Mapishi ya samaki kambale

allantence

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2012
Posts
353
Reaction score
301
Hello wana JF, natumaini mpo salama wazima wa afya, anayejua mapishi na maandalizi ya samaki Kambale anisaidie jinsi ya kumpika natanguliza shukrani.
 
Msafishe kambale, mtie chumvi mchemshe aive

Kwenye blenda Kata nyanya, tangawizi kiasi na kitunguu saumu...visage kisha weka pembeni.

Bandika sufuria, tia mafuta, kaanga vitunguu maji, tia mchanganyiko uliosaga kwenye blenda, Tia chumvi kidogo nyanya ziive haraka.

Nyanya zikiiva Tia kambale uliyemchemsha mwanzo...na Ile supu yake utakadiria mchuzi, kamulia ndimu au limao.

Kama Una Nazi utaweka pia utakoroga koroga Hadi mchuzi uchemke...ipua tayari Kwa kuliwa.

Nisamehe Kwa mwandiko.
 
Siwezi kula huyo samaki, hata apikwe vipi
 
Tayari kwa kuliwaπŸ’“πŸ˜
 
Mloweke na maji moto sana.

Halafu muoshe weka pembeni.

Katakata vitunguu maji, nyanya,hoho, karoti,bamia nyanya chungu, zote weka kwenye sufuria na ubandike jikoni.

Menya kitunguu swaum, twanga kisha weka kwenye sufuria linachomke jikoni, ongeza tumaji tudogo ili viive

Vikiiva vyote huo mchanganyiko wako dumbukiza huyo kambale weka na tui lako la nazi, tupia na kapilipili.

Songa kaugali lainiiiiii.

Enjoy msosi.

Angalizo: Makambale yakikaa mda mrefu huwa yanatoa funza kwenye bichwa
 
Makambare ni mimba za funza,haa haa
 
Thanks...
Kama ni mbichi je...?
Nawapenda ila naogopa kuwanunua maana sijui niaanzie wapi kupika...
U bachelor tabu
 
Thanks...
Kama ni mbichi je...?
Nawapenda ila naogopa kuwanunua maana sijui niaanzie wapi kupika...
U bachelor tabu
Kambale mbichi msugue vizuri Kwa majivu Ili kutoa ule utelezi, kisha muoshe mtie chumvi na ndimu/limao na umuweke pembeni.
Kisha andaa kitunguu maji, kitunguu saumu, tangawizi na hoho na nyanya. Hapa ukiweza saga vyote kwenye blenda kasoro hoho na kitunguu maji.
Kwenye sufuria kaanga kitunguu maji, kitunguu saumu, tangawizi, tia hoho na nyanya....
Nyanya zikiiva Tia Yule kambale ulomuandaa, kadiria mchuzi kisha funika aive....kadiria chumvi na ndimu kiasi upendacho.
Hapo Yuko tayari kuliwa Kwa ugali.πŸ˜‹
 
😊 Asante kwa darasa. Ubarikiwe maisha marefu
 
Dah! Samaki ananuka shombo utadhani nini sijui! Bonde la Mto Kilombero hawa kambale huuzwa kwa bei ya chini sana wakiwa wabichi. Binafsi, bora nile Kitoga. Ila siyo kambale.
 
Dah! Samaki ananuka shombo utadhani nini sijui! Bonde la Mto Kilombero hawa kambale huuzwa kwa bei ya chini sana wakiwa wabichi. Binafsi, bora nile Kitoga. Ila siyo kambale.
Ukimpata mlete nikupikie boss, anapigwa Nazi huyo humjui.
 
Kwanza eleza kambale wa aina gani alie kaushwa au mmbichi maana mbichi ana maandalizi yake na ni process kidogo utahitaji unga wa ugali vitunguu pilipili mtama tangawizi swaumu na pilipili mwendokasi

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…