani huwa nahakikisha nanyungu haikosekani. sasa mtoto wangu mmoja ukipika mboga ya majani nyingine tu analalamika "mimi napenda pitiku"
 
Back
Top Bottom