SukariTamu, @FP,
Kaunga
Za kunde
*Viambato
Mbale za Kunde------------kikombe kimoja
Maji--------------vikombe vitatu
Giligilani/kotmiri----kicha kimoja kidogo
Mchicha-----------mche mmoja mdogo
Kitunguu maji ------.kimoja
Chumvi------------nusu kijiko cha chai
Pilipili--------------robo kijiko cha chai
Bizari--------------nusu kijiko cha chai
Baking soda--------kijiko cha chai
Unga wa ngano-----kijiko kikubwa
Mafuta kwa ajili ya kuchomea/kaangia
*Namna ya kutayarisha
1. Roweka mbale za kunde kwenye maji kwa kiasi cha masaa 12
2. Chuja maji na usage kunde ama kwa food processor, blender, jiwe au kinu hadi zibakie vipande vidogo vidogo sana.
3. Kata kotmiri/giligilani, mchicha na kitunguu katika vipande vidogo vidogo
4. Tia chumvi, pilipili na bizari
5. Tia baking soda na unga wa ngano
5. Changanya vyote kwa pamoja kwenye bakuli
Weka mafuta kwenye karai yakishapata moto (medium heat), tengeza madonge ya badjia zako uchome
Zikigeuka rangi ya kahawia, toa kwenye mafuta.
Chuja kwenye chujio/chanja au paper towels
Tayari kwa kuliwa pamoja na chatne
*Nimejuta kuchangia kwenye hii thread