nyumbani kwangu nina bustani, yaani huwa nahakikisha nanyungu haikosekani. sasa mtoto wangu mmoja ukipika mboga ya majani nyingine tu analalamika "mimi napenda pitiku"
Mapishi ya Mlenda wa majani ya maboga:
Mahitaji:
1. bamia gram 250
2. Majani ya maboga 200
3. Nyanya chungu (kama utapenda) gram 100
4. Magadi 1/4 kijiko cha chai
5. chumvi - to taste
6. nyanya ndogo 1
7. Karanga zilizosagwa gram 100
8. maji - kikombe 1
Matayarisho:
1. Osha na kata bamia na nyanya chungu vipande vidogovidogo
2. Osha na kata majani ya maboga ndogondogo
Jinsi ya kupika
1. Bandika maji mpaka yachemke
2. weka chumvi na magadi
3. Weka majani ya maboga, bamia, na nyanya chungu
4. vikishachemka kwa kama dakika 5, weka nyanya, acha ichemke kidogo.
5. weka unga wa karanga na acha uchemke kwa kama dakika 5 - 7.
Tayari kwa kuliwa.
Mboga hii inapendeza kuliwa na ugali
tuweke pitiku kweli, siyo ya mjini ya kukaanga na mafuta na hoho........ ya manji na mwinyu tubwana pitiku kiboko mlongo wangu,bidae tuweke recipe yake hapa!
lazima aling'ang'ania kuku wa kienyeji, ha haaaaaaaaaaaaaaaa (utakoma kama huko uliko hakuna kuku wa kienyeji). mimi pia muoga kuanzisha mazungumzo na watu ambao sijawazoea, hata wadada, ila nikishawazoea sina shida tenaNgoni...apa job kwangu kuna wangoni wawili...
Mmoja ver shy akiwa na watu asiowajua ila muongeaji akiwa na kampani aliyoizoea. Ni mzushi mno na promiseless balaa. Never likes to hang out...baba na mama wote ni wangoni.
Huyu wa pili ndo kama nyie...she loves cooking. Yupo friendly tu kwa wote. Alikuja kwangu cku moja akatupikia ugali ila aling'ang'ania ninunue kuku...now i know y. Heheheheh
lazima aling'ang'ania kuku wa kienyeji, ha haaaaaaaaaaaaaaaa (utakoma kama huko uliko hakuna kuku wa kienyeji). mimi pia muoga kuanzisha mazungumzo na watu ambao sijawazoea, hata wadada, ila nikishawazoea sina shida tena
akikupikia uje utoe taarifa ilikuwaje. kwa huku uliko kama hakuna karanga unaweza hata kutumia peanut butteroook...now i get it! nimeonana naye tena leo asubuhi..ana aibu! ananikumbusha wadada wa miaka ya 80 na early 90s...
Hahaha..kuku wa kienyeji hakupatikana ila nitamuuliza kama anajua hivo vikitu mlivotaja hapo juu!!!
akikupikia uje utoe taarifa ilikuwaje. kwa huku uliko kama hakuna karanga unaweza hata kutumia peanut butter
Mngoni kwa nyama kha!hapo hajaweka likolo la nyungu pembeni a.k.a pitiku!
ahahahhahah sijui ilinipitaje hiii!
pitiku bana haina makuu!
ni majani ya maboga
chumvi
maji
na kapilipili
unakata majani ya maboga vidogo dogo,unaweka maji,na pilipili unabadnika jikoni!
maji yakichemka unaweka mboga
inaiva kama dk 8-10 hiv
halafu weka chumvi!
ehehehheheheh Kaunga come zis way!
Mentor hebu do ze nidful kwa huyo kamwali af unoe mambo!
A LOT IN STORE FOR YU!
lol!